Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Hili nalo, watu tunajenga tukiangalia leo badala ya miaka 20 ijayo, laundry room ni muhimu hata kama huna washing machine leo, miaka ijayo utainunua!!
Ni kweli, wakati ninajenga nilimpeleka rafiki yangu mmoja site kumuonesha (na yeye alikuwa anamalizia ujenzi wa nyumba yake wakati huo) kuna sehemu akaniuliza, " hapa ni kwa ajili ya nini mbona umeacha hivi" ilikuwa ni jikoni, nikamjibu " hapa nina plan ya kuweka dish washer" baadae akauliza na hapa " nikamwambia hii ni laundry room, plan yangu ni kuweka washing mashine, drying mashine na meza ya kupigia pasi. Alichoniambia baada ya hapo kilinishangaza kidogo, alisema " ACHA MAMBO YA UZUNGU MZEE, JENGA SIMPLE TU". So hii ndio mentality ya wabongo wengi..tunaogopa "uzungu"
 
Kuamini mafundi nikiambiwa cement imeisha napiga simu tu inapelekwa bila kufatilia. Kuna siku fundi anapiga simu kuwa wamesimama kazi kwa kuwa cement imeisha inabidi ipelekwe haraka.

Ikabidi niende mwenyewe kuangalia kazi imefikiaje hadi cement kuisha hivo, nilivyofika mafundi wakastuka sana maana hawakutarajia kuniona kwa wakati huo. Ikawa kila ninapoingia kukagua jamaa kama ananizuga ili niache nimsikilize yeye. Nikahisi kitu nikaongeza umakini kuangalia chumba hadi chumba.

Bwana weee! Si nikakuta kuna mifuko 9 ya cement haijatumika wameificha kwenye chumba chooni. Asee jamaa alibabaika sana akakosa la kusema.
Mwisho wa siku ukaamuaje?

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Unapojenga zingatia vipimo SQM ni lazima upange ziwe ngapi kwenye nyumba nzima!,sasa mtu anaweza akajenga nyumba ya vyumba vitatu tu lakini ina SQM 150 sasa unajiuliza huyu mtu ametoka kwenye hospital ya vichaa ama vipi![emoji276]wakati unaweza ukajenga nyumba ya vyumba vitatu kwa Sqm zisizozidi 76,hivi unapojenga chumba kimoja mita 5 unataka tuzo ama vipi?
Kila siku nasema nyumba kubwa ina faida sana kuwatajirisha wauza vifaa vya ujenzi kuliko mwenye nyumba

Siriazi vyumba vitatu sqm 76!! Hapo sasa utakua umejenga nini!!,Hio nyumba itakua haina hewa kabisa na imebanana kila kona.standard vyumba vitatu ni sqm 150 ikiwa spacious inafika 200sqm,hii inaitwa medium size house.

Lakini kila mtu ana mapenzi yake ,kiukweli sipend nyumba yenye vyumba vidogo sana hii ni kutokana na nyumba niliyokulia kwa wazee,kipind hicho nipo form 6 naona kabisa chumba ni kidogo hakina hewa vitu vimebanana nikawa najisemea ikitokea nimefanikiwa kujenga yangu huko badae ntaongeza kidogo ukubwa.ila sio mita 5 hizo ni nyingi labda kwa masta.

Asikuambie mtu kuna raha ya kulala kwenye chumba kikubwa chenye hewa .
 
Wakati najenga nilikua nashinda site na nabeba hadi tofali mwenyewe ,siku moja fundi wangu akaongeza nguvu ya fundi mmoja na saidia wake nilipofika nikasalimia fresh nikaingia kusambaza tofali bwana bwana yule fundi mgeni acha aanze domo domo we unakuja kwenye kazi kibishoo traki safi nini we mtoto wa mama tuu me namchora tu ,fundi wangu akamwambia we ndie boss huyooo[emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]aliendelea na kazi kwelii
 
Siriazi vyumba vitatu sqm 76!! Hapo sasa utakua umejenga nini!!,Hio nyumba itakua haina hewa kabisa na imebanana kila kona.standard vyumba vitatu ni sqm 150 ikiwa spacious inafika 200sqm,hii inaitwa medium size house.

Lakini kila mtu ana mapenzi yake ,kiukweli sipend nyumba yenye vyumba vidogo sana hii ni kutokana na nyumba niliyokulia kwa wazee,kipind hicho nipo form 6 naona kabisa chumba ni kidogo hakina hewa vitu vimebanana nikawa najisemea ikitokea nimefanikiwa kujenga yangu huko badae ntaongeza kidogo ukubwa.ila sio mita 5 hizo ni nyingi labda kwa masta.

Asikuambie mtu kuna raha ya kulala kwenye chumba kikubwa chenye hewa .

Tatizo kubwa ni kukariri kiongozi!,chumba cha mita 3 ni kidogo?tatizo ni mazoea kwamba ni lazima nyumba iwe kubwa kama gulio ndio uonekane umejenga!,eti jamaa ana nyumba kubwa yule [emoji276]
 
Haya nyumba hii hapa 83 SQm ,ni matumizi mabaya sana ya akili na pesa kujenga nyumba ya vyumba 3 kwa SQM 150 ama 200 ni poor mind!,mwisho wa siku unatumia gharama kubwa pesa ambayo ilitakiwa uwekeze sehemu nyingine![emoji276],ni maaajabu sana tena sana kwa mtu mwenye kipato cha kati kujenga nyumba ya SQM 150 yenye vyumba 3,kuanzia SQM 150 kuendelea hiyo ni Guest house
IMG_2994.jpg
 
Tatizo kubwa tunalofeli watanzania ni upangiliaji wa vitu,sasa mtu unakuta kijiko chumbani ama jembe sebuleni linafanya nini!,jenga nyumba ndogo pangilia vitu vizuri utaondoa fikra za kujenga magodauni kwa kudhani ni nyumba
 
Kuna makosa kadhaa niliyafanya

1.Nilimuamini chalii mmoja kosa tu kasomea civil engeering nikq mtrust anichoree ramani kisha nikasafiri nje kidogo then nikawa tuma pesa ijengwe sikiwa na shaka coz aliye chora si ni engineer aisee niliporejea Bongo kuitazama lile boma yaan siku rizishwa nalo mosi vyuma vilikiwa vodogo, choo na bafu humo humo

Aisee sitokuja tena kumpa ndugu kazi ya ku deaign ramani au yoyote ile ya kuhusiana na ujenzi ata kama awe amesomea MIT, Oxford, ata Havard
 
UMejenga nyumba kwanini usiwe na plan ya tanki la maji? Lita 5,000 ama 10,000 linatosha kusukuma maisha kwa week nzima, ambapo inakuvusha hadi dawasco ama mamlaka ya maji ya mji wako watakapo toa maji tena in case kuna mgao.
Maji yanatoka kama mkojo ,pipa litajaa saa ngapi, alafu dawsco wana mtindo wakufungulia upepo badala ya maji , hiki kitendo kinapelekea bill kuja mpaka 70k, kwa mwezi,
 
Wazee wamejenga nyumba ya ghorofa moja master bedroom yao ipo juu sasa umri umeenda kupanda ngazi na kushuka kila siku kwenda chumbani wanaona shida

wamehamia chumba cha chini mdogo wangu ndo kahamia kwenye master bedroom juu


So ukijenga ghorofa baadae ukizeeka utarudi chini labda uweke lift [emoji28]
Na ndugu ya ni businessman aliweka lift Kwa sababu ni Mzee, lakini kabla hajakamilika aka rest in peace
 
A
Sema ukizeeka halafu hauna mazoezi!,kushindwa kupanda one floor labda uzee wa miaka 90+,lakini kama ulikuwa mtu wa mazoezi unapanda fresh tu,ndio maana kijijini unakuta mzee miaka 85+ analima na kufanya shughuli zake bila matatizo yeyote,ila mjini mzee miaka 65 yupo taabani
Anasa za dunia kaka, zinatupelekesha
 
Back
Top Bottom