Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Mimi nilikuwa mzee wa kutuma Ela, fundi aliniharibia kwenye Renta, aliunga Renta kienyeji, semu zingine akafunga zingine akaskip...sehemu za nje Renta ikawa juu na sehemu za ndani za milango zikawa chini..sehemu zingine pia hakuweka nondo..niligundua wakati nafanya marekebisho kibaraza Cha nje, kwAni tulivunja beam hatukuta nondo ata Moja.
 
Hiyo mkuu imenitokea mimi, nilinunua kiwanja 2010...nikaja kujenga 2015.. siku magufuli anaapishwa ndo nahamia kwangu,, ila sahiv nimezungukwa na waswahili wasiojielewa hata pakupitisha kigari hapapo...nikija kununua gar itabid ilale (CCM.) Natamani kuuza kwa bei ya kutupa nijenge sehemu nyingine..Kijumba chenyewe cha kawaida ila unaishi na watu wenye wivu balaa....

Makosa niliyoyafanya nilijenga kwa haraka haraka lengo nihamie kwangu kutokana kugombana gombana na mwenyenyumba..
Haraka haraka haina baraka..!!
 
Hii kuna rafiki yangu amejenga nyumba ya kisasa ila imekosa choo ndani..inamuuma saana...kwasababu alikua amejenga kidogo kidogo yani kwa kudunduliza...sasa kama unavyojua maisha yanabadilika...anajilaumu vibaya. Vyumba 5 ndani ila choo cha nje.
Vyumba vitano vyote vya nini, aue chumba kimoja afanye kutengeneza vyoo vya ndani. Tena achague chumba kilichopo karibu na chumba chake ili atengeneze choo cha master na choo cha public.
 
Kuajiri plumber uchwara. Kuta maji yanavuja rangi imebanduka sana
umenikumbusha kitu hapa
nilipanga pahala, maji ni dawasco na kila mtu mita yake
nilikua nalipa 40k kila mwezi, baada ya miezi 5 nakuja kustuka kuna leakage, tena sehem ya outlet ya bomba bafuni, na ni ngumu kugundua, maji yana 'chururu' kimya kimya mno yakiambaa ukutani mpaka chini , inaambaa na kona za sakafu, yalee mpaka kwenye kashimo, yaani chururu huioni mpaka uweke macho karib kabisa na ukuta(una tiles), nikapata jibu kwanini ukuta wote wa upande wa pili(kuna room) ulikua unapukutika

nikafunga koki kubwa ya nje, ikawa nikitaka kuchota najaza jaba na ndoo then nafunga koki, bili ya maji ilikuja 8000 kwa miezi iliyobaki
 
Hata kama una uwezo mdogo na eneo linaruhusu, jenga slope yako na ubakishe paking ya gari hata km wakat huo unamilik guta, amin maisha yanabadilika ikiw we ni mpambanaji wa haki, hari na mari miaka 20 haiwez pita kapa, ukakosa hata kirikuu!

Kingne ni kutenga kaeneo kadogo ka bustan binafsi huwa sifurahi kuishi ktk nyumba ambayo haina hata mti wa kivuri
 
Hii kuna rafiki yangu amejenga nyumba ya kisasa ila imekosa choo ndani..inamuuma saana...kwasababu alikua amejenga kidogo kidogo yani kwa kudunduliza...sasa kama unavyojua maisha yanabadilika...anajilaumu vibaya. Vyumba 5 ndani ila choo cha nje.
Si kimoja akibadilshe kuwa choo mbona rahisi sanaaa... Shimo la maji taka linakua njee maana huwezi jenga choo cha shimp ndani...!! Sioni kama kuna kitu kakosea hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…