Ni kitu gani kizuri umewahi kufanyiwa na kimeacha alama katika maisha Yako?

Ni kitu gani kizuri umewahi kufanyiwa na kimeacha alama katika maisha Yako?

Nilishawahi kukuandikia humu mwaka jana, kwangu ni binti alikua anaitwa Mariam, alikua junior kazini na akaacha kazi ya ofisini na kuja kunisaidia kulea mtoto wangu wa kwanza kwa sababu nilikua nina hofu ya kumuacha na dada wa kazi.

Alinionyesha wema wa ajabu, mpaka leo ninamkumbuka sana, bahati mbaya tumepotezana kwa zaidi ya miaka 10, sijui alipo 😔.
Naikumbuka hii My dada,inaonekana alifanya kitu kikubwa sana kwako bila yeye kujua. Fanya umtafute sasa
 
Hakina faida kwa leo wala jana ila kilinitambulisha nikatambulika mimi ni nani pale pepa zangu zilipokua zinatumika km marking scheme (shule ya msingi, secondary mpaka chuo) na kuambiwa nipande ubaoni niwaelekeze wenzangu walioshika mkia baada ya hapo wasioelewa wote wananifuata na kunizunguka niwapige tena msasa mpaka waelewe and lastly wanaweza kuondoka kabisa na pepa langu wakaendelee kujifunza nyumba maana wanakua bado hawajaelewa na mimi kurudi home nikiwa sina karatasi yoyote ya mtihani nilioufanya kwenda kuonyesha nimepata ngapi

Hizo alama hua haifutiki kamwe mengine siwezi kuyaweka hapa
Ulifanya kitu kizuri sana jamani. Utakumbukwa daima
 
Ni mengi sana hayahesabiki, hayaelezeki..

Nawaombea wote Mungu awafanyie makubwa zaidi..
 
Mara nyingi watu hukumbuka mabaya tu waliyopitia au kufanyiwa katika maisha Yao na watu mbalimbali.

Lakini Leo ningependa tujue mambo mazuri ambayo watu wamefanyiwa na yameacha alama katika maisha Yao.

Pengine watu waliozea kuwafanyia watu mabaya watajifunza kitu.
Karibuni watu wangu wa Nguvu.
ila binadamu ni kiumbe mbinafsi sana
yeye muda wote anawaza kutendewa this kutendewa that
kupendwa
kusikilizwa
kuthaminiwa
kujaliwa
kuthaminiwa

hakuna popote anakoweka uwekezaji wa kuwafanyia hayo wengine. very hopeless being
 
ila binadamu ni kiumbe mbinafsi sana
yeye muda wote anawaza kutendewa this kutendewa that
kupendwa
kusikilizwa
kuthaminiwa
kujaliwa
kuthaminiwa

hakuna popote anakoweka uwekezaji wa kuwafanyia hayo wengine. very hopeless being
Wewe hupendi hayo?
 
Vingi sana, watu wema wapo !!!!!!!!!
Hata hapa napofanya kazi ... ni assist tu niliipata !!.
#tuishi wa watu vizuri
 
Back
Top Bottom