Ni kitu gani watu wengine huona kuwa cha kawaida ila wewe huwezi kufanya au kuwa nacho?

Kujirekodi rekodi unaimba imba vinyimbo huku unafinya finya na kulamba midomo kisha kupost sijawahi na siwezi na huwa nashangaa wanaoweza wanawezaje
Too funny 😂!

Umeelezea vizuri kweli na umewasema wengi sana na wengineo wapo humu humu JF na wamekuruka hawajakugongea Like.

Pia, huwa wanageuza geuza/ wanatikisa vichwa vyao na kurembua vimacho.

Na ukifanya uchunguzi zaidi, utabaini kuwa wengine hawaimbi maneno yaliyopo kwenye wimbo, bali huwa wanachezesha tu vimidomo vyao [lip-synch]. Na ukichunguza zaidi, utagundua vimidomo vyao haviendani na maneno ya wimbo [off-key kind of].
 
We Ana…..wanaume gani hao ambao huwa wanajing’ata midomo na kuimba imba? Mi naonaga wadada tu….
 
Inakua kama mtu ambae anaimba wimbo ambao haujui🤣🤣🤣 kinachotia aibu zaidi ni ukute mtu mzima anafanya hayo😹
 
Kuna dada mmoja anarap mulemule
Na anatoa sauti
Yaani anaweka sauti yake , na ya wimbo kwa pamoja.
 
We Ana…..wanaume gani hao ambao huwa wanajing’ata midomo na kuimba imba? Mi naonaga wadada tu….
Wapo😂😂😂😂
Sasa hao ndio huwa wananiacha hoi.
Kaka mzima anajiuma midomo yaani ni hatari.

Kwa wadada ni kawaida.
 
Huwa nashangaa watu wengine wanaweza vipi kutembea barabarani/njiani wakiwa wanapiga mziki kwenye simu zao tena Kwa sauti kubwa mi siwezi

Mtu yupo ndani ya gari la abiria anapiga mziki kwenye simu yake tena Kwa sauti kubwa au akipigiwa simu anaweka loudspeaker anaongea jamani[emoji849].
 
Kumiliki au kuvaa nguo ndefu, hii kwa kweli siiwezi na imenishinda. [emoji119][emoji119]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…