Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Swali: je ni kitu gani kinachoweza kukufanya uachane na mke/mme/mpenzi wako?!Ni kitu gani unafikiri akifanya au kikitokea kwenye mahusiano yenu baada ya muda hutoweza kuendelea kuvumilia?!
Binafsi vitu ambavyo vinaweza kuniondolea yale mapenzi nlokua nayo mwanzo ni ....
1. Kunipiga - mwanaume kuniinulia mkono mwanamke mzima ambae kama kuna tatizo angeweza kunijulisha kwa njia nyingine na likatatulika kwa kweli siwezi kuvumilia.Maana ukichekelea leo jiandae na kesho!!
2.Kutoka nje ya mahusiano. - sijui kama itatokea siku nikabadilisha mawazo kuhusu hili ...kwa sasa hivi naamini kama mtu ananipenda na kuniheshimu kweli hawezi kutoka nje ya mahusiano tuliyonayo.Kama kuna kinachokosekana aniambie nirekebishe.
3.Kunidharau/tukana mbele za watu - inaonyesha haniheshimu...na kama haniheshimu siwezi kuona tukiendelea hata kufika mbali zaidi ya kua wapenzi tu maana kuheshimiana ni muhimu.
4. Kuonyesha kutokujali hisia/mawazo yangu - mtu ambae anamwachia mwenzake kazi nzima ya kujenga mahusiano ni sawa na mzigo mzito ambao unabebeka ila baada ya muda unachosha.Kuna watu ambao wao hata kumjulia mwenzake hali hawezi...kusongesha mahusiano mbele hawezi..yani we unakua na kazi ya kumpeleka upande huu na ule bila kujua kama kweli ndo kilichopo moyoni mwake.Kama unamlazimisha vile au anafanya tu kukuridhisha uendelee kuwepo kwa muda ule ambao anaweza kutumia uwepo wako.Ubaya wa watu kama hawa ni kwamba hata siku akiamka akakwambia sikuwahi kukupenda huwezi kumbishia kwasababu hakuwahi kukwambia wala kuonyesha kwa matendo!!
5.Ubinafsi - mtu wa mimi..mimi ..mimi.Kila kitu ni vile anavyotaka yeye au hamna kitu.Wakati mahusiano yanatakiwa yawe makubaliano na michango ya pande zote mbili.
6.Ulalamikaji/kutokua na shukrani - hata ufanye zuri gani huwezi pata asante na mbaya zaidi utaambulia malalamiko.
7.Kutokujiamini kulikopitiliza - maana mara nyingi hii hua inazaa tuhuma.Anakua hana imani kwamba unampenda kweli au ukienda sokoni unaenda kununua nyanya tu na kurudi.Tuhuma zikizidi zinaua hisia zilizokuwepo.
N.k....
Wewe je....?!
haya yote ukiyajumlisha ni kuwa hakuna upendo moyoni mwake..........kwa hiyo hakuna malalamiko ila kukubaliaa na hali iliyopo au kufungasha virago vyako..................because you are worthy more than he is willing to give to you..............................kwa hiyo nionapo hakuna reciprocating love or there is unrequited love..............I know I should be angry to no no one but accepting the situation as it comes..................