Nimejenga underground iliyofanywa na fundi wa mtaani (local fundi), wakati wa kumwaga slab, kwenye wiring map ya umeme hawakuweka zile hook za feni (pangaboi), sasa baada ya kumiminwa slab juu hakuna mahali pa kufunga feni au la niweke mbao za dari ili nipate mbao ya kufungia hook, kitu ambacho ni hasara, maana nitakuwa na slab na bado nimeweka dari.
Ninalazimia kutumia feni za kusimama ambazo sizipendi na zinaleta ghasia tu, sijui kama inawezekana kudrill ili tuweke hook ya feni ili nifunge pangaboi.