Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?


Sema ukizeeka halafu hauna mazoezi!,kushindwa kupanda one floor labda uzee wa miaka 90+,lakini kama ulikuwa mtu wa mazoezi unapanda fresh tu,ndio maana kijijini unakuta mzee miaka 85+ analima na kufanya shughuli zake bila matatizo yeyote,ila mjini mzee miaka 65 yupo taabani
 
Upo sahihi mkuu mazoezi ni muhimu

Sema wazee wameamua kuhamia chini sio kama hawawezi kabisa kupanda hapana ila wameamua hivyo kwakua wanaona usumbufu wa kupanda na kushuka ngazi kila siku plus risk za kudondoka na kuanguka

si unajua tena uzee injury ndogo tu inaweza ikakuletea madhara makubwa tofauti na atakayopata kijana ambaye bado ana nguvu
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kama una shimo lubwa kwenye msingi, unaweza kulitumia kama septic tank au kiaima cha maji, lakini hii lazima plan ianze wakati unaaanza kujenga.

Unaweza kuweka shimo la choo kwenye msingi na bado ukawa na hivi vyoo vya kawaida vya kuflash.

Watu qenye viwanja vidogo pia huwa wanaweka mashimo yao kwenye msingi wa nyumba

Kuna nyumba zingine huwa wanaweza visima
 
Go for surveyes plots hutojuta
 
Khatarious
 
Najuta kuwahi kujenga. Nilijenga nyumba yangu five years ago ilikua ni nyumba kali mtaani hapa sasa wamekuja vijana wamejenga vijumba vyao vya kawaida lkn well designed mpaka nyumba yangu inaonekana ya kishamba sana. Natamani nibomoe nijenge tena nikifikiria gharama naishia kuacha tu 🤨
 
Unajua kwanini? Kila siku style mpya zinaibuka..kwahiyo aliyejenga zamani nyumba yake itaonekana ya kishamba,kama unakumbuka kipindi cha nyuma watu walikua wanajenga na kupaua mgongo wa ng'ombe basi...siku hizi nyumba ina kona kona na bati zinakatika hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…