Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

ahahaaa yaani acha kabisa mafundi walinifanya nikanunua tape measure ya kwangu kabisa nakuwa nayo kiunoni maana kwa kufuatilia vipimo,kila nikifika lazima niwaombe tape measure yao, sasa wakati mwingine wakiniona tu wanaficha yao,ikabidi niingie dukani nikifika site na vuta tu kuhakiki vipimo bac wanabaki kutizamana tu
😀😀😀 Ukawa kama Dk Bilali aliyekuwa anatembea na kimkasi. Akifika sehemu akakuta kuna kitu cha kuzindua, anazindua hapo hapo...
 
Hujaeleweka
Okay,

Ipo hivi nilitafuta fundi nikampa kazi ya kupiga renta hadi kuezeka, mtindo wa uezekaji kulingana na ramani ni bati la kuficha kwa ndani.

Sasa basi kilichofanyika baada ya kuinua course nne slope ikaonekana ndogo. Basi tukasahuriana ukuta uinuke tena course moja ili baada ya hapo tofali za kulaza zifuate.
Mwenzangu kiherehere akaleta fundi wa kupaua akaendelea kupiga Kench kuzisupport kwa mbao ili baadae tofali ndio zifuate.

Baada ya hapo akalaza bati, nilipo fika site nakuta mafundi wamepanda juu ya zile bati wanapandisha tofali kule juu

Tatizo ni kwamba wanapo panda juu wanapunguza ubora wa bati maana ukiweka uzito misumari hulegea na bati kupinda

Kilichotakiwa kufanyika
1.kazi ya ukuta issue kabl ya kuanza kupiga kenchi
2.plaster na skimming ifanyike kama ikiwezekana mpaka rangi

Hii itasaidia unapo weka bati pasiwe na kitu chochote kinacho panda juu ya bati maana inaweza pelekea kupungua kwa uimara wake.
 

Attachments

  • 20221014_134505.jpg
    20221014_134505.jpg
    1.3 MB · Views: 111
[emoji23][emoji23][emoji23]mkuu njoo nikufanyie water proof treatment huko kwenye ungio la bat na tofar hutojuta tena call/WhatsApp 0757735884 au tembelea Instagram yetu highland_decor_solution
Kujenga nyumba bati kufichilia ndani(hidden roof) kwakweli maisha yamekuwa ya wasiwasi kipindi hiki cha mvua nakaa ndani utafikiri nimejificha chini ya mwembe.
 
Nilishauriwa Kujenga mashimo mawili ya choo,la square na duara ,sasa hivi wengi wananiambia naweza kutumia moja la duara,nawaza hili lingine la square kulifanya kisima cha kuvunia maji ya mvua .

sasa umbali wa shimo la maji taka na shimo la maji safi ni sqm moja ,japo hili la maji safi limesakafiwa ndani,wakuu huu ukaribu hautasumbua?
 
Nilishauriwa Kujenga mashimo mawili ya choo,la square na duara ,sasa hivi wengi wananiambia naweza kutumia moja la duara,nawaza hili lingine la square kulifanya kisima cha kuvunia maji ya mvua .

sasa umbali wa shimo la maji taka na shimo la maji safi ni sqm moja ,japo hili la maji safi limesakafiwa ndani,wakuu huu ukaribu hautasumbua?
hapo utakunywa sana mikojo mkuu na matumbo mtaugua sana.
 
Kuanza kujenga kwa pesa za pension baada ya kustaafu.
Mzee wangu baada ya kustaafu alifanya hicho kitu. Ni hatari kupita maelezo. Kwanini?

1. Mhusika hashauriki, anataka tu kujenga kwa sababu ana pesa mfukoni.

2. Anachokijenga huwa hakieleweki au hakikamiliki. Anaamini pesa yake ya pension inatosha kufanya chochote au kila kitu kitawezekana. Anaokota ramani popote anataka kujenga.
Daaah!!! Hii ilitokea kwa mzee wangu baada ya kustaafu akanunua jengo kubwa(pagale) hivyo kulimalizia limemkomba hela nyingi na bado hakijakamilika.

Aisee majumba makubwa yenye mavyumba makubwa kwa ajiri ya makazi tu ni msala bora hata liwe la biashara.
 
Nilichofanya sasa hivi nimenunua kiwanja hadi na njia ya kunipeleka main road...

haikua njia nimenunua in terms ya viwanja vya 5 kwa 10, nikaenda mbele tena nkakuta 5 kwa 15 nikaenda hvyo hvyo hadi cha kule mbele kilikua na 10 kwa 12 ... vyote hvyo si vya kujenga kitu ila n njia yangu ya kupita na kutoka na gari, Hajengi KIMA yoyote wala otesha mti nyau yoyote yule.

na hamna anaejua nmevnunua viwe njia wote wanajua n viwanja ntakuja jenga mabanda ya kuku.
Bosi hii so hasara. Kuna maeneo mengine yapo ya kishua kabisaa na hununui njia, tayari ipo na haina utata
 
Back
Top Bottom