Ni kitu gani ambacho hupendi kukifanya katika maisha yetu ya kila siku lakini unafanya kwakuwa huna namna

Ni kitu gani ambacho hupendi kukifanya katika maisha yetu ya kila siku lakini unafanya kwakuwa huna namna

Sipendi mizunguko isiyo na ulazima

Sipendi kupika nikiwa ghetto

Sipendi kuosha vyombo na sabuni ya kipande

Sipendi kuvaa vaa masweta ila inanilazimu sababu ya mkoa niliopo
Kupika nitakusaidia maana ndio kitu napenda kuliko zote.

Kuonsha vyombo sipendi ila hakuna namna.

Hama uko mama uje huku kwetu ..

Kwa pamoja tu jipe pole hakuna namna
 
Mtu akija akakupa offer ya kukutoa out mkanywe wine utakataa
Wewe unazungumzia 🍷..

Mtu anataka kukutoa Sunday brunch na unachomoa..sembuse wine..

Ila hii huwa inatokea mara chache sna tena kwa mtu ambae hujamwelewa🤪🤪
 
Nakataa vizuri tu, nishawahi kukataa offer ya lunch Mount Meru hotel nikabaki ghetto mchana huo nikapika ugali na kabichi.
Aise kuna mtu alitokea nielewa sana yuko vizuri tu lkni mimi Habari sina....
Mara yakwanza nilimkuta sehemu akaniomba nipate japo juice nikakubali..

Siku nyingine akaniomba anitoe dinner sehemu..😅😅waaaaaiiiii nilichomoa aise nikalala nyumbani tena niliishia kula tango na chumvi 😅😅

Kwa hiyo huwa inatokea kwa mtu ambae hautikisi mtima😅😅
 
sipendi kukatisha usingizi saa10 ajili ya kujiandaa kwenda job, jambo hili lanikwaza sana ila kwa kua hakuna jinsi nafanya tu
Pole sana mkuu jitahidi upate kampuni yako hakuna namna.

Na cha kusikitisha ni kwamba..siku ukija kuwa na ofisi yako mwenyewe utaamka mapema kuliko ulivyokuwa unaamka wakati umeajiriwa
 
Utaskia jamaa ana michongo kinoma yani ni Engineer kule Dodoma. Ukija mcheki mwamba mwenyewe hata deal ya laki 3 hatuwezi fanya 🤣🤣🤣
Yani tena nitakuunga kuliko roast beef la kitanga..akichomoa labda si mimi😅😅na mkwanja lazima uniongezee😅😅dadeki
 
Hamna kitu sipendi kama kula mshahara wote week moja tu baada ya kuingia ila ndo ila ndo ivyo kilimanjaro lager ni tamu ntafanyaje sasa. Lazma kurudishia mwili shukrani kidogo kwa kazi ngumu . All in all we are sure of where we are coming from and where we are but we are not sure about tomorrow.
Mkuu acha kujiendekeza kwa kula mshahara wote..
Ole wako wa mwezi huu uule wote..utanitambua😅😅
 
Nikipitaga karibu na makaburi huwa sipend kusoma majina ya kwenye misaraba ila najikutaga tu nimeisha yasoma
 
Back
Top Bottom