Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Watu wengi wakiwa watoto wanafanyiwa matukio ya kuumiza na kwasababu ya udogo wao wengi hupuuzwa au kuongezewa maumivu badala ya kushughulikia madhara yaliyoletwa. Kutokana na dhana iliyojengeka kuwa "Mkubwa hakosei" wazazi/ walezi wengi huwa hawaombi msamaha endapo amemkosea mtoto, na watoto kukosa amani (closure) ya kuombwa msamaha kutokana na alichofanyiwa.
Matokeo yake mtoto anakua akijiona yeye ni mkosaji lakini pia kuendelea kuumia akijua fika kitu kile hakikuwa sahihi mbali ya aliyekosea kutokubali kakosea lakini pia kabebeshwa mzigo kuwa yeye ndiyo mwenye kosa!
Wazazi/ walezi wanafanya kosa kubwa kudhani kuwa kwakuwa ni mtoto basi atasahau, wakiwaacha wengi kukua na vinyongo na kuathiri mahusiano yao na waliosababisha maumivu hayo au kwa wengine watakaokuwa chini yao.
Je, ni kitu gani mzazi/ mlezi wako alikukosea bila kukuomba msamaha na huwa kinakuumiza mpaka leo, kwa walioweza kusamehe mlifanyaje?