Ni tabia gani umepanga/ulipanga kuiacha kufanya punde tu ukiuanza mwaka mpya? Vipi matokeo yake

Ni tabia gani umepanga/ulipanga kuiacha kufanya punde tu ukiuanza mwaka mpya? Vipi matokeo yake

Half american

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
46,410
Reaction score
114,823
Habari wakuu, herini wote kwa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Tukiwa kwenye siku ya mwisho ya mwaka 2023 ni jambo jema sana kumshukuru Mungu na kumuomba atuvushe salama wote tuuone na kuuanza mwaka mpya wa 2024.

Kama ilivyo kawaida kwa miaka mingine iliyopita, baadhi yetu huweka maazimio ya kufanya kitu fulani kwa mara ya mwisho na kuahidi kubadilika kabisa mwaka mpya ukishaanza. Wengi ni ishu ya tabia na mazoea ya kufanya jambo fulani kwa mfano kuvuta sigara, kunywa pombe, kujichukulia sheria mkononi na tabia nyinginezo.

Hii ya kufanya kwa mara ya mwisho inawagharimu wengi sana na kushindwa kuacha tabia husika.

Binafsi mwisho wa mwaka jana niliweka azimio la kuachana na unywaji wa soda kabisa ila nimeshindwa kulifanikisha hilo, kwa kiasi fulani nimepunguza ila sijaweza kuacha jumla. Nipeni mbinu wakuu.

Ni tabia gani unapambana kuiacha kila mwaka na imeshindikana? Tupeane mbinu za kuacha/kuondokana kwa waliofanikiwa kuachana na mazoea/tabia hizo.

Wale wa kushindana na pombe na wanawake slow down ni hatari kwa afya.

Tuumalize mwaka 2023 salama wakuu.

NB: Pambana na yale mambo yaliyokukwamisha mwaka uliopita ufanye mwaka mpya kuwa wa kipekee kwako na wanaokuzunguka.
 
Wakuu

Kila mwaka kuna rafiki yangu huahidi akivuka mwaka mpya ataacha pombe, lakini haifiki hata mwezi mmoja tayari anarudi tena. Yaani ameshindwa kabisa kuacha.

Familia, kwenu je—ni kitu gani unaahidi kuacha kila mwaka, lakini bado hukiachi? 👇🔥
 
Hatari sana ,ugomvi na majirani usioisha hiki kitu kinanitafuna sana .

Japo ugomvi nauanzisha mimi japo wakinizidi nguvu naomba msamaha yanaisha ila lazima wiki au mwezi unaofuata lazima nilianzishe tena kama kulipiza
 
Back
Top Bottom