Ni kitu gani ulikijaribu kwa lengo la kutesti mara moja ila kimekuingiza kwenye shimo la uraibu/addiction unatamani kutoka lakini unashindwa?

Ni kitu gani ulikijaribu kwa lengo la kutesti mara moja ila kimekuingiza kwenye shimo la uraibu/addiction unatamani kutoka lakini unashindwa?

Ninakumbuka siku moja nilikuwa nipo nipo tu wala sina kampani, ghafla wazo likanijia nikanunue fegi nijaribu mara moja tu nione ikoje.

Kuanzia hapo mdogo mdogo nikaanza kupiga paf kila jioni na huwezi amini hakuna mtu wa karibu anaejua ninavuta wala kunishuhudia naivuta, huwa naenda kuvutia sehemu za mbali watu hawanijui.

Nimejaribu mara kadhaa kuacha ikiwemo kupause kwa mwaka mzima ila ghafla nikarudi.

Nachojutia zaidi ni kwamba sigara hainilevi tena kama mwanzo, ninaivuta tu kwa mazoea lakini kuacha inakuwa ngumu.

NB: Kiwe ni kitu ambacho unatamani kukiacha, kama una enjoy hakihusiki
Kunywa pombe aisee natamani kuacha sana ila naweza kaa ata week 2 bila kunywa ila nikibaki mwenyewe ghetto siku mzima nikiboreka tu mawazo yananiijia kwenda kunywa najikuta nimekunywa
 
kwa hiyo nikishatoka hapo nakuwa nimeweza kuacha?
Utaelezwa madhara na utafanyiwa counselling.
Tatizo Watanzania tunaona hospital kama sehemu ya matibabu ya kimwili tu,no hata kisaikolojia pia. Pale ni sehemu hata mishe zako haziendi vizuri unaweza kwenda kupata ushauri(cha msingi umpate mtu sahihi wa hiyo shida)
 
Back
Top Bottom