NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Huwa nashangaa sana baadhi ya wakristo kulazimisha ukaribu na taifa la Israel kujidanganya kwamba dini ya kikristo inawaunganisha,
Wengine wamefika mahala kuweka bendera ya taifa la Israel makanisani, kwenye vyombo vya usafiri, wallpaper za simu, n.k.
Wayahudi sio wakristo na wanampinga Yesu kwao hawamtambui, ila nguvu wanayotumia wakristo kulazimisha ukaribu na wayahudi inashangaza sana kiasi cha kuonekana wazi wakristo wanajipendekeza maana wao wayahudi hawautambui ukristo
Mjumuisho wa dini ya kikristo israel ni kwamba asilimia 1 tu ni wakristo, yani hapa katika waisrael 100 kuna mkristo moja tu.
Kwao hawamtambui Yesu kwamba alikidhi vigezo vyao kwahio hawautambui ukristo lakini hali ilivyo kwa mataifa ya kikristo ni kama wanajipendekeza sana kuwa karibu na waisrael ambao wao hawautambui ukristo .