Ni kwa kiasi gani unaridhika na jina lako ulilopewa na wazazi wako?

Nalipenda jina langu ila lipo common kiasi na kupita mtaa mpya ukasikia mtu anaitwa sio kitu kipya, kwenda sehemu na usikute mtu anaitwa hivyo ni nadra zaidi ya nadra. Ila bado nalipenda
 
Mimi MKUU sijaridhika nalo,,,jina langu halisi ni KISIGINO..DOLE GUMBA..naona hata aibu nikitongoza mwanamke akitaka nijitambulishe....hakuna kitu nilijisikia VIBAYA kama shuleni wakati wa kuitwa majina..inaniuma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Shuleni nafikiri hii inaumiza wengi, ukizingatia hapo mnakuwa bado watoto hivyo ikifika jina lako kuitwa wenzako wote wanacheka.... ila ukikua ukiwa na hela utaitwa vizuri tu mzee. [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Jina langu nalipenda sana, na nikiskia mtu anaitwa hilo jina hua natokea kumpenda ghafla!

Kwenye social networks pia natumia jina langu halisi, kasoro JF tu. Sijawahi tamani jina lingine lolote

Hongera sana mkuu.
 
Nalipenda la kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…