Ni kozi gani ukimuona mtu anasoma chuo unabaki unasikitika?

Ni kozi gani ukimuona mtu anasoma chuo unabaki unasikitika?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Kuna kipindi Nilikuwa nataka kusoma kozi ya Basic Records & Archives Management. Wiki chache kabla ya ku-apply nikakutana na mjomba angu mmoja kasoma soma kidogo. Nikamuelezea nilichokuwa nataka kusoma

Badala ya kunipa support akainama akaniuliza "Kwa jinsi internet inavyoshika kasi duniani unadhani ni kampuni itakayomlipa mtu mshahara wa kupanga mafile wakati taasisi zote zinaingia kwenye mifumo ya e-office?"

Sikuwa na cha kumjibu ila nilibadilisha uamuzi

Nyie vipi, ni kozi gani ukisikia mtu anasoma unasikitika?
 
KIla kozi inaumuhimu.
Ah wapi zipo kozi nyingine hazina mantiki, ukizingatia vijana wengi wanasoma Tz wanawaza kuajiriwa.

Unakuta eti

"Bachelor of Life Long Learning & Community Development" kuna dogo nilimwambia thubutu.

Eti "Bachelor of Public Administration and Youth Development ". Labda kwa vile serikali imeibuka na wizara ya vijana.

Eti "Bachelor of Development Studies" 🤔

Kuna kozi nyingine inafaha usome ukiwa una mipango yako mingine binafsi. Ila kama target ni kuwin soko la ajira utalia na kusaga meno.
 
Nimesoma computer science nafanya data science, data analytics ,machine learning lakini naomba kazi sipati nashindwa kuelewa kipind icho najua instructional design content 😀 lakini nashindwa kuelewa kwamba shida nini
Akili yako umeiseti kusjiriwa tu fanya content au freelance kazi kibao
 
Nimesoma computer science nafanya data science, data analytics ,machine learning lakini naomba kazi sipati nashindwa kuelewa kipind icho najua instructional design content 😀 lakini nashindwa kuelewa kwamba shida nini
Wewe ni mzembe sana.
Kuna vijana wa form 4 wanajiongeza na kupiga hela mitandaoni kupitia hizi mambo halafu wewe umezubaa unangoja kuajiriwa
 
Wakuu,

Kuna kipindi Nilikuwa nataka kusoma kozi ya Basic Records & Archives Management. Wiki chache kabla ya ku-apply nikakutana na mjomba angu mmoja kasoma soma kidogo. Nikamuelezea nilichokuwa nataka kusoma

Badala ya kunipa support akainama akaniuliza "Kwa jinsi internet inavyoshika kasi duniani unadhani ni kampuni itakayomlipa mtu mshahara wa kupanga mafile wakati taasisi zote zinaingia kwenye mifumo ya e-office?"

Sikuwa na cha kumjibu ila nilibadilisha uamuzi

Nyie vipi, ni kozi gani ukisikia mtu anasoma unasikitika?
Hayo mambo ya kukariri ni shida sana,hapa ofisini kwangu mimi kuna watu 2 mwaka huu wamepata ajira kwa kazi hiyohiyo,paper work kuieliminate kabisa itachukua miaka mingi sana hasa huku kwetu Africa...
 
Back
Top Bottom