Ni kitu gani ambacho kiliwahi kukutoa ushamba?

Ni kitu gani ambacho kiliwahi kukutoa ushamba?

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Umenikumbusha hii kitu aisee, nami smartphone ilinitoa ushamba kipindi hicho ndio zimeingia ingia, sijui ilikua nokia n ngapi vile!!! Kama siku 4sikupokea simu kila ikiita nashindwa kuipokea maana mpaka uislide button ndio ipokeleke, sasa ikiita kila nikibonyeza haipokeleki, kuuliza naona aibu alafu pia nashindwa wa kumuuliza maana wengi hawakuwa nazo, nakumbuka niliulizia watu kama wawili wakawa hawajui. Basi siku hiyo akili ikanijia ikabidi nisome manual ndio nikaelewa. Daah nilivyoweza haki nilijichekaaa.
A haha kweli ushamba mzigo
 
Daaah siku ya kwanza kuingia kituo cha mwendokasi, nililipia nauli tena nkatoa elfu5 ili nisiambiwe nauli haitoshi, ilikuwa ni pale urafiki naenda posta nikampa mdada(mlinzi) anisaidie kuscan sasa kimbembe kupita pale mlangoni nkadhani kile kichuma kinafungukia juu. Nilinyanyua lile chuma mpaka mrembo mmoja akanionea huruma akaja kusogeza tu mlango ukafunguka. Kwa aibu nilokuwa nayo nilisubiri mpka watu wote mle ndani ya kituo wakaondoka ndo na mimi nikapanda gari
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Elevator bhana iliniacha hoi way back! Nilipanda na kushuka zaidi ya mara tano bila kujua uelekeo wangu haha hah mwisho wa siku nikajikuta ground floor hah hah mlinzi alinichapa sana bila kujua nilikusudia kufanya nini katika elevator ile! hiyo ilikuwa pale data star enzi hiyo! sitasahau hah hah
 
Duh huwa nikirudi kjjn huwa simuulizii kabisa. Ila kakaake niko naye hapa town tunapiga kazi ni mt mzima . Nahs demu keshaolewa
 
khaa siku ya kwanza kutazama kideo tena ilikuwa picha ya Yesu...hapo tunekusanywa uwanja wa ccm huko kileji...
 
Nilialikwa birthday ya rafiki yangu halafu wakaserve table wine zile za box kwa chini kidogo unaivuta kanatoka ka koki kapo kama bomba hivi ambako ndo unafungua kujimiminia sasa mimi kwa vile nilipewa kwanza.
Nikaanza hangaika toboa juu nikizani lile box ndani kuna chupa ya wine!!..Kuna dada mmoja akanishtua hapo box juu lipo nusu tayari [emoji2]..
Aseh sipendi kaa siti ya mbele kwenye sherehe tena!!...
 
Back
Top Bottom