Ni kitu gani watu wengine huona kuwa cha kawaida ila wewe huwezi kufanya au kuwa nacho?

Ni kitu gani watu wengine huona kuwa cha kawaida ila wewe huwezi kufanya au kuwa nacho?

Kupost vijembe whatsapp....mtu akipost vijembe aibu huwa naona mimi, kugombana kidogo wasapu mie siwezi!!!

Kujirekodi rekodi unaimba imba vinyimbo huku unafinya finya na kulamba midomo kisha kupost sijawahi na siwezi na huwa nashangaa wanaoweza wanawezaje
 
Kuna vitu ambavyo watu wengine wanaona kama trend au kawaida ila Mimi siwezi kufanya au kumiliki.Mfano kuweka na mito mingi kwenye kitanda,kuwa na Snapchat kwenye simu au account ya TikTok n.k! Wadau ni kitu au jambo gani hilo huwezi kufanya au kumiliki?
Kumtukana mwanamke.

Pia siwezi kuvumilia tusi linalotoka kinywani mwa mwanamke. Nitaondoka hilo eneo .

Kwa wanaume wenzangu haina shida.
 
Dah, kweli tuko tofauti.. me pensi nashindwa kuvaa church tu!
Mimi naivaa mbele ya mke wangu tu,

Zile ndefu zinazokaribia kwenye Ankle ndio navaa hadi public.

Sasa utakuta mtu amevaa kipensi kimeishia magotini na yupo comfortable kabisa, akikaa kipensi kinavutika hadi mapajani. Hiyo nilivaa enzi nipo primary tu.
 
Back
Top Bottom