Ni kitu gani kilikupelekea mpaka ukajiunga na mtandao wa jamiiforum

Ni kitu gani kilikupelekea mpaka ukajiunga na mtandao wa jamiiforum

zink

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2021
Posts
1,208
Reaction score
2,352
Nakumbuka mwaka 2016 kipindi icho nikiwa kidato cha 3 nilipata demu flani hivi na kusema ukweli nilitokea kumpenda sana huyu mwanamke, kiasi kwamba nikawa namchunguza maana nilihisi uwenda akawa anatoka na wadau wengine, hali hii ilinipelekea nikawa nagoogle sana kuhusu dalili za mwanamke anaekupenda, mara nagoogle dalili za mwanamke mwenye wapenzi ya mmoja, sasa katika kugoogle nikawa napata majibu ambayo yanayonipeleka moja kwa moja kwenye jukwaa la mapenzi, hivyo nikawa mlevi wa jukwaa la mapenzi.

Pia mwaka 2018 kipindi nipo A level nikapata tena demu mwingine aisee nae nae nilimpenda sana na nikawa namfatilia sana hivyo nikajikuta nagoogle sana mada za mapenzi ambazo majibu yake nikawa nayapata kwenye jukwaa la mapenzi nahisi kwa watu wanaongoza kufatilia mada za mapenzi ni mimi maana nilikua kama mlevi tena wa mapenzi.

Mwisho kabisa siwezi kusahau jukwaa la mambo ya technology maana nilikua nalifatilia sana mambo ya simu, laptop na games mbali mbali, naweza kusema kwa kifupi mambo ya mapenzi na technology ndio yamenileta humu jf.

Karibuni sana wadau na nyie mueleze sababu zipi ziliwapelekea mpaka mkajiunga na mtandao wa jamiiforum.

NAWASILISHA.
 
So kipindi chote hicho karibia miaka 5 (2016-2021) ulikuwa unatumia JF kama guest hukuwahi kujiunga?

Maana bado unaonekana mgeni hata mwezi huna.
Screenshot_2021-10-16-19-29-22-422_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
 
Kidato cha tatu ulishaanza kugoogle dalili za mwanamke kukupenda/dalili za mwanamke kua na wanaume wengi,

Nawapa pole wasomeshaji wako.
Mkuu hii ipo kwa wanaume wengi wanaoanza mapenzi lazima ufatilie tu
 
Ngoja waje wajuaji waseme kumbe 2016 upo kidato Cha tatu
Wakati mnyama mkali hapa na I'd yangu ya mwendokasi
the terrible nilikua Cha mbele Yako
Ndio wazee wa humu watajua hawajui!

Mkuu maada za interigence na historical background,Siasa na mengine mengi zilinivutia Sana sababu nilikua napenda kujisomea Sana vitabu nikawa Kila nikizama google ingine baadhi ya majibu yanaangukia humu nikavutiwa Sana baadhi ya michango ya members humu,
Nikajoin baada ya kua msomaji wa muda mrefu!
Kabla ya hapo nilikua mtu wa novel sana!
 
Hongera mkuu mimi mambo ya siasa na kusoma vitabu wala sipatani navyo kabisa.
 
zamani jamii forum ilikua ina watu wenye kufikiri kwa mapana pia watu waliheshimiana kutukana matusi au kumjibu vibaya member mwenzio ilikua mwiko unapigwa ban haraka sana jf kulikua hakuna mada za upuuzi kama za fb kulikua hakuja vamiwa na watoto wasio jielewa walichoka maisha nakuja kumalizia hasira zao humu lakini sikuhizi mods wamelala mtu anamtukania wazazi member mwenzie anadunda tuu mtu anamtishia mtu anapeta tuu miko ya jf sasa hivi imekiukwa umekua mtandao wa bora liende zamani mtu unakua na hamu kabisa umalize mishe uzame jf kupata nondo za watu wanao jitambua lakini kwa sasa makasiriko vichambo kukoseana adabu kuvunjiana heshima ndio maisha ya jf mada za kupuuzwa zimejaa humu majukwaa mpaka ya great thinker yamevamiwa na watu wa hovyo mno.
 
Vijana siku hizi wana umarekani mwingi mkuuu na kuiga iga vitu.
 
Back
Top Bottom