Ni Kitendo cha Nadra sana kuwaona Askari wa Uingereza Special Air Service (SAS) na Navy Seals

Ni Kitendo cha Nadra sana kuwaona Askari wa Uingereza Special Air Service (SAS) na Navy Seals

Nchi kam zakwetu huenda kuwa tunazo. Maybe hawana training kama ya wenzetu.
The thing is hiv vikosi ni vya siri sana kias kwamba members wa huko hawajulikani majina yao.

Uwa wanajulikana baadae wakishatoka nje ya jeshi. Kustaaf au kuacha.

Mfano kuna kikos maalum cha polis kutoka kenya kinaitwa GSU(general security unit) a.k.a recce. Hawa jamaa wamekuja kujulikana kwenye tukio la westgate. Hakuna ambae alikuwa akifaham existence yao.

Vikosi vipo. Ila vinafichwa sana kwa usiri mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
GSU inafahamika sana Kenya toka miaka ya 90ni kama FFU hapa bongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vifo 21+ bado mnawasifia! Kenya iongeze nguvu kwenye intelijensia ya nchi haya matukio yakome bila kupoteza maisha sio kusifia upuuuzi kisa tu mzungu kafanya
 
Mkuu huwa naheshimu mawazo yako lakini nahisi leo umeandika upuuzi. Hapo hatishii kuua anakwenda kuyaua magaidi, ndio maana yupo full kivita.

Huu uzi sio wa siasa zetu za CCM na CDM, mheshimu aliyeupandisha jukwaani.
Hujielewi na wala hujamuelewa malcom

Hivi shule ulipelekwa kujaza taka kichwani au

Amekuelimisha kazi ya walinzi sio kubinya watu mbavu wewe unakasirika

Certified Idiot
 
Mkuu sijakuelewa unamaanisha nini!. Uzi unahusiana na huyo SAS member wewe unakuja na habari zisizo na kichwa wala miguu!.

Au ndio yale madhara ya Makonda kuruhusu watu wapige kinywani 24/7?.
Wewe ndio Tahira uliyeanza kuandika habari za mzenji mlinzi

Madhara ya kuzaliwa kwa bahati mbaya ndio akili Kama zako
 
Mazee nimejiuliza kwanini Kenya Safari hii imewadhibiti haraka Magaidi Kumbe Kulikua kuna hawa Jamaa wanaotoka katika Most Elite Army Units on Earth

Tukianza na Navy Seal hawa ni Elites Army unit ya Marekani Wanao operate Katika Sea, Air na Land (combat) Interview na Mafunzo ya Navy Seal ni Magumu kuliko kikosi chochote cha Jeshi Ulimwenguni ni Vigumu sana kupambana nao wanajua Sana Kutumia Silaha na Kujilinda kwa kutumia miili yao Katika Tukio la Dusit walikuepo Navy Seal

Kuna British Special Air Service (SAS) hawa huwa hawaonekani Hovyo ni moja ya Vikosi bora wakiwa wamebobea katika mambo ya Kupambana na Ugaidi, na Kuokoa Mateka katlka Tukio la Dusit alikuepo mmoja ambaye alifika na Gari yenye namba za Ubalozi Akiwa na Mavazi ya Kulinda Mwili na Silaha na Alipambana na Magaidi Direct Mpaka Waingereza wenyewe wanashangaa kuwaona SAS wakipambana mchana kwani huwa wanapenda sana kufanya shughuli zao usiku.

SAS na Navy Seals ni watu waliondoka bila hata mkwaruzo wowote.

SAS huyu ana Kisu kipo tumboni hapo kinaonekana hapo kwa ajili ya mapambano ya Mkono kwa Mkono ana Pisto ana Hiyo Bunduki inayoitwa Modified Colt Canada Rifle Japo kichwani hana Helment huku akiwa katupia Jeans.
View attachment 997444

View attachment 997630

Najiuliza Kwenye Nchi zinazoendelea Elites Forces Unit kama hizi huwa zipo? Je ni kutokana na Uonevu wa Alshaabab Nchini Kenya Waliombwa waanzishe makazi yao nchini Kenya?
huku kwetu kukundi kama hicho kinaitwa WASIOJULIKANA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la rais kutojua vikosi vilivyoko nchini wake halijakaa sawa,unajua rais wa nchi ndio mkuu wa agent za ujasusi wa nchi husika,sasa kama majasusi wasijue vikosi vilivyoko nchini kwao hao ni majasusi au ni mgambo wa jiji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inatokea mkuu. Lakin inategemea na muundo wa serikali yenyewe.
Kwa mfano USA ..CIA ina secret branches... ama vitengo vidogo vilovyoko chini yake. Hiv vitengo ni vya siri sana.. na hata budget yake huitwa black budget only members DOJ wanajua jamaa wanapokea kias gani.
Hiv vikos ni siri.. rais anaweza kuvisikia lakin hata aisijue members wake ni akina nani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mazee nimejiuliza kwanini Kenya Safari hii imewadhibiti haraka Magaidi Kumbe Kulikua kuna hawa Jamaa wanaotoka katika Most Elite Army Units on Earth

Tukianza na Navy Seal hawa ni Elites Army unit ya Marekani Wanao operate Katika Sea, Air na Land (combat) Interview na Mafunzo ya Navy Seal ni Magumu kuliko kikosi chochote cha Jeshi Ulimwenguni ni Vigumu sana kupambana nao wanajua Sana Kutumia Silaha na Kujilinda kwa kutumia miili yao Katika Tukio la Dusit walikuepo Navy Seal

Kuna British Special Air Service (SAS) hawa huwa hawaonekani Hovyo ni moja ya Vikosi bora wakiwa wamebobea katika mambo ya Kupambana na Ugaidi, na Kuokoa Mateka katlka Tukio la Dusit alikuepo mmoja ambaye alifika na Gari yenye namba za Ubalozi Akiwa na Mavazi ya Kulinda Mwili na Silaha na Alipambana na Magaidi Direct Mpaka Waingereza wenyewe wanashangaa kuwaona SAS wakipambana mchana kwani huwa wanapenda sana kufanya shughuli zao usiku.

SAS na Navy Seals ni watu waliondoka bila hata mkwaruzo wowote.

SAS huyu ana Kisu kipo tumboni hapo kinaonekana hapo kwa ajili ya mapambano ya Mkono kwa Mkono ana Pisto ana Hiyo Bunduki inayoitwa Modified Colt Canada Rifle Japo kichwani hana Helment huku akiwa katupia Jeans.
View attachment 997444

View attachment 997630

Najiuliza Kwenye Nchi zinazoendelea Elites Forces Unit kama hizi huwa zipo? Je ni kutokana na Uonevu wa Alshaabab Nchini Kenya Waliombwa waanzishe makazi yao nchini Kenya?
kwa miaka mingi sasa Kenya kuna millitary base za uingereza, ila kwa kutokujua au kubisha kwa makusudi wakenya wanabisha nchi yao haina tofauti sana na koloni la uingereza, uchumi mkubwa wa kenya upo owned na ulaya kwa hiyo kwao siyo hasara kuilinda kenya kwa gharama yeyote ili kiukweli kulinda masilahi yao na si ya makwabwela wa kenya. TUMWOMBENI MUNGU SANA KWA HILI TUPO HURU
 
Good basi alikuwa at right place at a right time. Nawa admire SAS. Tough straight. Hawana muda wa video kama navy seals.
Correction huyu jamaa ni mmoja wa ma trainer waliopo Kenya. Hapa UK kaitwa Hero kwenye vyombo vya habari na wameweka sababu ya yeye kuwepo katika hiyo operation

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unavyosema Navy Seals hawako fit kihivyo mimi ndiyo napata ukakasi kabisa. Maana historia inatuambia kwamba Navy Seals walianzishwa baada ya Delta Force kuonakana haifanyi vizuro kwenye baadhi ya maeneo. Mathalani, nadhani katika dunia hii ya leo vifaa mbali na mazoezi ni moja ya sababu ya kikosi kuwa imara. Hivi kuna kikosi cha makomandoo ambacho kina vifaa vya ajabu kama Navy Seals ? Mwanajeshi wa kawaida wa Marekani akiwa amevaa full gear siyo chini ya milioni 40 za kitanzania (Do your research). Hapa ndipo wanapokuwa mbele ya vikosi vingine duniani.

Lakini sasa nakubaliana na wewe kwamba SAS ni hatari kwenye mambo mengi kwasababu tofauti kabisa na kikosi kingine chochote cha makomando hapa duniani SAS ndicho kikosi kilichopigana vita ya pili ya dunia na kufanikiwa kuonyesha umahiri wa hali ya juu sana.

SAS is ana amalgamation of multiple military units that were under the shadow of the British Empire. Wanahistoria wanasema hivi, Uingereza kama lilivyokuwa dola la Mrumi alikuwa akivamia nchi na kikuta kwamba kuna vikosi vyenye ustadi mkubwa wa kupigana. Alikuwa anachukua ujuzi huo na kufundishia jeshi lake. Alifanya hayo mambo Scotland ambako wanajeshi wake walikuwa wanajua sana vita vya msituni, hapa akatengeneza the Levat Scouts. Akafanya hivyo British India ambako wanajeshi wa Nepal na India wale walikuwa na utaalamu wa pekee sana na Uingereza akatengeza The Ghurkas.

Baada ya kuwatwanga makaburu kule Afrika Kusini, Uingereza alishangazwa sana na ujuzi wa makomando wa kikabiru. Akaamua kuuchukua na kujifunza, vita ya kwanza ya dunia inatokea. Makomando wa Kikaburu ndiyo walitumiwa kuja kupigana na Mjerumani hapa Afrika Mashariki, Namibia na sehemu nyingine. Tafuta kitabu kinaitwa The Boer Commando.

Mwaka 1941 Winston Churchill alipowa mapendekezo ya kuanzisha SAS na wataalamu walishauri kwamba, kikosi hiki kiwe kinaunganisha utaalamu wa vikosi vyote ambavyo Uingereza aliwahi kuvianzisha huko nyuma. SAS ni mchanganyiko wa Ghurkas, Levat Scouts, Boer Commandos na vinginevyo.

Wanautaalamu wa hali ya juu sana, lakini hili halifai kusema kwamba Navy Seals hawana uwezo. Laiti kama Osama Bin Laden angekuwa anaongea basi angalisema hili. Japo siku hizi tena Marekani anatumia kikosi kinaitwa JSOC ambacho kinasemekana kuwa ndiyo hatari zaidi katika kushughulikia maadui wa Marekani. Afghanistani wanasema hiki kikosi kimewashughulikia sana Taliban hadi basi. Ni zao la zao la Jasusi+Ukomando...

Wenyewe hawataki kabisa kizungumziwe hata na vyombo vya habari....

Sent using Jamii Forums mobile app
JSOC sio kikosi bali ni command. Joint special operation command. Hawa jamaa ndio wako reponsible kupanga mission,execute, training for all special forces unit.
Under JSOC command.. amri zinatolewa kwa vikosi kama navy seal , delta force, amry green beret

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata TZ tunanao hao special force tena wiko vizuri tu na wameshafanya mission impossible nyingi tu sema kimya kimya tena zingine ukiambiwa huwezi amini kama zimefanywa na askari wa kawaida tu sio special force. Tuko vizuri tuendelee kuunga mkono juhudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
... nakubaliana na wewe! Kama lile lililong'ata konda kule Tunduma liko vizuri mno maana linatumia silaha "zote".
 
...Ninyi watu ninyi...!!! Kwa hiyo, shambulio la hivi majuzi ilikuwa 'practical' ya trainees wa jeshi la kenya?
====
Acheni masihara katika matukio ya hatari!
hujaelewa nini sasa, Member wa SAS alikua akitoa mafunzo katika jeshi la kenya wakati tukio linatokea, so akaamua kwenda kusaidia. Hope umeelewa
 
Huyo SAS alikuwa yuko kikazi nchini Kenya. Anatoa mafunzo. Siku ya tukio alikuwa mjini kwenye msele yake ila kwenye gari alikuwa na zana zake zote. Akavaa akawahi eneo la tukio.
... kuna majamaa hayaogopi risasi aisee! Jamaa aka-cancel plan zake zote za siku hiyo na kuwahi eneo la tukio; yuko fit balaa! Ingekuwa wale wa kwetu waliomng'ata konda wangekufa kwa kihoro papo hapo na mavitambi yao utafikiri wajawazito!
 
Ubalozin huwa kuna kila kitu. Tactical gia na silaha.
Rember tofauti na vikos vingine ex- SAS member huitwa kusaida wakat wa hatari..
So ni ishu ya sim na kuletewa vifaa vya kaz

Sent using Jamii Forums mobile app
... neno ubalozi likitajwa namkumbuka Khashogi! Balozi za Saudia zinakuwaga na visu maalum vya kuwachinjia wabaya wao na viroba vya kuhifadhi nyama baada ya kuwacharanga.
 
Hili la rais kutojua vikosi vilivyoko nchini wake halijakaa sawa,unajua rais wa nchi ndio mkuu wa agent za ujasusi wa nchi husika,sasa kama majasusi wasijue vikosi vilivyoko nchini kwao hao ni majasusi au ni mgambo wa jiji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais cheo chake ni cha muda mfupi sana while usalama wa nchi is everlasting! Kila mtu ana tabia yake; mkikutana na mropokaji anaweza hata kutoa siri kwa kujua au kutokujua; akiwa madarakani au baada ya kustaafu. So, ni sahihi wasijue.
 
Back
Top Bottom