Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

😀😀😀 Ukawa kama Dk Bilali aliyekuwa anatembea na kimkasi. Akifika sehemu akakuta kuna kitu cha kuzindua, anazindua hapo hapo...
 
Hujaeleweka
Okay,

Ipo hivi nilitafuta fundi nikampa kazi ya kupiga renta hadi kuezeka, mtindo wa uezekaji kulingana na ramani ni bati la kuficha kwa ndani.

Sasa basi kilichofanyika baada ya kuinua course nne slope ikaonekana ndogo. Basi tukasahuriana ukuta uinuke tena course moja ili baada ya hapo tofali za kulaza zifuate.
Mwenzangu kiherehere akaleta fundi wa kupaua akaendelea kupiga Kench kuzisupport kwa mbao ili baadae tofali ndio zifuate.

Baada ya hapo akalaza bati, nilipo fika site nakuta mafundi wamepanda juu ya zile bati wanapandisha tofali kule juu

Tatizo ni kwamba wanapo panda juu wanapunguza ubora wa bati maana ukiweka uzito misumari hulegea na bati kupinda

Kilichotakiwa kufanyika
1.kazi ya ukuta issue kabl ya kuanza kupiga kenchi
2.plaster na skimming ifanyike kama ikiwezekana mpaka rangi

Hii itasaidia unapo weka bati pasiwe na kitu chochote kinacho panda juu ya bati maana inaweza pelekea kupungua kwa uimara wake.
 

Attachments

  • 20221014_134505.jpg
    1.3 MB · Views: 111
[emoji23][emoji23][emoji23]mkuu njoo nikufanyie water proof treatment huko kwenye ungio la bat na tofar hutojuta tena call/WhatsApp 0757735884 au tembelea Instagram yetu highland_decor_solution
Kujenga nyumba bati kufichilia ndani(hidden roof) kwakweli maisha yamekuwa ya wasiwasi kipindi hiki cha mvua nakaa ndani utafikiri nimejificha chini ya mwembe.
 
Nilishauriwa Kujenga mashimo mawili ya choo,la square na duara ,sasa hivi wengi wananiambia naweza kutumia moja la duara,nawaza hili lingine la square kulifanya kisima cha kuvunia maji ya mvua .

sasa umbali wa shimo la maji taka na shimo la maji safi ni sqm moja ,japo hili la maji safi limesakafiwa ndani,wakuu huu ukaribu hautasumbua?
 
hapo utakunywa sana mikojo mkuu na matumbo mtaugua sana.
 
Daaah!!! Hii ilitokea kwa mzee wangu baada ya kustaafu akanunua jengo kubwa(pagale) hivyo kulimalizia limemkomba hela nyingi na bado hakijakamilika.

Aisee majumba makubwa yenye mavyumba makubwa kwa ajiri ya makazi tu ni msala bora hata liwe la biashara.
 
Bosi hii so hasara. Kuna maeneo mengine yapo ya kishua kabisaa na hununui njia, tayari ipo na haina utata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…