Ni kwa asilimia ngapi ukizaliwa familia ya kifukara unaweza kutoboa?

Ni kwa asilimia ngapi ukizaliwa familia ya kifukara unaweza kutoboa?

Maisha ni timing na uwezo kucheza na nyakati bila kusahau bidii na uvumilivu katika kila harakati za utafutaji. Pia kumbuka hauwezi kupata mafanikio bila kupitia changamoto za kukatishwa tamaa kuchekwa kudharaulika kuchukiwa zengwe na fitna, ukiweza kuvuka hapo basi mbele nyeupe...............wachawi wapo sehemu zoteView attachment 2788198
Umeongea point kubwa. Vijana wakikutana na dharau na wao wanapandisha mabega na kudai bora wale makande kuliko pilau la masimango. Wanashindwa kujua kuna wakati inabidi ule pilau la masimango huku ukijipanga kimyakimya.
 
Kuna mambo mengi yanayomfanya mtu atoboe kimaisha hata kama umezaliwa fukara kabisa. Kati ya hayo kuna kitu kinaitwa "bahati". Hii ndio mpango mzima, sema tu ni vile huwezi kuikuta inauzwa dukani ukainunua.
 
Kupata utajiri ni mipango ya mungu sio mipango yako wapo watu walio zaliwa kwenye ufukara leo ni matajiri na wapo walio zaliwa kwenye utajiri leo ni mafukara,likini sikulazimishi kuamini haya
Ni Mungu na sio mungu ndugu.
 
Kuna mambo mengi yanayomfanya mtu atoboe kimaisha hata kama umezaliwa fukara kabisa. Kati ya hayo kuna kitu kinaitwa "bahati". Hii ndio mpango mzima, sema tu ni vile huwezi kuikuta inauzwa dukani ukainunua.
Bahati = fursa iliyokutana na maandalizi.

#YNWA
 
Jitazame kwa ndani ukiona huwezi jua hata kwa nje huweze binafsi Mimi najiona tajiri

Umasikini upo katika Akili Kama hauna magonjwa Makubwa yakukufanya ulale ndani then ukawa masikini Basi Hilo ni tatizo lako na sio Familia yako

Then ile hali ya kukosa hela mpaka ya kula huwa tunairuhusu sisi Wenyewe.
Nashukuru kwa kuniponya moyo wangu..yaani unapaswa kujitazama ndani yako. Ukiona huwezi ndani inamaanisha kiukweli hauwezi in physical manner.
 
Kupata utajiri ni mipango ya mungu sio mipango yako wapo watu walio zaliwa kwenye ufukara leo ni matajiri na wapo walio zaliwa kwenye utajiri leo ni mafukara,likini sikulazimishi kuamini haya
Dah! Yaani kwa fikra hizo bado tuna safari ndefu mzee. Kwa hiyo kama ni mipango ya Mungu, itabidi tukae tu kusubiri hiyo mipango? Kwamba mpaka pale Mungu atakapotujalia? Ukiwa na hiyo mindset ya "majaliwa ya Mungu" utakufa masikini mpaka kizazi chako chote. Ni Iman mbaya sana hiyo anayowatafuna watu kila siku. Mtu unakaa hauna mipango yoyote alafu unasema utajiri ni mipango ya Mungu? Are you serious??
Mimi naamini kuwa kitu cha kwanza katika kuondokana na umasikini ni kubadilisha fikra zetu kwanza. Ni kuondoa ile dhana kuwa " sisi tumeumbwa kuwa masikini, Mungu ndio ametujaalia umasikini". Tukiweza kuwa fikra positive, then kila mmoja wetu anaweza kuwa na maisha bora sana sio lazima wote kuwa matajiri but at least we can afford our basic needs.
 
Aiseee wewe ni kamanda
Jiambie kwamba lazima utoboe. Lakini unatakiwa uwe na uwendawazimu fulani hivi ili uweze kutoboa kama umetoka familia maskini. Kwa akili za kawaida haiwezekani. Kaa mbali na anasa zote na pia achana na kuoa fukara mwenzako kwa kujifariji mna mapenzi ya kweli kwamba mtaanzia chini. Kwa kijana uliyetoka chuo jipe muda wa kutafuta hela kwanza. Ila kama manzi yuko fresh kifedha yeye binafsi hadi familia yake muoe upate mtaji.
 
Katika hali ya kawaida ukizaliwa familia fukara kutoboa ni muujiza! Utaanzaje kwa mfano kutoboa! Tupe uzoefu wenu!
Mengi katoboa wakati mdogo alisema walikuwa wanalala na ngombe, shuleni alikuwa anaenda peku, diamond naye kakulia shida sa hivi si unaona alivyonona, Kama hipo hipo tu kikubwa mapambano na uzima.
 
Katika hali ya kawaida ukizaliwa familia fukara kutoboa ni muujiza! Utaanzaje kwa mfano kutoboa! Tupe uzoefu wenu!
Tatizo una akili ambazo unafikiri Kwa kutumia masabuli!!
Mm nimezaliwa Familia maskini kabisa!!
Tena Baba allinikataa! na Mama aliolewa na mwanaume mwingine. Hivyo Mimi nilelewa na Bibi Mungu amlaze mahali pema Bibi yangu!!
Niliishia Elimu ya msingi. Lakini nilisoma QT mjini Moro Kwa Rikado maria,( peku peku) niliishi Moro takribani miaka 19

Nikijidhughulisha na shughuli mbali mbali. Ikiwepo kufuga kuku, na nilipata tenda ya kupeleka nyama ya ngo'mbe kwenye chuo kikuu kimoja hapo mjini Moro.

Lakini alikuja COVID-19 ilinirudisha nyuma Kwa kiasi kikubwa!! Sikukata tamaa!! Nikarudisha mpira Kwa kipa. Nikarudi Singida. Singida tuna neema ya mabwawa mengi!! nikajiingiza kwenye shughuli za uvuvi. Kwa kifupi mpaka Sasa namiliki million 50 nipo Tabora Loya..
Acha kukariri dogo! Mungu ni mwema Kwa Kila mtu!!
 
Paka Sasa Nina kampuni ya uvuvi, na nina watu zaidi ya 30. Kwahio hio hata ukizaliwa familia maskini, lakini Bado unanafasi ya kufanya vizuri!! We mtangulize tu Mungu!!
 
Mungu atujalie wakuu tufanikiwe,kuwa masikini tumechoka
 
Back
Top Bottom