Ni kosa gani ulifanya wakati unanunua kiwanja cha makazi au biashara?

Ni kosa gani ulifanya wakati unanunua kiwanja cha makazi au biashara?

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Habari zenu wakuu? Lengo ni kuelishana, kosa ulilolifanya wewe kupitia comment yako huenda likamsaidia mwingine!

Mimi kosa kubwa nililolifanya ni kununua eneo sloped, limenipasua kichwa lile eneo, eneo lina viwanja takribani 300, sasa mimi nilienda kununua wa mwisho nikakuta maeneo mazuri yameshawahiwa.

Kibaya zaidi bei yake ilipoa poa kidogo, nikasema siyo mbaya ngoja nijilipue nyie 😀

Kwa sisi ambao tunapesa za kuunga unga ukinunua eneo kama hilo jiandae.
 
Jamaa yangu aliuziwa kumbe ni road reserve
Kosa kubwa kuliko yote ni kununua ardhi yenye mgogoro aidha wa kifamilia mambo ya urithi ama mipaka
Ndio maana wanashauri kabla ya kununua eneo nenda kajiridhishe kwanza kwa mamlaka husika
 
Kununua viwanja ni umasikini tu. Nikiwa rais nabomoa Nchi nzima. Huwa naangalia vita kule GAZA wapalestina hawana kitu wana jenga miji mizuuri, sisi tunaambiwa tuna amani na kila kitu, lakini makazi yetu hovyo kabisa.
 
Kuna jamaa kanunua kiwanja bei nzuri sana sana heka 1 halafu ni karibu na center ya eneo husika,
Ilikuwa ni kiangazi pako tambarare saafi pana ukoka wa kijani...jamaa akatamba ataweka bonge la garden kwa mbele na nyuma bustani ya mboga......ikawa usiku,,,,ikawa mchana...mvua ikanyesha......😊...KUMCHEKA NI DHAMBI.
 
🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom