Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Umenikumbusha mbali. Wakati niko mdogo (shule ya msingi), nilipokea barua ya babu shuleni. Wakati huo mawasiliano ni ya barua tu (S. L. P. la shule ama kijiji). Hakukuwa na simu wala internet. Basi katika utoto wangu, nikafungua bahasha na kuisoma ile barua. Kulikuwa na sh 20/= ndani yake. Alikuwa ametumiwa babu na mjukuu wake aliyekuwa anafanya kazi mjini. Baada ya kuisoma, nikampa mpwa wangu aipeleke nyumbani ikiwepo ile sh 20/=. Mimi nilikuwa nakwenda sehemu nyingine wakati yeye alikuwa anaelekea nyumbani.
Ilipofika nyumbani ile sh 20/= haikuwemo. Basi akatafutwa aliyeichukuwa. Yule mpwa wangu akasema ni mimi. Ni kweli nilisoma barua lakini sikuchukuwa ile sh 20/=. Mi nikakataa kuwa sikuichukuwa. Mpwa anasema ni mimi niliyeichukuwa. Basi nilipigwa kipigo cha mbwa mwizi (Mroto = mbwakoko). Bahati mbaya yule mpwa wangu alifariki utotoni. Angekuwepo sasa, ningemkumbusha siku moja.