Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Kumbe Thinkpads zinakubalika hadi huko dunia ya kwanza?. Huwa nazichukulia kawaida sana.
 
Kumbe Thinkpads zinakubalika hadi huko dunia ya kwanza?. Huwa nazichukulia kawaida sana.
Thinkpad ndiyo laptops zinazotumika zaidi kwenye corporate world Marekani.

Thinkpad kama hii ya X1 Carbon ina specs nzuri sana tu kwa kazi za kawaida, na unaweza ku customize na Lenovo kwa matakwa yako.
 
Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako
Mwisho wa siku ndio utasikia nataka kupangisha
 
nimekosea mengi ila kuna hili la kumuweka kijana kipindi sijaamia bila kuwa na makubaliano yoyote, sasa nimeamia na kijana sijui namuamishaje....
Hii mie pia iliwahi kunitokea siku za nyuma kijana alikaa akapata mke na mtoto. Siku nataka kuhamia kwenye hiyo nyumba ikabidi nikamlipie chumba na sebule mwaka ili atoke kwangu
 
Usije ukatumia pesa yooote kwenye ujenzi ukakaa usubiri muijiza.

Kwa mfano una 2mil unataka uingiize kwenye ujenzi. Tumia 1.5 tu 500k iweke pembeni.

Au una 20 Mil. Weka 15mil kwenye jengo 5mil iweke pembeni. Utanielewa baadae
Ebu fafanua maana nataka kuanza ujenzi hapa nina million 60. So niingize ngapi kwa ujenzi nibakize ngapi na kwa nini?
 
Hii kuna rafiki yangu amejenga nyumba ya kisasa ila imekosa choo ndani..inamuuma saana...kwasababu alikua amejenga kidogo kidogo yani kwa kudunduliza...sasa kama unavyojua maisha yanabadilika...anajilaumu vibaya. Vyumba 5 ndani ila choo cha nje.
Yaani ata fundi alishindwa kumshauri
 
Nyumba inatakiwa kupewa muda wa kukauka. Unaweka msingi unasubiria kidogo ukauke na kunywa maji vizuri wakati unadadisi ni vitu gani ambavyo vinatakiwa kuwekwa hapo kwenye msingi kabla ya kupandisha ukuta.
Mkuu Zemanda shukurani sana kwa madini ya thamani uliyotoa, vipi ni muda wa siku gapi tangu msingi umejengwa ndipo ukuta wa tofali uanze kujengwa?
 
Namshukuru Mungu amenijaalia uwezo wa ku design ndani pangu paweje...

Ninaamini kwamba usipojali kiwanja unachojengea bati umepoteza.

Ukijenga nyumba ukawwka bati. Umefukia kiwanja.

Jenga floor mbili. Utakuwa umesave kiwanja.

Tunajenga nyumba zetu. Lakini tunasahau tunaziba viwanja juu kwenyer paa
 
Nyumba ndefu si inakuwa zuri hasa ukanda huu wa mwambao wa pwani kutokana na misimu ya joto, kwani joto ndani ya nyumba linakuwa si kali tofauti na nyumba fupi au?
 
Asante sana kwa ushauri na mwongozo, Mungu azidi kukuweka.
 
M
Mkuu asante sana ku share elimu, sorry naomba kuuliza je kwani mtu akishakuwa ni fundi ujenzi anaweza asiwe vizuri kwenye ujenzi wa msingi (Fondation)?
 
Urefu wa kwenda juu ni mabati alivyopaua labda, lakini kozi moja iliyoongezeka haiwezi kufanya nyumba iwe ndefu kias Cha kusema "sana"
 
Naombeni ushauri kesho naenda kukutana na fundi ili anipigie gharama za kuanza msingi kwanza

Je kuna ulazima wa kuwa na vyoo viwili vya ndani kimoja master na kimoja cha public, nyumba ya vyumba viwili tu

Au nikiweka choo kimoja tu hicho cha public itakuwa good

Kibaraza cha jikoni hicho kina umuhimu wa kukaa hapo au nikiondoe

Na naomba mnisaidie kwenye upande wa ukubwa sebule inakuwa na ukubwa gani standard urefu na upanda(futi na meter)

Chumba cha master kinakuwa na ukubwa gani pia,chumba cha kawaida kinakuwa na ukubwa gani, choo kinakuwa na ukubwa gani na jiko la kawaida linakuwa na ukubwa gani.

Sitaki nyumba kubwa inisumbue kwenye kuimalizia, nataka iliyotulia standard isinitese kwenye vifaa vinavyoanzia na english huko
 

Attachments

  • IMG_20250214_110953.jpg
    549.1 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…