Asee Mie nakumbuka mwaka 2003 nilienda Kariakoo kununua nguo.
Nimezunguka kama dakika 15 sijapata nguo ninayoipenda(niliyoifuata),nkajisemea moyoni moyoni yani mie mjanja mzima wa town leo nakosa nguo kariakoo! SIKUBALI!
Nikizama tena,ile paap kutupa jicho nikaona kuna sehemu meza watu wamejaa kinoma,,nikasogoea,kucheki tu kuna nguo nyingi yani kama zote...Moyo ukasema ndio hapahapa leo patanikoma!!
Mwanaume nikaanza kusagula..sagula,,sagulaaaaa kama dakika 30 mpaka nimebaki peke yangu sijapata kitu,,Kumbe!! bana jamaa mwenye meza yake ananichora tu huku ananitupia nguo cheki na hiyo Dogo,,mara cheki hiyo dogo hadi jamaa kachoka...
Baadae nkamua niache tu kusagula nisepe!,,weee jamaa mwenye meza ya nguo wacha acharuke weee dogo acha UNGESE yani umenishuhurisha lisaa lizima afu now unasema unataka kusepa!..CHEKI NGUO HAPO UNUNUE..Mara wamenijalia nunua nunua nunuaaa kelele kibao...mwanaume nikaone isiwe tabu nikainama tena na kuibuka na nguo kama 7 kwa hasira afu kuwaonesha hela nilikuwa nayo nikaongeza zingine 3..Nikalipa huyoo nikasepa...ASEE KUFIKA HOME ZILE NGUO 6 NI BLAUZI,2 taiti si taiti yani kama za kihindi hivi...na mbili zingine zinamatobo ya panya hata ukienda kwa fundi hakubali kushona...!!!
ASEE MPAKA LEO NIMEAPA SITO KUJA KUSAGULA HATA SIKU MOJA....mwnedo ni Classic Wear tu