Ni kitu gani ambacho kiliwahi kukutoa ushamba?

Ni kitu gani ambacho kiliwahi kukutoa ushamba?

Siku ya kwanza kwenda dukani kununua condom nlienda pharmacy nkamkuta mama, khah nliulizia dawa za aina mbali mbali nkachukua dawa za minyoo, magnesium mwishowe akanambia mbona sijiamini nkamwambia anipe ndom alicheka hatar haf akanipa bure nliskia aibu had kutoka nje. Bas kila mara akikutana na mimi anacheka tu
 
Mimi nilienda bank kufungua account sasa nilipokuwa mle ndani kwenye arakati za kujiandikisha na nn muda wa kutoka nakaza kuvuta mlango badala ya kusukuma daaa navuta mpk nakuja kugutuka watu wananishanga daaa kwakweli niliona aibu
Dada yangu PULL AND PUSH HUKUELEWA MAANA YAKE [emoji23] [emoji23] [emoji85] [emoji85]
 
Nakumbukia nikiwa form one oldmoshi miaka ya sabini, nikaambiwa nizime balbu ya umeme. Nilipuliza kwa mdomo kama nilivyozoea kuzima kibatari.
 
Simu yangu ya kwanza kumiliki ilikuwa Alkatel, siku tatu za mwanzo sikuwahi kuiona iki vibrate.
The other day nilikuwa naendesha baiskeli simu nikatumbukiza kwenye back pack, sijui ilijibonyeza vipi ikaita kwa vibration, kitu ambacho nilikuwa sijakitegemea kabisa.
Nikajua ntakuwa nimebeba panya au snake kabisa. Niliruka kama ninja baiskeli ikadondokea chaka lingine mimi kwenye vumbi, begi nalo nimetupia mbali kabisa..
Nikatafuta bonge la fimbo nikaanza kutoa kichapo kwa lile begi hadi niliporidhika chochote kilichomo kitakuwa kimeshakufa.
Kuja kufungua begi duuh!! simu haifai. Nilitamani kwenda kujishtaki polisi mwenyewe
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji14] [emoji14] [emoji23] [emoji23] jamaa yakweli haya un unatupangaa maana nimechekasana kama nakuona vile
 
Dada yangu PULL AND PUSH HUKUELEWA MAANA YAKE [emoji23] [emoji23] [emoji85] [emoji85]
Palikuwa hapajaandikwa kwann nisielewe kweli tena... Nenda kaangaliee tawi la Mandela kituo shuka T.O.T
 
Kwa mala ya kwanza nimeingia mjini nikitokea kijijini niliko zoea kula ugali mkubwa wa kusaza maziwa jumlisha michembe na numbu za kusombelea walio wahi kukaa kijijini mtanielewa zaid.Nilifika mjini mida ya jioni sana.Kasheshe ilikuja wakati wa msosi usiku naona zinapakuliwa ndizi nakuhifadhiwa kwenye ile kitu mnaita hotpot baada ya hapo ikawekwa mezani then nikaona kilamtu anachukua mule anaweka kwenye sahani yake anakaa kwenye kochi nakuanza kula nikawaza ndotunakulaa ama nikama kibuludisho kwa mgeni kwasababu sikuamini kama zilendizi zilizopikwa zinaweza kuwa chakula cha usiku maana ningeweza kuzila zilendizi zote nakuzimaliza bila kushiba.Bas zamuyangu ikafika nikachukua sahani wakawa wananishangaa maana nilichukua za kutosha nikala zikaisha badae naona watu wanaingia kulala ohooo nikaanza kupata wazo kuwa inawezekana nimsosi wa usiku kweli bado nilikuwa sjaamini sababu baba yangu mdogo ambae ndo mwenyejiwangu mkuu alikuwa hajaludi toka kazini alipo lud akamwambia mkewe mgeni amekula akajibu ndio huku mimi nikiskia kauli hiyo ndonikaamini kuwa tayali baba aliniita nakuniuliza kama nimekula nikamwambia ndio ila naskia njaa balaa ikabid nipikiwe ugali mkubwa usiku huo.nyumbanzima nilionekana wa ajabu
 
Nilialikwa birthday ya rafiki yangu halafu wakaserve table wine zile za box kwa chini kidogo unaivuta kanatoka ka koki kapo kama bomba hivi ambako ndo unafungua kujimiminia sasa mimi kwa vile nilipewa kwanza.
Nikaanza hangaika toboa juu nikizani lile box ndani kuna chupa ya wine!!..Kuna dada mmoja akanishtua hapo box juu lipo nusu tayari [emoji2]..
Aseh sipendi kaa siti ya mbele kwenye sherehe tena!!...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ata sikushangai!!! Mara ya kwanza kupanda ilikua airport Addis Ababa... Yaani ile timing ya kuingia na kutoka kwenye ngazi inanisumbua.... Sijatumia tena escalators naogopa kuaibika siku [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji38] [emoji38] [emoji38] mimi juzi nilienda Samora pale jengo jipya la NHC bwana wee nikaziachilia mbali.
 
Baada ya kutembelea ukweni na kupiga menyu ya maana na kuvimbiwa mbaya,nikauliza msalani nikaonyeshwa,si nikaingia na kushusha mzigo wa hatare,sasa si unajua tena vyoo vya kizungu vyataka kufrash maji mengi,nmeshamaliza shughuli bhana,si nikavuta ile kamba,maji hola[emoji15] kumbe yamekatika kitaaambo!!ooh balaa hili jamani[emoji30] kucheki kwenye ndoo ,nmenawa yameisha!!asalaalee!!nikatoka nikatafute maji japo nimuombe beki 3 kiasi tu nikafrash!!,ile niko namnong'oneza beki 3,naona shemeji mkubwa(dada mtu) nae anaelekea msalani!!hatareee[emoji125] [emoji125] si akaingia bhana!!pliz sitaki kukumbuka zaid ile aibu!!nini kilifuata?ntarudi[emoji124] [emoji124]
Hahahaha hii tamu sana hapo mpka nguvu za kiume zinapungua
 
kulia uma sijui visu sijui vijiko na vikoro koro juu ya meza vilinitoa ushamba kweli.mm sezoea hayo mambo .ikabidi mzee meza nzima niliineza msosi watu vepe wananiangalia ninavyoaibika na vile videmu vizuri vinanicheka mhahahahha
 
Je nikitu gani ambacho kiliwai kukutoa ushamba katika maisha yko unacho kikumbuka..

Mimi ni pikipiki ilinitoa ushamba sana hicho kitu enzi hizo lakin
weka na chako twende sawa
Siku nimeambiwa nikwangue nazi niweke kwenye mboga kitu samaki Baada ya kumaliza kuikuna badala ya kuichuja na kutoa makapi kitu nilikiweka kama kilivyo due ilibidi itafutwe mboga nyingine kuokoa jahazi
 
😀😀😀😀
Siku nimeambiwa nikwangue nazi niweke kwenye mboga kitu samaki Baada ya kumaliza kuikuna badala ya kuichuja na kutoa makapi kitu nilikiweka kama kilivyo due ilibidi itafutwe mboga nyingine kuokoa jahazi
mliomba mboga nn?
 
Back
Top Bottom