Binafsi nilikua nasoma Jamii Forum kama guest lakini kuna dada alinivutia sana sijui siku hizi yupo wapi, nilijikuta ninampenda yule dada kuanzia naman anavyowasilisha mada, anavyochangia katika majukwaa mbalimbali na hata vile anavyojielewa, she was the best yani nilikua mpaka natamani nimpate nimuoe kabisa
Mwaka 2014, nikaamua kujiunga Jamii forum ili nijiweke karibu na huyo dada, nilitumia mbinu zote kumpata ila nikagonga mwamba kwanza hata PM alikua hajibu , sikumoja nikajitosa kumfungulia uzi, wakati uzi unatrend huyo dada akapotea hapa jukwaani moja kwa moja sijui aliamua kuikimbia JF au ana ID mpya, nilitamani niondoke JF moja kwa moja lakini najipa moyo kwamba atarudi