DiasporaUSA
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 23,382
- 29,639
Naitwa Lambert Franklin HarrisonWakuu salama..!!
Je, ingekuwa ni utashi wako ungejiita jina lako hilo hilo.?
Nimeanza na ulizo hilo, kwa maana katika nyakati za ukuaji imebainika watu huweza kujipachika majina tofauti tofauti kulingana na mazingira au matakwa ya nyakati.
Si ajabu kwa kila mmoja wetu, basi tuseme wengi kama sio wote, tumewahi kujiita majina mbalimbali.
Mfano majina ya watu maarufu tuliowaona kwenye filamu, au hata vibonzo na wanyama wakali.
Pamoja na ukweli kuwa majina ni utambulisho tu, lakini kuna kipindi tumewahi kuhisi kuna majina mazuri na mabaya. Hivyo tumewahi kutamani jina fulani au kuchukia lingine.
Kwa kuwa tunapewa majina tukiwa wadogo sana, hii haitupi haki ya kuchagua majina tuyapendayo. Hii hutulazimu kutii na kukua hivyo, na pale tunapopata kujitambua wengi wetu tumekuwa tukijaribu kubadili majina yetu.
Mifano ni mingi ila mojawapo ni ID za JF, na hata zile mnaita ‘a.k.a’ za almaarufu ni ushahidi tosha wa kutaka kubadili jina, japo vyeti vitabaki na majina asilia ila huenda kuna namna roho yako inatamani vinginevyo.
Hebu niulize tena, ingekuwa unazaliwa unaachwa ukue bila jina, hilo ulilojichagulia sasa ndo ungependa uitwe.?
Kuna jina zuri na baya.? Ooh jina lako zuri (kinafiki likiwa baya huambiwi), ooh jina lako gumu, oooh jina lako refu etc. [hapa tafadhali tujali matamshi tu, sio nguvu za jina kiimani].
Jina lako ulilopewa na wazazi wako, unaridhika nalo au unatii tu na kuheshimu wazazi au kwamba huna namna ya kufanya.?
Cheers [emoji1635]
Jina moja la kibabe sana
Sent using Jamii Forums mobile app