Ni kwa kiasi gani unaridhika na jina lako ulilopewa na wazazi wako?

Naitwa Lambert Franklin Harrison
Jina moja la kibabe sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
‘Wengi wenu’.

Akiwa hivi anajitambulisha vile, mara huku vile.... eti ana jina la nyumbani na la kutokea [emoji16][emoji16][emoji16]
Mimi natambulika kwa jina moja tu
Hili jingine wazazi hupenda kuniita Mara chache Sana.. Tena huunganisha yote matatu.

Character yangu ni ileile sehemu zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri au ubaya wa jina hutegemea thamani ya mwenye jina hilo, wapo watu waliopewa majina ‘magumu’ ila wameyabadili majina hayo na kuwavutia wengi.

Jina kama Dangote sijui Mengi sijui Magufuli hakuna mtu angeyatamani bila kujua thamani ya wenye nayo, siku hizi kila mzazi anatamani aite mtoto wake Obama sijui Mufuruki.

Wengi hatujui hilo, tunachagua majina mazuri ili tufurahie, hakuna jina zuri wala baya au gumu.

Jina langu hili hili nikilijaza thamani mbona litakuwa rahisi na tamu kutamkwa [emoji39][emoji39][emoji39]
 
Hoja hapa sio kukataa majina, kukubali au kukataa kuna sababu nyingi nyuma yake.

Hapa ni ile tu hali ya kuwa umewahi japo kutamani jina lingine, iwe kiutani au kitoto au ni kweli unafurahia mno jina lako.

Kama hivi kujiita kwenye mitandao, hata kama sio lazima uwe incognito mfano fesibuku na Instagram lakini utakuta huandiki jina lako kwa usahihi.
 
Nilivyokua mdogo nilikua silipendi jina langu. Gumu lazma umtajie mtu zaidi ya mara moja ndo aliskie, kuandika wengi walikua wanakosea, wengine wakawa wanali modify kulitamka wanavyotaka. Nilikua nakasirika sana nikiwa form 1 nikamfata shangazi nikwambia mimi hili jina silitaki twende RITA tukalibadilishe officially. Akaniangalia akasema hilo ndo jina lako. Mengi yamekua attached na hilo jina. Bahati etc usibadilishe. Nimekua mkubwa sasa I don't care nalipenda sana jina langu. Ndo nalitumia across all social media sina haja ya kujipa nickname coz it's already Unique.

Sent From Galaxy S9
 
Naomba kulifahamu 😍
 
We jamaa bhana

Sent using kidole gumba
 
Jina langu nalipenda sana, na nikiskia mtu anaitwa hilo jina hua natokea kumpenda ghafla!

Kwenye social networks pia natumia jina langu halisi, kasoro JF tu. Sijawahi tamani jina lingine lolote
 
Tuttyfruity
Lakini ni kwa mbinde, yaani ni baada ya kujaribu na kushindwa.... au ni baada ya kuaminishwa hizo attachments ndo ukaanza kuuona uzuri wa jina lako.

That’s the reality, wengi wetu tunapitia hayo at some point in our life.... hasa majina ya mizimu [surnames] ila ukiwa mkubwa ndo unaelewa.

Mimi vijana wangu nimewapa majina yao kama kawaida, ila cha ajabu hawapendi kujitambulisha kwa ‘Surname’ yetu ambayo sijui wanahisi ni ushamba.... furaha yao ni majina ‘mazuri’ hivyo wanataja jina lao na la baba [mimi] tu japo surname lipo kwa cheti.

Inaenda na umri na utambuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…