Ni kutojitambua mwanaume ukikimbiwa na mwanamke kwa sababu za kiuchumi

Ni kutojitambua mwanaume ukikimbiwa na mwanamke kwa sababu za kiuchumi

Usikariri kuwa kila mwanaume anae kimbiwa au Kutalakiana na mke wake ni kwa sababu mme ka-lost! Mfano Jeff Bezos, Bill Gates, Roman Abramovich, Kanye West......!
 
kwahiyo baba unatushaurije sisi wanawake ambao waume zetu wamefulia, vipi tubaki tukiwavumili ili wapate waje kutusumbua na michepuko yao, au tutimue mbio bila kugeuka nyuma!!?
 
Usikariri kuwa kila mwanaume anae kimbiwa au Kutalakiana na mke wake ni kwa sababu mme ka-lost! Mfano Jeff Bezos, Bill Gates, Roman Abramovich, Kanye West......!
Umeelewa uzi au umedandia? Huu uzi ni juu ya wanaume wanaolia na kulalamika kuhusu kukimbiwa na wake zao baada ya kipato kuyumba
 
kwahiyo baba unatushaurije sisi wanawake ambao waume zetu wamefulia, vipi tubaki tukiwavumili ili wapate waje kutusumbua na michepuko yao, au tutimue mbio bila kugeuka nyuma!!?
Changanya vizuri karata zako na piga mahesabu vizuri maana huko uendako hakuna guarantee! Uamue ama kukaa na huyo mumeo ufe na umasikini; au ubusti ubongo wa mumeo aone fursa mtoke wote!; au kama aelewi na wewe una plan B sepa! We want men to come to their senses! Ms R
 
Changanya vizuri karata zako na piga mahesabu vizuri maana huko uendako hakuna guarantee! Uamue ama kukaa na huyo mumeo ufe na umasikini; au ubusti ubongo wa mumeo aone fursa mtoke wote!; au kama aelewi na wewe una plan B sepa! We want men to come to their senses! Ms R
great thinker,, what a marvelous answer 😌🤼‍♀️ thanks
 
Ni kutojitambua mwanaume ukikimbiwa na mwanamke kwasababu za kiuchumi alafu unaanza kulalamika na kulialia eti mke wangu kanikimbia!!! Ulitaka afanyeje? Mti ukimea kando ya kijito cha maji jani lake litakuwa bichi na utazaa matunda yake kwa misimu yake yote. Lakini pindi kijito kikikauka uwe na uhakika mti nao utakauka na kufa! Kwa mukutadha huu mti ni mke kijito ni mme!

Tofauti ya mti na mwanamke ni uwezo wa kutembea (movement) laiti mti ungekuwa na uwezo huo ungekimbia hicho kijito. Sasa mwanamke mbali na uwezo wa kutembea lakini ana akili! Mwanamke hawezi kuona kijito kimekauka alafu akakaa hapo afe eti kwasababu ameolewa wakati ana akili anaona wanaume wengine wanaoweza kumpa mahitaji yake.

Sasa uamuzi wa je! kuwaendea hao wanaume wengine kwa mahitaji yake kutakuwa endelevu na kumpa mustakabali (future) ya kuishi ama la! ndo changamoto kwa huyo mwanamke maana hasipochanganya karata zake vizuri mwisho wa siku anaweza kuangukia pua. Kama mkeo ana upeo na wewe mwanaume umeonyesha kwa vitendo HUNA uwezekano wa kujinasua na shida iliyowakumba nakuhakikishia mke atakukimbia.

Hii ni kwamba kama mme utakuwa na maneno matupu yasiyokuwa na mashiko kuhusu mustakabali wake au wenu, mwanamke kukukimbia ni BUSARA TOSHA na ya hali ya juu! Sasa mwanamke atakaaje na mwanamme asiye na njia ya uhai (kijito cha maji kilichokauka?). Ebu wanaume tuwe wakweli; kwamfano: ukiwa na ukwasi ukapanga nyumba nzuri alafu ukashindwa kulipa kodi si unafukuzwa?

Ukiwa unamiliki gari kubwa (Landcruiser V8) alafu ukaishiwa uwezo wa kulijaza mafuta na service, si linaharibika?Ukiwa umeajiriwa alafu usienende na matazamio ya mwajiri si unafukuzwa kazi? Kama umeweka heshima Bar alafu ukaanza kupunguza uwezo wa malipo kuendana na umakini wa huduma wanayokupa pamoja na "tips" unazoachia Barmaid, uwe na uhakika next time unaweza kukosa parking na kiti. Sasa kukimbiwa na mke kwa kushindwa kumpa mahitaji uliyomuaminisha wakati mnaingia mahusiano, akikumbia imekuwa NONGWA? Be serious guys! Pamoja na kwamba nguvu ya kiuchumi ya mwanaume ni nguvu ya ulimwengu wa kimwili unaoonekana; lakini mwanaume anayo pia nguvu ya kiroho.

Ukipoteza nguvu ya kimwili bado unaweza kummudu mke kwa kutumia nguvu ya kiroho na mke akakaa na wewe katika kipindi hicho cha ugumu wa maisha bila kujali ni cha muda mfupi au ndo basi tena mpaka mwisho wenu.

Wanaume tuchukue nafasi zetu zimeporwa na shetani! Mwanaune ukipoteza nguvu za kimwili (uchumi) alafu nguvu za kiroho zikashindwa kuleta mahitaji ya muhimu kama chakula mezani, mwanamke uhamua kwenda kwa wachawi au kwa mizimu ya kwao au kujichukulia sheria mkononi kukutanguliza mbele ya haki (RIP) maana kaona kabanwa kila kona.

Leo ni siku ya wanaume inabidi kutafakari wapi tulipojikwaa? Happy Men's Day
Poa umesomeka
 
Mtoa maada ukosahihi lakin ingekuwa hivo ulivosema wew ndo inavotakiwa iwe kwenye jamii,inawezekana hata Mama yako kuna kipindi ange mkimbia baba yako.
Pia Mwanaume anayependa uhai wake na future nzuri ya familia yake hapaswi kufanya vitu ili mkewe asimkimbie,maana njia za utaftaji sio rahisi kuzicontrol etikisa una wanaokutegema vingnevyo utakufa na sonona.
Kwa upande mwingine WANAUME tuache kuwalilia wanawake wanapotukimbia kama tunaviwango vya chini kuliko wanavyotaka tuwaache waende kiroho safi.
Wanawake tumieni haki yenu ya msingi msikubali kuishi na wanaume marofa wasio weza kuwahudumia kadri mnavyotaka,ilihali mnauwezo wa kuwakimbia na kwenda kuishi yasiyo mzigo.
 
Back
Top Bottom