zink
JF-Expert Member
- Sep 18, 2021
- 1,208
- 2,352
Nakumbuka mwaka 2016 kipindi icho nikiwa kidato cha 3 nilipata demu flani hivi na kusema ukweli nilitokea kumpenda sana huyu mwanamke, kiasi kwamba nikawa namchunguza maana nilihisi uwenda akawa anatoka na wadau wengine, hali hii ilinipelekea nikawa nagoogle sana kuhusu dalili za mwanamke anaekupenda, mara nagoogle dalili za mwanamke mwenye wapenzi ya mmoja, sasa katika kugoogle nikawa napata majibu ambayo yanayonipeleka moja kwa moja kwenye jukwaa la mapenzi, hivyo nikawa mlevi wa jukwaa la mapenzi.
Pia mwaka 2018 kipindi nipo A level nikapata tena demu mwingine aisee nae nae nilimpenda sana na nikawa namfatilia sana hivyo nikajikuta nagoogle sana mada za mapenzi ambazo majibu yake nikawa nayapata kwenye jukwaa la mapenzi nahisi kwa watu wanaongoza kufatilia mada za mapenzi ni mimi maana nilikua kama mlevi tena wa mapenzi.
Mwisho kabisa siwezi kusahau jukwaa la mambo ya technology maana nilikua nalifatilia sana mambo ya simu, laptop na games mbali mbali, naweza kusema kwa kifupi mambo ya mapenzi na technology ndio yamenileta humu jf.
Karibuni sana wadau na nyie mueleze sababu zipi ziliwapelekea mpaka mkajiunga na mtandao wa jamiiforum.
NAWASILISHA.