Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Nina eneo langu hapo mpigi magoe kwa mama mzungu nataka anza kifanyi makeke…

Shukrani kwa uzi huu mzuri na wenye kufundisha mambo kadhaa muhimu
Siku yoyote inayojenga hata tofari moja unatakiwa kuwepo.
Hakuna watu wasio waaminifu kama wajezi.
Na utumie Kipande system.
Anamaliza kazi huku ukiwepo ndio umlipe.
 
Update: nilifika jana kucheki site yangu baada ya kipindi kirefu kupita… mji umekua na unakua kwa kasi…bei ya viwanja imepanda na hofu yako ya maji ya Dawasco basi imeisha, maji yamefika na kila kinachoitajika kipo kwa sasa…
Vizuri changamoto iliyobaki ni barabara
 
Nimejenga kwenye mtaa ambao jirani yangu kaamua kugeuza nyumba yake danguro na kilabu cha pombe kali. Asubuhi unakutana na used condoms kibao. Maisha haya
Uza eneo au mpige figisu mpaka ahame

Tia hata kiberit nyumba ila zingatia watu wakiwa macho ili wasidhurike
 
Katika ununuzi wa vifaa kwa ajili ya ujenzi ,simenti ndio itakuwa ya mwisho au itanunuliwa siku hiyo hiyo.

Nilijikuta namwaga zege mara mbili baada ya kwanza kuharibika. Kumbe nilinunua simenti muda mrefu na sikuitunza vizuri ikaharibika.

Siku tunaenda kutoa mbao tulikutana na mchanga almanusra imwangukie fundi.Nyingine tulikuta imeganda, nyingine iko kawaida lakini kumbe ilisha-expire.

Hii hali ya kununua vifaa kidogo kidogo inahitaji umakini sana katika uhifadhi wake.
 
Cement ina expire?
 
Ndiyo. Muda wake wa kutumika ukiisha bila kutumika ina-expire ndg. Na ukihifadhi vibaya ikapata baridi au unyevu unakuta ndani imeganda inakuwa na mabongebonge haifai tena kwa matumizi.
Ndugu, Cement haina expire date. Kinachotokea ni kwamba unahifadhi sehemu yenye unyevu then ina absorb maji inaganda.
 
Hiyo haiwezi kuwa nyumba. Kwanza ile bomoa jenga bomoa jenga itadhoofisha kuta na kuharibu uimara wa structure ya nyumba yote.
 
Tunachofanya sio kununua na kuvichukua unalipia dukani [deposit] ukiwa tayari kwa ujenzi unaenda tu kuchukua
 
Tunachofanya sio kununua na kuvichukua unalipia dukani [deposit] ukiwa tayari kwa ujenzi unaenda tu kuchukua
Hii ni sawa kwa kipindi hiki zamani kidogo uaminifu na watu wa maduka ulikuwa mdogo sana,unaona bora vitu vyako ujitunzie mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…