Aisee mimi nmeondoka home 1998 baada ya kumaliza kidato cha nne,nilikuwa napapenda sana home hadi leo napapenda sana ila pale home dingi alikuwa na mgongoro wa ardhi na mama mmoja jirani yake kiasi kwamba kila mara walikuwa wakipelekana mahakamani na dingi mara zote alikuwa anashinda.
Yule bibi alikuwa mtaalamu wa kutengeneza matukio ya ajabu hasa ya kuonekana anaonewa ili serikali na jamii iwe upande wake na sisi kama vijana tulikuwa upande wa baba tukiona kweli anaonewa.Sasa bwana kuna siku nyumba ya huyo bibi ilichomwa moto japo inasemekana huyu bibi na kijana wake walichoma wenyewe,
ikawa washukiwa ni dingi na bro wangu wakakamatwa na kukawa tetesi kuwa yawezekana na mimi nilishiriki zoezi hilo.Mama yangu alivosikia tetesi hizo na ndo nimemaliza shule alifanya mpango na kunitorosha usiku wa manane na kunipandisha bus alfajir kwenda mkoa mwingine ambao niliendelea na masomo na baadae kazi,familia na maisha yangu yakaanzia hapo hadi sasa.
Kesi ya mzee na bro ilichukua muda sana Kwan walikaa ndani mno ukizingatia vijana wa yule bibi walikuwa na pesa waliitumia vilivyo kuhakikisha wanakandamiza familia yangu,kesi tulikuja kushinda na kuonekana hatuna hatia but mzee alitoka huko jela tayari amekata tamaa na hakukaa muda mrefu,alifariki.
Nipo mbali na home na wala sijawahi ht kuwaza kujenga kibanda changu huko,nimebaki kumfanya mama yangu aishi km malaika hapo nyumbani kwake alikomwacha mzee,but kisasi changu bado kipo rohoni