Ni kitu gani watu wengine huona kuwa cha kawaida ila wewe huwezi kufanya au kuwa nacho?

Mimi kitu ambacho siwezi kufanya ni ile kutamani au kuona wivu kwa ajili ya Mtu fulani. Siwezi kufanya kabisa maana haya maisha yana mambo mengi sana
 
Nilipo highlight red hapo yaani hii ni tabia ya Mabinti wengine anaji snap au anatengeneza video TikTok huku anaimba nyimbo za Mbosso au za kuitamani ndoa huwa nawashangaaga sana. Alafu hiyo anayefanya hivyo ni graduate kabisa
😂😂😂😂jamani
 
Nagonga vizuri km niko na shoga angu au niko na mtu. Alone siwezi 😂
niliona jamaa moja anatafuna ice cream ya ukwaju kwa daladala, dah ni kama vile anafuna chupa, halafu meno yakiganzi anapose kidogo.. mpaka yapate moto kwanza anang'ata tena 🐒

mie mbavu sina nashindwa kujizuia kucheka🤣
namcheki jamaa anapambana iishe haraka ni kama kajishtukia watu wote walikua wanamcheki ..
 
Uoga wako ndio umaskini wako. Jamaa asingewazingatia kabisaa amalize askrimu yake
 
Kuangalia Movie zilizotafsiriwa, au zile zinazooneshwa DSTV.
Kwenda bar mida ya usiku afu mtu anakunywa juice huwa nashangaa.
Kupaka ile super black
Pia nawashangaa wale unamkuta kavaa kipensi kifupi halafu kimebana afu unakuta mnene na kitambi duuuh
Wanaovaa Air max
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…