Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Aliyekuwa anamrekodi sio fundi hata! Ni rafiki yangu tu tena yuko vizuri mnoo, katikati ya storee zao ndo akaanza sasa kujisifia jinsi alivyonipiga[emoji849][emoji849][emoji848]

Asee nilishangaa sanaa
[emoji1787][emoji1787]
 
Hili limenikuta, lakini huyu fundi maku najua ntamkomeshea wapi!

Halafu rafiki yake kamtegesha loud speaker akawa ananisema vibaya, eti mi bahili na nalalia sana labor charge, kwahiyo ameniibia laki nne baada ya kupanga mbinu na supplier wa material

Namvutia kasi tu ngoja amalize ujenzi, hela ake simpi
Pole sana Mkuu, mafundi wengi wamekuwa sio waaminifu.

Kuna mmoja nilipoona ananiibia nikiwa mbali, nikafanya maamuzi ya kumpeleka Wife kusimamia.

Alichokifanya ilikuwa nikilipia kwa Supplier tofali 1000 basi yeye anamwambia Supplier apeleke tofali 750 badala ya 1000.

Hiyo siku nikatimba Site bila taarifa na nikaanza kuhesabu mwenyewe hizo tofali, mbona nilimtimua siku hiyo hiyo na huyo Supplier naye nikavunja mkataba naye pia.

Mafundi wanatuumiza sana Wajenzi, ujenzi wa Milioni 100 unaweza kuta unatumia milioni 120 usipokuwa makini
 
Pole sana Mkuu, mafundi wengi wamekuwa sio waaminifu.

Kuna mmoja nilipoona ananiibia nikiwa mbali, nikafanya maamuzi ya kumpeleka Wife kusimamia.

Alichokifanya ilikuwa nikilipia kwa Supplier tofali 1000 basi yeye anamwambia Supplier apeleke tofali 750 badala ya 1000.

Hiyo siku nikatimba Site bila taarifa na nikaanza kuhesabu mwenyewe hizo tofali, mbona nilimtimua siku hiyo hiyo na huyo Supplier naye nikavunja mkataba naye pia.

Mafundi wanatuumiza sana Wajenzi, ujenzi wa Milioni 100 unaweza kuta unatumia milioni 120 usipokuwa makini
Asee ni noma sana....hivi fundi mi nimeamua kukupa ridhiki bado unaniiibia?

Mi ntakomaa nao hawa wapuuzi
 
Asee ni noma sana....hivi fundi mi nimeamua kukupa ridhiki bado unaniiibia?

Mi ntakomaa nao hawa wapuuzi
Inabidi uwe bandidu unapodeal na mafundi wa kibongo, otherwise unaweza kuta ujenzi usikamilike na hela zikawa hazitoshi kukamisha Ujenzi
 
All the best Mkuu, najua utakuwa umeupitia uzi waliomtaja rafiki yako Kigosi kuhusu Kujenga. Wewe umejikomboa tayari [emoji122][emoji122]
Hahaha ndio mkuu....na nimediss hataree[emoji1787][emoji1787]
 
Sana Mkuu, alafu hajui mali ya wizi hata huwezi kuifanyia jambo la manufaa.

Hao mafundi wameniibia lakini hakuna cha ziada wamefanya zaidi ya kwenda kulewea hela zangu pamoja na kuhongea mademu.

Saivi nikitaka kujenga ni vyema niweke kambi hapo hapo hadi Ujenzi uishe kwa hatua niliyopanga
Nimekuelewa

Kitu nilichojifunza kwenye ujenzi wa nyumba ya kwanza unakupa uzoefu ambao utautumia kwenye ujenzi mwingine

Kuna baadhi ya makosa hautayarudia
 
Hahaha ndio mkuu....na nimediss hataree[emoji1787][emoji1787]
Ndiyo ufanye kumkumbusha hata kiutani ajenge, mwambie kama wewe Ke umejenga yeye Me anashindwa nini😅, ikitokea mkagombana kwa kauli hiyo mimi nitajitolea kuwa mpatanishi wenu 🤪🏃🏃🏃
 
Ndiyo ufanye kumkumbusha hata kiutani ajenge, mwambie kama wewe Ke umejenga yeye Me anashindwa nini[emoji28], ikitokea mkagombana kwa kauli hiyo mimi nitajitolea kuwa mpatanishi wenu [emoji2957][emoji125][emoji125][emoji125]
Hahahahhhaha sawa mkuu
 
NINA MAKOSA KADHAA NGOJA NIYAWEKE.
Kosa la kwanza!
Kiwanja sikununua nilipewa na Bi. Mkubwa(Mama mzazi) na tayari nilishakuwa na Milioni saba ninazo za kuanzia ujenzi hivyo nikamwita fundi mchundo nikampeleka site aanze ujenzi. Kosa ni kwamba sikumtafuta mchora ramani wala Engineer niliona ni kupoteza pesa tu.
Fundi mchundo kufika site akachukua karatasi na peni akachora ramani ya harakaharaka na akapima uwanja kesho ujenzi ukaanza.
Kile kiwanja kilikuwa cha muinuko na lazima ili usingi ukae sawa utoe underground ya chumba kimoja au viwili kwa ufanisi zaidi. Fundi akashauri eti tutaweka vifusi kujazia zile underground na sio tuweke vyumba. Kasheshe msingi ulipokaa sawa kila akipiga hesabu ya kuweka kifusi anaona kabisa haiwezekani kwa maana nafasi ya ground ni kubwa kifusi lazima kitavunja ukuta.
Nikapata hasara ya kujenga underground, ambayo kama ningechorewa ramani ningejiandaa toka mwanzo. Nikalazimika kutoa underground ya chumba kimoja kile cha pili kwa vile kilijua juu kidogo kuogopa gharama nikajazia kifusi. Bajeti ya msingi iliongozeka kwa zaidi ya milioni 1.5 kwa kuweka underground.
Kumbuka underground lazima umwage zege na nondo kama unajenga ghorofa.
KOSA LA PILI
Kwenye hatua ya kusimamisha Boma nikahamishwa kikazi mkoa mwingine hivyo nikawa najenga kupitia simu yaani Fundi ananiambia kinachohitajika nami namtumia pesa, halafu tukakubaliana Boma litaisha kwa siku tano na pesa nimlipe ya siku (daily pay) aisee ile kazi ilikuja kuisha kwa wiki mbili maana Fundi alikuwa anafanya kazi ikifika saa nane anaondoka sababu kibao. Na nilipigwa kwenye malighafi maana nilikuwa natuma pesa tu kwake.
Hapa nilijifunza kama unataka kumlipa Fundi kwa kila siku itakulazimu ushinde site au umtafute msimamizi.
KOSA LA TATU
Ramani ya nyumba niliochelewa na Fundi mchundo ina vyumba viwili tu vya kulala labda ukiongeza na ile underground ndio inakuwa vyumba vitatu. Na sio kama eneo halitoshi ila nadhanj kwa vile sio fani yake maana kaacha eneo kubwa tu la kutoa chumba kizima.
Sasa huwa nikipata nafasi nakwenda site na wanangu, wawili wa kike na mmoja wa kiume ambae ndio mkubwa wao. Sasa mwanzoni nilipanga yule wa kiume ndio atakuwa analala kwenye hiyo underground lakini ameniambia baba fanya ufanyavyo ila mimi sitalala huku bondeni kwenye banda la kuku akimaanisha ile underground.
Maana kile chumba kimejitenga kabisa na vyumba vya ndani, na siwezi kuweka watoto wa kike kule nitakuwa nimewatoa sadaka kwa vijana wa kiume watachangamkia fursa.
Nimepanga na mama watoto ile underground tuifanye stoo hakuna namna, mpaka sasa kichwa kinaniuma mwanangu wa kiume atalala wapi? Kuna muda wife ananitania eti tugawane vyumba yeye alale na watoto wa kike na mimi nilale na mwanangu wa kiume ili vyumba vitoshe.
Hiyo nyumba ramani yake pia ina jiko, dining, sebule, choo cha master na choo cha public.
Na siwezi kuua dining au jiko nifanye chumba kwa kuwa ni nafasi ndogo haitatosha kabisa.
Haya ndio makosa nilioyafanya kwenye ujenzi wa nyumba yangu ila nimejifunza vitu vingi sana kwenye ujenzi ambapo kama nitabahatika kujenga nyumba nyingine makosa haya hayatatokea tena.
 
Huu ujenzi wa "kupigiana simu na fundi" unawagharimu wengi sana. Mtu yupo Mbeya kikazi anajenga nyumba Dar, watu wanaumizwa sana. Hakuna fundi siyekuwa mwizi, wanatofautiana viwango tu, ila maisha yao ni magumu(wengi wao) so option iliyopo ni kuiba.

Nilichonote ni kuwa mafundi wengi hawajui kufanya makadirio, yaani mpeleke site mwambie akadirie materials, wengi wanaangukia chaka tu. Hivyo, ukijenga pamoja na tathmini ya fundi ongeza % fulani kwenye gharama zako ili usiishie njiani.

Ukiona fundi anashindwa hata kusoma ramani, manake hata hesabu ya vifaa hawezi. Mfano, kama unataka kupaua, fundi akija, don't show him ramani yako, mwambie akupe roughly paa litakaa vipi, ukiona manyanga tafuta namna nyingine.

Jenga na simamia mwenyewe, kuwa site, ikiwezekana kama ni mwajiriwa tumia muda wa likizo kufanya hivyo, nenda kwa supplier nunua materials mwenyewe, zikija site kama ni kuzihesabu do it. Hii itasaidia kupunguza wizi.

Tatizo linakuja kama huna ABCs za ujenzi, akikosea huwezi kumrekebisha, akipindisha ukuta hutajua nk. Ila ukiwa na abcs akikosea hapo hapo unamwambia, wanakasirika lakini that's part of it, hata huko kwa wachina wanashusha ukuta na kuanza upya wakikosea.
 
Back
Top Bottom