1 Petro 3:10-11 “Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya, atende mema;
Atafute amani, aifuate sana.”
Unapokuwa hodari ndani yako (moyoni), maana yake ni kwamba unalitunza Neno na hilo Neno linakupa Nguvu. Mabaya yanapokujia hiyo nguvu inakuwa kama ngao kuzuia mabaya yasiingie ndani ya moyo wako na hata kuleta uchungu.
Unakuta mtu kwa sababu kuna mtu amemkwaza haendi kanisani, mpendwa unapaswa kutambua kuwa ni rahisi mno kwenda kuzimu kama wewe sio hodari ndani yako, kwa nini?
Kwa sababu ibilisi atawaruhusu watu wakukosee ili uwe na hasira na uchungu.
Mara zote uchungu unaondoa tumaini ndani yako, Imani na upendo, na kama ukikosa hayo matatu, wewe umekwisha kabisa katika maisha ya kiroho. Kwa sababu maisha ya kiroho yako ndani ya tumaini, Imani na pendo, ikiwa hayo matatu yakiondoka kwako kwa sababu ya uchungu basi unapoteza Ukristo wako.
Ndiyo maana unaweza kuona unapokuwa unafanya biashara na huku unabeba uchungu ndani yako hatua kwa hatua ibilisi atawaleta watu wakukosee na ukiwa na uchungu biashara yako inaanza kudidimia hata kufa kabisa.
Ingawa una mume mzuri kwa sababu umeruhusu uchungu huo uchungu unakuwa kama ukuta kati yako na mumeo, wakati mwingine anaweza akawa sio mume au mke wako amekukosea ni mtu mwingine amekukosea lakini kwa sababu umebeba uchungu unatengeneza ukuta kati yako na mume au mke wako na ghafla mnaanza kugombana na matokeo yake mnaweza hata kuachana kabisa, kwa sababu ya uchungu.
Ukiona hali hiyo tatizo sio mume wako au mke wako tatizo ni uchungu uliouweka moyoni. Kwa nini leo kuna vita ndani ya ndoa na wakati zamani mlikuwa mnafanya vitu vile vile mnavyofanya leo na hakukuwa na vita? Kwa sababu ya uchungu mliouruhusu kukaa ndani yenu. Kama mnataka kuiona furaha, amani na mafanikio msiruhusu uchungu katika maisha yenu.
#chomozanews