Ni kitu gani kilikupelekea mpaka ukajiunga na mtandao wa jamiiforum

Ni kitu gani kilikupelekea mpaka ukajiunga na mtandao wa jamiiforum

zamani jamii forum ilikua ina watu wenye kufikiri kwa mapana pia watu waliheshimiana kutukana matusi au kumjibu vibaya member mwenzio ilikua mwiko unapigwa ban haraka sana jf kulikua hakuna mada za upuuzi kama za fb kulikua hakuja vamiwa na watoto wasio jielewa walichoka maisha nakuja kumalizia hasira zao humu lakini sikuhizi mods wamelala mtu anamtukania wazazi member mwenzie anadunda tuu mtu anamtishia mtu anapeta tuu miko ya jf sasa hivi imekiukwa umekua mtandao wa bora liende zamani mtu unakua na hamu kabisa umalize mishe uzame jf kupata nondo za watu wanao jitambua lakini kwa sasa makasiriko vichambo kukoseana adabu kuvunjiana heshima ndio maisha ya jf mada za kupuuzwa zimejaa humu majukwaa mpaka ya great thinker yamevamiwa na watu wa hovyo mno.
Jamii Forum Maadili nawapa pole. Pamoja na makorokocho yote ya humu lakini hutaki kujitoa nyambafu.
 
Kuna msela wangu, alikua anakuja huku jukwaa la wazee wa kubeti akaniambia kuna na kuuliza maswali kama ya kitechnologia ukapata wajuzi wakakupa majibu ya maswalia yako.

Basi mzee na mimi nikaruka nayo jamii forum.
Ila mie majukwaa yangu ni
~Jukwaa la Dini.
~Mahusiano, urafik
~na habar na hoja mchanganyiko utanikuza hizo area
Aiseee hongera mkuu me kuna majukwaa huwa sitembelei kabisa kama kubet, dini nk no
 
Mimi nilijiunga humu nkifuata "katuni mix". Ila cku hizi siipati tena hiyo katuni. Sijui mchoraji alienda wapi.

Lakini hivi karibuni nimejionea vituko sana. Matusi tele. Tena bila kujali wanatukana hadi marais. Baya zaidi hadi wengine walishakwenda mbele za haki. Lakini bado matusi yanawafuata. Nadhan mods wako mrengo fulani. Na sio vizuri.
Hahahhaah mtapata taabu sana
 
Nakumbuka mwaka 2016 kipindi icho nikiwa kidato cha 3 nilipata demu flani hivi na kusema ukweli nilitokea kumpenda sana huyu mwanamke, kiasi kwamba nikawa namchunguza maana nilihisi uwenda akawa anatoka na wadau wengine, hali hii ilinipelekea nikawa nagoogle sana kuhusu dalili za mwanamke anaekupenda, mara nagoogle dalili za mwanamke mwenye wapenzi ya mmoja, sasa katika kugoogle nikawa napata majibu ambayo yanayonipeleka moja kwa moja kwenye jukwaa la mapenzi, hivyo nikawa mlevi wa jukwaa la mapenzi.

Pia mwaka 2018 kipindi nipo A level nikapata tena demu mwingine aisee nae nae nilimpenda sana na nikawa namfatilia sana hivyo nikajikuta nagoogle sana mada za mapenzi ambazo majibu yake nikawa nayapata kwenye jukwaa la mapenzi nahisi kwa watu wanaongoza kufatilia mada za mapenzi ni mimi maana nilikua kama mlevi tena wa mapenzi.

Mwisho kabisa siwezi kusahau jukwaa la mambo ya technology maana nilikua nalifatilia sana mambo ya simu, laptop na games mbali mbali, naweza kusema kwa kifupi mambo ya mapenzi na technology ndio yamenileta humu jf.

Karibuni sana wadau na nyie mueleze sababu zipi ziliwapelekea mpaka mkajiunga na mtandao wa jamiiforum.

NAWASILISHA.
Bila shaka Kwenye jukwaa la Mapenzi ulikuwa mlevi wa Stori za Kasie
Na jukwaa la technology ulikuwa mlevi wa nyuzi za Chief-Mkwawa
 
Ujakosea mkuu huyo chief mkwawa na kasie salute kwao ila chief mkwawa sijui amejifunzia wapi maana huwa najiuliza sipaji jibu
Chief ni moja ya IT Guru sana na ana blogs zake nyingi hapa bongo hivyo mambo ya technology hapo umefika.
Hongera kwake
 
Chief ni moja ya IT Guru sana na ana blogs zake nyingi hapa bongo hivyo mambo ya technology hapo umefika.
Hongera kwake
Aisee nampongeza tena jamaa amenisaidia sana yani huwa nasoma post zake ni hatari tupu.
 
Back
Top Bottom