Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Duh, mzee familia ya watu wangapii hiyo? Halafu maji kukatika mwezi mzima mbona ni nadra sana kwa hayo maeneo? Labda ukame kama wa mwaka jana
Mbezi kuna maeneo yana maji 24/7, yaani kuna kile kipindi maji yalikatika sana ila baadhi ya maeneo ni kama watu walikuwa wanaishi huko Masaki.

Familia yenye wanawake wengi na watoto hata ufanyaje matumizi ya maji yatakuwa makubwa sana.
 
Nilishauriwa Kujenga mashimo mawili ya choo,la square na duara ,sasa hivi wengi wananiambia naweza kutumia moja la duara,nawaza hili lingine la square kulifanya kisima cha kuvunia maji ya mvua .

sasa umbali wa shimo la maji taka na shimo la maji safi ni sqm moja ,japo hili la maji safi limesakafiwa ndani,wakuu huu ukaribu hautasumbua?
Amekushauri vibaya mkuu
Kila shimo lina kazi yake
Nakushauri ujenge yote

Na hilo unaloita la square linapaswa kuwa mstatili na ukiweza kutenganisha mabomba ya maji ya bafuni na jikoni yaelekeze moja kwa moja kwenye shimo la duara
 
Mchwa ndani ya nyumba nikiwazuia huku wanatokea huku japo nimepiga tiles ila wakipata upenyo hata crake tu yaani kama tunacheza kidali vile ukisahau kukagua furnitures na kuzigeuza mara kwa mara imekula kwako unakuta wamekula fisher board yote.
Kwa mnaojenga maeneo ya vichuguuni au maeneo yenye mchwa kabla ya kupiga jamvi au rough floor ya nyumba nzima hakikisha unapulizia dawa ya mchwa ndio upige jamvi/rough floor.
 
Pia mkumbuke kuzingatia uelekeo wa kuchomoza na kuzama kwa jua wa eneo husika sio kujenga tu kama ramani ilivyo.
Kuna block yangu ipo shambani hapo Mkuranga master bedroom ipo upande jua linapozama kwahiyo lile jua la jioni lote linatandika chumbani hivyo kama unataka kulala vizuri nasubiri hadi saa nne usiku ndio room inakua imepoa.
 
Kingine ni kuzingati slope ya kiwanja na uelekeo wa vyoo na eneo utakalo chimba mashimo ya vyoo hii ili nigharimu nikavunja msingi wote wa nyumba yaani fundi alivyokua kiazi vyoo vyote kaweka upande wa chini ambao hakutoshi nafasi ya kuchimba mashimo kwahiyo mashimo yange chimbwa ule upande juu wa mwinuko.
Hivyo kufanya bomba za septic kupanda mwiniko na ingekula kama bomba 5 ili kufikia mashimo.
 
Aliwah kusema hili swala pia the late JPM, ukisubiri uwe na hela ndo ujenge hutakaa utoboe,
Imagine 30milion unajua unachonoka na bonge la nyuma, kitu kikaishia kwenye gofu lenye mbao juu[emoji3][emoji3]
Ni kweli kwenye ujenzi ukisubiri pesa zijae huwezi kujenga hata siku moja ni busara kuanza na ulichokuwa nacho

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom