Ni kumbukumbu ipi unaikumbuka siku ulivyoondoka kwenu na kilichokufanya uondoke kwenda kuanza maisha ya kujitegemea?

Mimi nilitoroka, hakuna aliyekuwa anajua zaidi ya mdogo wangu,ilikuwa mwaka 1997, nilikuja kuwapa taalifa baada ya mwezi mmoja,mwaka 2000 nikapita kutoka bandalini na gari zangu mbili,niliwaacha mtaani vijana wamechanganyikiwa
 
Mimi binafsi namaliza mwaka wa3 chuo naaapa nikirud sikai home ni bora nikose kazi ya udaktari lakin nitafanya kzi yyte ila sio kukaaa home nitapambana tu
 
Mimi binafsi namaliza mwaka wa3 chuo naaapa nikirud sikai home ni bora nikose kazi ya udaktari lakin nitafanya kzi yyte ila sio kukaaa home nitapambana tu
Upo muhimbili sio 👻
 
Nasoma tu hapa comment zenu naona wengine mpo na wazazi wote wawili na madogo kama hivyo.
ILA me nipo na mzee tu namsaidia kazi za hapa na pale ila hizi dharau zake zinanifany niweke ahadi moyoni kwamba siku nikiondoka hapa.

Ataniona tu kwenye picha.
 
Aisee mimi nmeondoka home 1998 baada ya kumaliza kidato cha nne,nilikuwa napapenda sana home hadi leo napapenda sana ila pale home dingi alikuwa na mgongoro wa ardhi na mama mmoja jirani yake kiasi kwamba kila mara walikuwa wakipelekana mahakamani na dingi mara zote alikuwa anashinda.

Yule bibi alikuwa mtaalamu wa kutengeneza matukio ya ajabu hasa ya kuonekana anaonewa ili serikali na jamii iwe upande wake na sisi kama vijana tulikuwa upande wa baba tukiona kweli anaonewa.Sasa bwana kuna siku nyumba ya huyo bibi ilichomwa moto japo inasemekana huyu bibi na kijana wake walichoma wenyewe,

ikawa washukiwa ni dingi na bro wangu wakakamatwa na kukawa tetesi kuwa yawezekana na mimi nilishiriki zoezi hilo.Mama yangu alivosikia tetesi hizo na ndo nimemaliza shule alifanya mpango na kunitorosha usiku wa manane na kunipandisha bus alfajir kwenda mkoa mwingine ambao niliendelea na masomo na baadae kazi,familia na maisha yangu yakaanzia hapo hadi sasa.

Kesi ya mzee na bro ilichukua muda sana Kwan walikaa ndani mno ukizingatia vijana wa yule bibi walikuwa na pesa waliitumia vilivyo kuhakikisha wanakandamiza familia yangu,kesi tulikuja kushinda na kuonekana hatuna hatia but mzee alitoka huko jela tayari amekata tamaa na hakukaa muda mrefu,alifariki.

Nipo mbali na home na wala sijawahi ht kuwaza kujenga kibanda changu huko,nimebaki kumfanya mama yangu aishi km malaika hapo nyumbani kwake alikomwacha mzee,but kisasi changu bado kipo rohoni
 
Aisee mimi nmeondoka home 1998 baada ya kumaliza kidato cha nne,nilikuwa napapenda sana home hadi leo napapenda sana ila pale home dingi alikuwa na mgongoro wa ardhi...
Pole sana Nyalumana,

Ungemuhamisha Mama huko aliko nimehisi huruma juu yake alivyobaki kwenye kumbukumbu mbaya ya kumpoteza mpendwa wake na bado anamuona adui yake.

Usifanye kisasi cha kuja kukutia hatiani historia ikajirudia.
 
Achana na Visasi Mkuu,Nina jirani nimekuwa namshika Sana mkono inasemekana alikuwa na vyeti fyeke vya bwana jiwe..Basi Mimi ninafuga kuku kwangu na yeye anafuga kuku kwake,,Sasa kuku wake mmoja ikawa hajui anatagia kusikofahamika jamaa akawa ananishutumu Sana kupitia wanangu yaan akiwaona wanangu anawaambia mnakula mayai Yangu,,Mara mnakula kuku wangu aisee..


Nimekaa muda mrefu sijaenda kumtembelea juzi nikaenda kumsabahi nafikiri amejifunza kitu,,na hakuamini Kama ningekwenda kwake maana mgogoro ulifukuta Sana mpk nikajenga bonge la uzio....


Achana na kisasi ,,unaweza kukosa furaha ya maisha milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…