Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Wakuu Msaada maana septic imepigwa plaster haiachii maji taka. Eneo ni dogo kufanya mbinu ya kuchimba na kuyaachia kwenye mfereji ( kuchimba na kumwaga kojoto, kuyaachia njia style ya kisasa) hapatoshi
 
Usije ukatumia pesa yooote kwenye ujenzi ukakaa usubiri muijiza.

Kwa mfano una 2mil unataka uingiize kwenye ujenzi. Tumia 1.5 tu 500k iweke pembeni.

Au una 20 Mil. Weka 15mil kwenye jengo 5mil iweke pembeni. Utanielewa baadae
Mpauko wake hua si wakitoto, unaishiwa hata shilingi alfu 10 na huna pa kuipata
 
Uko mulemule.

Tena epuka fundi mjauaji..

Yaani badilisha haraka Wala usiogope Chochote
ahahaaa yaani acha kabisa mafundi walinifanya nikanunua tape measure ya kwangu kabisa nakuwa nayo kiunoni maana kwa kufuatilia vipimo,kila nikifika lazima niwaombe tape measure yao, sasa wakati mwingine wakiniona tu wanaficha yao,ikabidi niingie dukani nikifika site na vuta tu kuhakiki vipimo bac wanabaki kutizamana tu
 
Usije ukatumia pesa yooote kwenye ujenzi ukakaa usubiri muijiza.

Kwa mfano una 2mil unataka uingiize kwenye ujenzi. Tumia 1.5 tu 500k iweke pembeni.

Au una 20 Mil. Weka 15mil kwenye jengo 5mil iweke pembeni. Utanielewa baadae
Nilishawahi kujilipua hivi nikabaki na 86k(elfu 86) tu kwenye account na ndio ilikuwa january nikaishia kupiga plaster tu.
Nikapata msiba wa mjomba wangu Moro nikashindwa kwenda nikasingizia naumwa na mafua na kifua kikali ila hali nilikuwa naijua mwenyewe.

Mungu mkubwa, Nilipumzika mwezi mmoja tu alhamdullilah mishe zikakaa sawa nikamalizia.
 
ahahaaa yaani acha kabisa mafundi walinifanya nikanunua tape measure ya kwangu kabisa nakuwa nayo kiunoni maana kwa kufuatilia vipimo,kila nikifika lazima niwaombe tape measure yao, sasa wakati mwingine wakiniona tu wanaficha yao,ikabidi niingie dukani nikifika site na vuta tu kuhakiki vipimo bac wanabaki kutizamana tu
Nilikuwa na tape measure yangu natembea nayo kwenye bag yaani nikawa najua vipimo vya nyumba nzima hunidanganyi.
Mafundi walikuwa wana mind sana hasa wa tiles wanaojenga kwa sqm
 
Ni maeneo yasiyopimwa bila shaka, kama maeneo yamepimwa njia zipo ni sheria, unanunua tu plot, habari ya njia utaiona ktk ramani ya block
Maskini mimi ninunue eneo lililopimwa 20x20 milioni 10 kweli?

wakati mipori imejaa huko kibao haina watu,mnauziana kwa kurusha jiwe litapofika ndio mwisho wa kiwanja chako!

kikubwa maji na umeme viwe vimeshafika,upimaji utanikuta site.
 
Hapa jirani yangu Dodoma Kuna jmaa anafunja nyumba yake kwani alimpa fundi kila kitu ili yeye aje achukue funguo tu nyumba ikisha jamaaa kufika kuchukua fungu akakuta sebule Ni ndogo kuliko choo na jiko Ni kubwa kuliko master

Na nyumba ikisha pauliwa kila kitu na kupigwa plaster
Hasra aliyopata hatokah hasau jamaa amemua kufunja baadh ya kuta na room ili kubalance ukubwa wa sebule iliyo ndogo Kama choo na choo kiko kikbwa kuliko sebule

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Ha ha ha ha sebule kuliko choo 😃
 
hakuna mantiki ya kuweka wiring mbili zaidi ya kuongeza gharama

kinachofanyika ni kuweka 'change over switch' ya kubadili tanesco-solar mle kwenye DB (lile box lenye mifyuzi) na kama solar yako ni Inverterless, hapo utakua unabadili taa, unatoa za AC unaweka za DC ,

kama ni solar ya Inverter hapo hutabadili taa, zaidi fundi ataunga njia zinakazolishwa na solar mle mle kwenye DB kulingana na pendekezo la mteja pindi anapohamisha tanesco to solar
Pia njia sio lazima ufungunge mfumo mzima wa solar, unaweza kufunga back za battery na inverter pekee zinajichaji wakati wa unaumeme wa January, ukikatika ngoma unawashwa
 
Nilishawahi kujilipua hivi nikabaki na 86k(elfu 86) tu kwenye account na ndio ilikuwa january nikaishia kupiga plaster tu.
Nikapata msiba wa mjomba wangu Moro nikashindwa kwenda nikasingizia naumwa na mafua na kifua kikali ila hali nilikuwa naijua mwenyewe.

Mungu mkubwa, Nilipumzika mwezi mmoja tu alhamdullilah mishe zikakaa sawa nikamalizia.
Haimaanishi Ile pesa baki au kota Moja kiluiwekanni Ili uingiize kwenye matatizo ya kifamilia no. Ila ukiona ukiwa na keshi na unaendelea ujenzi unakuwa na confidence..ukiwa Huna kitu hata mafundi watakutukana tu
 
Mimi nilinunua eneo dogo kwa milioni 4 ni 20*20 tukakubaliana na mwenyeeneo niongee 4m zingine aniongezee 20*20, nikaenda kukopa bank kurudi nakuta amepauza, ikabidi ile hela nianze ujenzi nyumba ilichukuwa miaka 4 kufikia hatua ya kuhamia nikiwa namaliza vitu vichache vilivyobaini.

Chumba changu cha master nilikijenga sehemu mbaya hakina upepo, vyumba 2 sio masters na ni vidogo ukipata ugeni ni shughuli.

Parking ni ndogo.
 
hakuna mantiki ya kuweka wiring mbili zaidi ya kuongeza gharama

kinachofanyika ni kuweka 'change over switch' ya kubadili tanesco-solar mle kwenye DB (lile box lenye mifyuzi) na kama solar yako ni Inverterless, hapo utakua unabadili taa, unatoa za AC unaweka za DC ,

kama ni solar ya Inverter hapo hutabadili taa, zaidi fundi ataunga njia zinakazolishwa na solar mle mle kwenye DB kulingana na pendekezo la mteja pindi anapohamisha tanesco to solar
Kweli Teknolojia imekua. Asante kwa Elimu mkuu[emoji120]
 
Back
Top Bottom