Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Nilivyo uziwa sikua nagari.nikajenga nikamaliza nanjia yakuingilia nakutokea ilikuwepo kwasababu wakati waujenzi gari yavifaa ilikuwa inaingia Hadi site.sasa nimehamia nikakaa miezi6 nikanunua gari Alie niuzia tukaanza mgogoro mara apande miti sehemu ninayo pita mara aanzishe biashara yatofari sehemu ninayo pita kiasi chakubakisha kichochoro chawapita kwamiguu.nikampeleka kwamjumbe akaambiwa angoe miti yake akingoa sikuchache ana panda tena.nikaona Bora niuze nikajenga sehem salama yenye majirani wanao jielewa sio yule chawivu anaetamani kilamtu atembee kwamguu
Aiseee

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Kwa sasa,kulingana na mambo ya mgao wa umeme, kuwa na mfumo wa solar ni muhimu sana.
Mfumo wa solar utatumia hiyohiyo wiring kwa mtu mwenye uwezo kwa kuweka inverter na change over switch ili kubadili tanesco/solar, vyote hivyo vitahitaji distribution network mapema ikiwa ni sehemu ya battery,inverter na solar yenyewe.


Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
Hizo "inverter" change over switch zina gharama gani? Huo mfumo una gharimu kiasi gani?
 
Ukiwa na familia mkuu tank hata uwe nazo tatu bado utaziona kama ndoo nne,nina tank mbili moja 2000ltr na lingine 4000ltr na kisima cha kuvunia maji ya mvua ila hayo maji kwa matumizi ya kawaida ya familia kufua nguo za watoto na wote ni wadogo hawajaosha vyombo kufua nguo za wakubwa yasipotumika kwa akili hayakai mwezi.

Naishi Mbezi huko maji Dawasa engineer wanafungua siku wanazotaka wao so yanayopatikana kidogo yasipotumika kwa akili itanitoka siyo chini ya 120K per month budget ya maji tu.
Bora kuchimba kisima?
 
Habari wana JF

Ni kosa gani ulilifanya kipindi unajenga na ungependa wengine wajifunze ili lisitokee kwao?
Nilikuwa wa kwanza kujenga nyumba sehemu ambayo ilikuwa imepanuliwa kuwa sehemu ya jiji la Mwanza sehemu za Mkolani. Nikajenga nyumba yangu kubwa ya kisasa kwa gharama kubwa sana hasa kwa vile ilinilazimu kujivutia maji na umeme mwenyewe. Baada ya miaka 15 eneo likavamaiwa na ujenzi holela wao wakiuita upimaji shirikishi na hivyo jumba langu kuzungukwa na vijumba visivyo na mpangilio kiasi kuwa hata njia ya kwenda nyumbani kwangu haipo tena inabidi nizunguke zunguke kwa kubahatisha hadi kufika nyumbani.

Ushauri wangu ni kwamba epuka kujenga eneo ambalo halijajengwa kwani hujui litakuja kujengwa vipi.
 
Back
Top Bottom