Ni Kitendo cha Nadra sana kuwaona Askari wa Uingereza Special Air Service (SAS) na Navy Seals

Ni Kitendo cha Nadra sana kuwaona Askari wa Uingereza Special Air Service (SAS) na Navy Seals

Ila taarifa kutoka Kenya zinasema jamaa yuko Kuwa train askari wa Kenya, ila siku ilipotokea tukio na yeye alikuwepo hapo kama wateja wengine tu sasa magaid walipolianzisha ikabidi aende kwenye gari yake na kuchukua vifaa kwa ajili ya mapambano maana inasemekans popote anapoenda anakuwa full equipped.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Correction. SAS huwa ndio unit bora zaid..
Selection ya SAS ni ngumu sana kuliko Navy seals.

SBS(special boat services). Hawa ni pacha wa SAS ila wamebobea kwenye maji.

Huyo unae muona hapo alikuwa off duty, au anaweza kuwa ex-SAS since wanaruhusiwa kustaaf ktk umri mdogo.
Huyu bwana alikuwepo eneo hilo wakati panavamiwa.. si kwamba alitumwa au kenya iliomba msaada hapana.
Ni tukio limemkuta akaamua kutoa msaada since yeye ni expert kwenye counter terrorism.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuweka point vizuri, kama wengine walivyosema, huyo mwanajeshi anawafanyia mafunzo special unit ya Kenya. Anatokea Uingereza. Uingereza na Kenya wanaushirikiano wa karibu sana kwenye mafunzo ya kijeshi, hata mwaka jana mtoto wa malkia wa Uingereza aliwatembelea wanajeshi wenzake waliokuwa wanafanya mafunzo ya pamoja alipoitembelea Kenya.

Kuwa kwake pale ni kwa sababu walioitwa ni wanafunzi wake na kama ujuavyo wanajeshi marafiki huwa wana umoja Sana. Sio kweli kwamba alikuwa kwenye eneo la tukio kabla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes ni SAS member. Lakin inategemea kama ni yuko in active duty.. au yuko likizo.. au amestaaf.
Kumbuka hawa jamaa wakistaaf nchi bado inawatambua. Huwa wanatembea na ile elite patch ya SAS.. likitokea la kutokea basi wajue ni mwenzao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo yupo kwa ajili ya training kwenye Kenya special forces
Nilisoma kwenye gazeti la Mirror UK wanavyo msifia ni balaa
Jamaa lilimkuta tu tukio hilo akiwa na mambo yake ndipo akarudi kwenye gari lake ambapo zana zake zilikuwa humo.
Akavaa na kuchukua silaha na kuanza kutoa maelekezo kwa jeshi la kenya
Yaani jamaa alishika usukani mpaka anamaliza mission

Sent from my SM using Tapatalk
 
Nchi kam zakwetu huenda kuwa tunazo. Maybe hawana training kama ya wenzetu.
The thing is hiv vikosi ni vya siri sana kias kwamba members wa huko hawajulikani majina yao.

Uwa wanajulikana baadae wakishatoka nje ya jeshi. Kustaaf au kuacha.

Mfano kuna kikos maalum cha polis kutoka kenya kinaitwa GSU(general security unit) a.k.a recce. Hawa jamaa wamekuja kujulikana kwenye tukio la westgate. Hakuna ambae alikuwa akifaham existence yao.

Vikosi vipo. Ila vinafichwa sana kwa usiri mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Recce ni kikosi ndani ya GSU. Vikosi vya Recce na flying squad vinafahamika kwa raia. Na nilazima watu wafahamu hivi vikosi kwa sababu ya kujenga hofu kwa wabaya wa nchi na majambazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mazee nimejiuliza kwanini Kenya Safari hii imewadhibiti haraka Magaidi Kumbe Kulikua kuna hawa Jamaa wanaotoka katika Most Elite Army Units on Earth

Tukianza na Navy Seal hawa ni Elites Army unit ya Marekani Wanao operate Katika Sea, Air na Land (combat) Interview na Mafunzo ya Navy Seal ni Magumu kuliko kikosi chochote cha Jeshi Ulimwenguni ni Vigumu sana kupambana nao wanajua Sana Kutumia Silaha na Kujilinda kwa kutumia miili yao Katika Tukio la Dusit walikuepo Navy Seal

Kuna British Special Air Service (SAS) hawa huwa hawaonekani Hovyo ni moja ya Vikosi bora wakiwa wamebobea katika mambo ya Kupambana na Ugaidi, na Kuokoa Mateka katlka Tukio la Dusit alikuepo mmoja ambaye alifika na Gari yenye namba za Ubalozi Akiwa na Mavazi ya Kulinda Mwili na Silaha na Alipambana na Magaidi Direct Mpaka Waingereza wenyewe wanashangaa kuwaona SAS wakipambana mchana kwani huwa wanapenda sana kufanya shughuli zao usiku.

SAS na Navy Seals ni watu waliondoka bila hata mkwaruzo wowote.

SAS huyu ana Kisu kipo tumboni hapo kinaonekana hapo kwa ajili ya mapambano ya Mkono kwa Mkono ana Pisto ana Hiyo Bunduki inayoitwa Modified Colt Canada Rifle Japo kichwani hana Helment huku akiwa katupia Jeans.
View attachment 997444

Najiuliza Kwenye Nchi zinazoendelea Elites Forces Unit kama hizi huwa zipo? Je ni kutokana na Uonevu wa Alshaabab Nchini Kenya Waliombwa waanzishe makazi yao nchini Kenya?
Weka mbali na watoto.

evarist_chahali-20190117-0001.jpeg
evarist_chahali-20190117-0002.jpeg
evarist_chahali-20190117-0003.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEAL hawako fit kiivyo. Ila SAS wako vizur.
Delta force ambao huwa wanafanya kazi kwa siri.. sometimes C.I.A huwaajiri kwa muda under SAD, kama CAG operators.
Delta force waasis wake ni SAS, new zealand SAS NZSAS, Australia.. majesh mengi europe uasis umeanza kutoka SAS. Na baadhi ya nchi za asia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unavyosema Navy Seals hawako fit kihivyo mimi ndiyo napata ukakasi kabisa. Maana historia inatuambia kwamba Navy Seals walianzishwa baada ya Delta Force kuonakana haifanyi vizuro kwenye baadhi ya maeneo. Mathalani, nadhani katika dunia hii ya leo vifaa mbali na mazoezi ni moja ya sababu ya kikosi kuwa imara. Hivi kuna kikosi cha makomandoo ambacho kina vifaa vya ajabu kama Navy Seals ? Mwanajeshi wa kawaida wa Marekani akiwa amevaa full gear siyo chini ya milioni 40 za kitanzania (Do your research). Hapa ndipo wanapokuwa mbele ya vikosi vingine duniani.

Lakini sasa nakubaliana na wewe kwamba SAS ni hatari kwenye mambo mengi kwasababu tofauti kabisa na kikosi kingine chochote cha makomando hapa duniani SAS ndicho kikosi kilichopigana vita ya pili ya dunia na kufanikiwa kuonyesha umahiri wa hali ya juu sana.

SAS is ana amalgamation of multiple military units that were under the shadow of the British Empire. Wanahistoria wanasema hivi, Uingereza kama lilivyokuwa dola la Mrumi alikuwa akivamia nchi na kikuta kwamba kuna vikosi vyenye ustadi mkubwa wa kupigana. Alikuwa anachukua ujuzi huo na kufundishia jeshi lake. Alifanya hayo mambo Scotland ambako wanajeshi wake walikuwa wanajua sana vita vya msituni, hapa akatengeneza the Levat Scouts. Akafanya hivyo British India ambako wanajeshi wa Nepal na India wale walikuwa na utaalamu wa pekee sana na Uingereza akatengeza The Ghurkas.

Baada ya kuwatwanga makaburu kule Afrika Kusini, Uingereza alishangazwa sana na ujuzi wa makomando wa kikabiru. Akaamua kuuchukua na kujifunza, vita ya kwanza ya dunia inatokea. Makomando wa Kikaburu ndiyo walitumiwa kuja kupigana na Mjerumani hapa Afrika Mashariki, Namibia na sehemu nyingine. Tafuta kitabu kinaitwa The Boer Commando.

Mwaka 1941 Winston Churchill alipowa mapendekezo ya kuanzisha SAS na wataalamu walishauri kwamba, kikosi hiki kiwe kinaunganisha utaalamu wa vikosi vyote ambavyo Uingereza aliwahi kuvianzisha huko nyuma. SAS ni mchanganyiko wa Ghurkas, Levat Scouts, Boer Commandos na vinginevyo.

Wanautaalamu wa hali ya juu sana, lakini hili halifai kusema kwamba Navy Seals hawana uwezo. Laiti kama Osama Bin Laden angekuwa anaongea basi angalisema hili. Japo siku hizi tena Marekani anatumia kikosi kinaitwa JSOC ambacho kinasemekana kuwa ndiyo hatari zaidi katika kushughulikia maadui wa Marekani. Afghanistani wanasema hiki kikosi kimewashughulikia sana Taliban hadi basi. Ni zao la zao la Jasusi+Ukomando...

Wenyewe hawataki kabisa kizungumziwe hata na vyombo vya habari....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Correction. SAS huwa ndio unit bora zaid..
Selection ya SAS ni ngumu sana kuliko Navy seals.

SBS(special boat services). Hawa ni pacha wa SAS ila wamebobea kwenye maji.

Huyo unae muona hapo alikuwa off duty, au anaweza kuwa ex-SAS since wanaruhusiwa kustaaf ktk umri mdogo.
Huyu bwana alikuwepo eneo hilo wakati panavamiwa.. si kwamba alitumwa au kenya iliomba msaada hapana.
Ni tukio limemkuta akaamua kutoa msaada since yeye ni expert kwenye counter terrorism.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kenya walikuwepo SAS, US navy seal na wengine. Tunashukuru tukio limeisha, poleni wafiwa.

Hero SAS soldier and US Navy Seals 'helped battle Islamist terrorists attacking Kenyan hotel' | Daily Mail Online

Hero US Navy SEALs stormed Kenyan hotel and exchanged fire with Islamist terrorists | Daily Mail Online
 
Mkuu Troll historia inasema kwamba vikosi vya ulinzi na usalama vya Marekani kuanzia Intelijensi (OSS na CIA) hadi jeshi vilipata mafunzo makubwa sana kutoka kwa Muingereza. Yaani kama ambavyo Tanzania tulikuwa tunategemea Cuba, Urusi na Uchina, basi Marekani alikuwa anategemea sana Uingereza......

Uwezo wa SAS ni mkubwa sana, sijui hata kwanini imekuwa hivyo. Lakini hata wanajeshi wa nchi nyingine wanasema jamaa wako vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mob
ile app

Upo sahihi, ndio best of the best, Crème de la crème,

USA, Israel, wamejifunza hapo.
 
Hata TZ tunanao hao special force tena wiko vizuri tu na wameshafanya mission impossible nyingi tu sema kimya kimya tena zingine ukiambiwa huwezi amini kama zimefanywa na askari wa kawaida tu sio special force. Tuko vizuri tuendelee kuunga mkono juhudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Au za kule Comoros mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo SAS yupo kwa ajili ya kuwapa mafunzo Wakenya nao wana kikosi chao cha kujilinda na ugaidi...Na huyo jamaa anatembea kwenye Gari yake akiwa na vifaa alivyovaa wakati wote na alichonishangaza yeye havai element sijui kichwani ila siraha anayokua nayo ni kubwa sana na ana shabaha sana kila risasi inafika kwenye Target yake na amewaokoa wakenya wengi na ndie aliefanya magaidi kwenda kujificha gorofa ya saba maana alikua haogopi kitu anaingia chumba kwa chumba mwenyewe wakenya wakiwa mbali na kutoka nje kuangalia ramani ya jengo...jamaa yupo fit sana aisee..ameiva vizuri kwa kweli..
Ulikuwepo au umeadithiwa mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mleta mada punguza mahaba!! Eti SAS na SEAL ndiyo vikosi bora ulimwenguni!! Vikosi vya wengine unavijua?? Au series na propaganda za kimarekani zimekupa upofu???
Operesheni nyingi tu za SEAL zimeshindwa, tena huko Somalia, Yemeni ,Afghanistan n.k.
Poa mkuu basi kikosi bora Simba Sports Club. Kikosi kipana. Happy?!
 
Nani amekudanganya kwamba hao magaidi waliuwawa ama kuzibitiwa?wakenya wanacheza movie zao kama ule uongo wa jeshi kuwadhiti magaidi kwenye tukio LA westgate
Kwahiyo mkuu tusiwaamini waliokuwa kwenye tukio wanaosema magaidi wameuwawa tukuamini wewe ambae uko Tandale Kwa Mtogole muda huu?!
 
Mazee nimejiuliza kwanini Kenya Safari hii imewadhibiti haraka Magaidi Kumbe Kulikua kuna hawa Jamaa wanaotoka katika Most Elite Army Units on Earth

Tukianza na Navy Seal hawa ni Elites Army unit ya Marekani Wanao operate Katika Sea, Air na Land (combat) Interview na Mafunzo ya Navy Seal ni Magumu kuliko kikosi chochote cha Jeshi Ulimwenguni ni Vigumu sana kupambana nao wanajua Sana Kutumia Silaha na Kujilinda kwa kutumia miili yao Katika Tukio la Dusit walikuepo Navy Seal

Kuna British Special Air Service (SAS) hawa huwa hawaonekani Hovyo ni moja ya Vikosi bora wakiwa wamebobea katika mambo ya Kupambana na Ugaidi, na Kuokoa Mateka katlka Tukio la Dusit alikuepo mmoja ambaye alifika na Gari yenye namba za Ubalozi Akiwa na Mavazi ya Kulinda Mwili na Silaha na Alipambana na Magaidi Direct Mpaka Waingereza wenyewe wanashangaa kuwaona SAS wakipambana mchana kwani huwa wanapenda sana kufanya shughuli zao usiku.

SAS na Navy Seals ni watu waliondoka bila hata mkwaruzo wowote.

SAS huyu ana Kisu kipo tumboni hapo kinaonekana hapo kwa ajili ya mapambano ya Mkono kwa Mkono ana Pisto ana Hiyo Bunduki inayoitwa Modified Colt Canada Rifle Japo kichwani hana Helment huku akiwa katupia Jeans.
View attachment 997444

View attachment 997630

Najiuliza Kwenye Nchi zinazoendelea Elites Forces Unit kama hizi huwa zipo? Je ni kutokana na Uonevu wa Alshaabab Nchini Kenya Waliombwa waanzishe makazi yao nchini Kenya?
Jamani kabla hamujaleta uzi mfanyege research kujua sababu ya hao watu kuwepo Katika eneo la tukio.

Kenya kuna kikosa kidogo cha hao jamaa kutrain wanajeshi Kenya. Kilichofanyika walienda kuwasaidia wanafunzi wao sababu kuna Waingereza na Wamarekani Wahanga pia.

Al shabab ni tishio kubwa hivyo wanawasaidia wakenya kupambana nao.
 
Back
Top Bottom