Ni kitu gani mzazi/ mlezi alikukosea ukiwa mdogo bila kukuomba msamaha na kinakuumiza mpaka leo, mlioweza kusamehe mlifanyaje?

Ni kitu gani mzazi/ mlezi alikukosea ukiwa mdogo bila kukuomba msamaha na kinakuumiza mpaka leo, mlioweza kusamehe mlifanyaje?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Watu wengi wakiwa watoto wanafanyiwa matukio ya kuumiza na kwasababu ya udogo wao wengi hupuuzwa au kuongezewa maumivu badala ya kushughulikia madhara yaliyoletwa. Kutokana na dhana iliyojengeka kuwa "Mkubwa hakosei" wazazi/ walezi wengi huwa hawaombi msamaha endapo amemkosea mtoto, na watoto kukosa amani (closure) ya kuombwa msamaha kutokana na alichofanyiwa.

Matokeo yake mtoto anakua akijiona yeye ni mkosaji lakini pia kuendelea kuumia akijua fika kitu kile hakikuwa sahihi mbali ya aliyekosea kutokubali kakosea lakini pia kabebeshwa mzigo kuwa yeye ndiyo mwenye kosa!

Wazazi/ walezi wanafanya kosa kubwa kudhani kuwa kwakuwa ni mtoto basi atasahau, wakiwaacha wengi kukua na vinyongo na kuathiri mahusiano yao na waliosababisha maumivu hayo au kwa wengine watakaokuwa chini yao.

Je, ni kitu gani mzazi/ mlezi wako alikukosea bila kukuomba msamaha na huwa kinakuumiza mpaka leo, kwa walioweza kusamehe mlifanyaje?
 
Kunipangia Cha kufanya even kusoma ila nilikuja kufundishwa kumsamehe mzazi bila condition yoyote.

Na kadri uelewa na ufahamu ulivozidi nikaja gundua hawakuwa na Nia mbaya but Ni tafsiri zao juu ya Yale yote waliyoyaona.
#Usiongeze mipaka iliyowekwa na wazee wako.
 
Hakuna mzazi duniani anaomba mambo mabaya kwa mtoto wake ,hata akikuchagulia mke au mme lengo lake huwa ni zuri sana,na kumbuka Akitoka Mungu wa pili ni mzazi hasa mama.Usikumbuke negative kwa mzazi,jitahidi sana ukumbuke negatively kwa mzazi
 
Dah mtoa mada umenigusa sana mimi nasumbuliwa sana na hili jambo kuna mambo ya kawaida tu mzazi unakuta alikosea nipo na miaka 4 lakini mpaka leo na ukubwa huu nayakumbuka yananiumiza sana ..
 
Hakuna mzazi duniani anaomba mambo mabaya kwa mtoto wake ,hata akikuchagulia mke au mme lengo lake huwa ni zuri sana,na kumbuka Akitoka Mungu wa pili ni mzazi hasa mama.Usikumbuke negative kwa mzazi,jitahidi sana ukumbuke negatively kwa mzazi
Vipi ukishindwa kabisa kusahau, unafanya nini kupona maumivu hayo?
 
Dah mtoa mada umenigusa sana mimi nasumbuliwa sana na hili jambo kuna mambo ya kawaida tu mzazi unakuta alikosea nipo na miaka 4 lakini mpaka leo na ukubwa huu nayakumbuka yananiumiza sana ..
Pole sana mkuu
 
Ongea nae,mchane makavu....
Hao mama zenu wa kinyaki ambao hata ukijikwaa ukaanguka au umeungua na moto jikoni badala ya kukupa pole anakulamba mboko "umchane makavu" akuangalie tu??!!
Ilopa likoneka,ndipo apa....
 
Mnareta uzungu kwa maisha ya mtu mweusi.

Yan mzazi /mlezi akuombe ww msama.

Jaman mitandao ya kijamii na Series na documentary tunazoangalia zisitudanganye na kutuchanganya akili zikatufanya tuone na Sisi watu weusi tunaweza kua wazungu
 
Lakini pia tunatakiwa kukumbuka laiti wangetuacha tu tukafanya lile tunalolipenda sisi tungefika hapa tulipo?

Mzazi anatakiwa akuongoze ili usiharibikiwe - spare the rod, spoil the child. Yeye kama binaadamu lazima atakosea lakini lazima aonyeshe authority yake mbele ya watoto na familia yake.
 
Kunilazinisha kuendelea kusoma shule ambayo seconds masters wote wananitongoza na walimu watatu.....Siku ya siku nkaja jua alikua akinifundisha kutokukimbia matatizo bila ya kuyatatua
Uliwakubalia au uliendelea kubana?
 
Uliwakubalia au uliendelea kubana?
Nliendelea kubana lkn nlikua hata nkikaa na mkaka atapigwa bila makosa.....Nlikosa raha siku namaliza shule nlimwambia mama kila kitu ndo akabaki anashangaa.....Ety akaanza kunambia ushahid unao nikamwambia sina akasema kam hauna basi
 
Back
Top Bottom