Ni kivipi Serikali itajiwajibisha Kwa upotevu wa mabilioni ya fedha kuhamia Dodoma kumbe ni geresha?

Ni kivipi Serikali itajiwajibisha Kwa upotevu wa mabilioni ya fedha kuhamia Dodoma kumbe ni geresha?

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Upole wtu ni mzuri na unapaswa uendelezwe Kwa kila mtu, lakini endapo tunataka tuondokane na kichefuchefu cha umasikini uliotopea, some time ni kuvunja upole wetu hasa linapokuja swala la masilahi ya nchi yetu Kwa ujumla, Ni Kwa namna gani serikali tunaweza kuiwajibisha inapotumia fedha zetu bila mpango mzuri?

Takribani miaka mitano iliyopita, kumewepo na bajeti kubwa ya kuhamisha makao makuu, kutoka Ikulu ya magogoni Hadi kujengwa Ikulu mpya katika mji mkuu wa Kiserikali jijini Dodoma

Mabilioni ya fedha yametumika kuhamisha ofsi za kiserikali karibu wizara zote zimejenga ofisi zake huko Dodoma na kuhamia kabisa.

Kinachonishangaza, ni kuwaona Baadhi ya viongozi tena wakirudi Dar kiwiziwizi yaani kama wanakuja tena kuweka makazi jijini Dar

Je hawa viongozi hawana uchungu na mabilioni ya fedha waliowekeza huko? Kama wananchi walipa Kodi, wakumbuke kwamba hizo fedha zinatuuma kupotelea Kwenye majengo yasiyo kaliwa na watu

Ni kivipi Serikali inaweza kujiwajibisha Kwa upotevu wa mabilioni ya fedha kutumika kujenga maofsi makao makuu ya nchi halafu kuyatekeleza?

Na kama serikali haikuwa na mpango wa kuhamia Dodoma, Kwa nini fedha hizi zisingetumika kutoa ajira mpya Kwa vijana?
 
Kwa hiyo unamaanisha PM anapowawajibisha watumishi wa wizara ya fedha kujilipa miposho, pia atwambie Kwa nini serikali ilitumia nguvu nyingi na fedha nyingi kujenga wasikotaka kuhamia siyo??
 
Kwani nani tena amerudi huko Mjini Darulisalamu Wajameni? Serikali si IPO Idodomya au nani yupo huko?
 
Serikali hii hii ya "Sisi -M" ??

Mara yako ya mwisho lini kusikia kiongozi mkubwa kuwajibishwa na kuburuzwa kortini ni lini??
 
Serikali hii hii ya "Sisi -M" ??

Mara yako mwisho lini kusikia kiongozi mkubwa kuwajibishwa na kuburuzwa kortini ni lini??
Dagaa ndio wamejaa jela mtumishi kapiga ya brush anakaa nje ya Kazi au ndani na sio viongozi.
 
Kuhamia dodoma ilikuwa ni mbinu ya kutakasishia tu kodi zetu.Na sio tija kiuchumi.
 
Yaani hapo akiwa Dar analipwa posho za kuwa nje ya ofisi ya Dodoma. Akiwa Dodoma analipwa posho ya kuwa nje ya ofisi yake ya Dar
Kwa sababu hakujajulikana ni wapi zilipo ofisi zake rasimi??
 
Ccm ni chama cha kishetani na hii ni serikali ya kihuni
 
Kwa hiyo unamaanisha PM anapowawajibisha watumishi wa wizara ya fedha kujilipa miposho, pia atwambie Kwa nini serikali ilitumia nguvu nyingi na fedha nyingi kujenga wasikotaka kuhamia siyo??
Yap
 
Ccm ni chama cha kishetani na hii ni serikali ya kihuni
Kwenye hili, kama kweli hawana Nia ya kuhamia tena Dodoma, ni ufisadi wa fedha zetu, huku ni kulitia umasikini Taifa letu
 
Mpango mzima wa kuhamia Dodoma ni wizi.
Kujenga majengo ya serikali huko Dodoma ni wizi.
Kurudi Dar ni wizi
Kuendelea kujenga majengo huko Dodoma ni wizi.

Kila kitu wizi.
 
Mi mwenyewe Dodoma sikai watu wanategemea kuuza ukili,vikapu ,ubuyu na karanga zilizopukuchuliwa maganda ndio upeleke Ikulu?!.Bure kabisa.
 

Mpango mzima wa kuhamia Dodoma ni wizi.
Kujenga majengo ya serikali huko Dodoma ni wizi.
Kurudi Dar ni wizi
Kuendelea kujenga majengo huko Dodoma ni wizi.

Kila kitu wizi.
Du!!
 
Back
Top Bottom