Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?


Swali langu lilikua ni Kwanini viongozi wasiwe babu zako maana unasema walikua wengi je ni nini kiliwafanya wampe mwalimu uongozi. Inamaana kwa kipindi hicho hawakua na uwezo. Unasema Nacte ilikuwa inahujumu shule zenu na ushahidi unao, sasa unasita nini kuuweka hapa ili watu waone, umesema kulikua na hujuma basi unalojukumu la kudhibitisha hizo hujuma hapa. Leo ni 2023 bado mnahujumiwa kama mnavyo dai ni juzi tu matokeo yametoka bado mnashika mikia mixa mizero kibao kwene shule zenu na majina yenu.
 
 
KIKAO CHA KUUNDA TANU NYUMBANI KWA HAMZA KIBWANA MWAPACHU NANSIO, UKEREWE 1953

Ilikuwa miezi ya mwanzo ya mwaka wa 1953 kabla ya kufika April, 1953.

Abdul Sykes Act. President na Secretary wa TAA akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) walikwenda Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu.

Abdul Sykes alikuwa anataka kupata kauli ya mwisho ya Hamza Mwapachu kuhusu Julius Nyerere kuingizwa katika uongozi wa juu wa TAA kwenye uchaguzi wa viongozi wa TAA uliokuwa ufanyike mwezi April.

Uchaguzi ulifanyika kama walivyokubaliana watu hawa watatu na TAA ikawa chini ya uongozi wa Julius Kambarage Nyerere kama ilivyo hapo chini:

J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias, Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer, Ally K. Sykes Assistant Treasurer.

Committee members: Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo, Patrick Aoko.

(Tanganyika Standard 19 June 1953)
 
Unaweza ukasema maneno meng sana na unaweza ukaja na theory nying sana ila kuna kitu kimoja kinaitwa(lucky) bahati

Leo messi na C7 sio kwamba ndio wachezaji bora dunia nzima kwa miaka10 ila ni bahati

Unaweza ukawa bora sana au unaweza ukawa mzr sana ila km huna bahati ni kaz sana kufika mbali na watu weng wamefanikiwa sio kwa juhudi zao ila ni lucky bahati
 
Hiki Kiswahili anachoongea Mohamed Said,inaonekana hata wazee waliomsaidia Nyerere ndio walichoongea-kimejaa ujanja ujanja mwingi-endapo Nyerere angekaa nao bega kwa bega,hii nchi ingemshinda mapema-ilibidi kwa manufaa ya nchi apige upanga mapema
Kwani Nyerere hii nchi aliiweza? Siyo yeye aliyetuingiza kwenye umasikini mkubwa na yeye ndiyo chanzo cha ufisadi nchi hii.
 
Mkoko...
Ilikuwa unayajua haya?
 
kwahiyo Tanzania nzima mjuvi wa historia ya TANU ni wewe tu na ukoo wako? Mudi wacha urongo!

Prof.Haroub ni gwiji wa tafiti kuliko hivyo vipeperushi vyako.
 
kwahiyo Tanzania nzima mjuvi wa historia ya TANU ni wewe tu na ukoo wako? Mudi wacha urongo!

Prof.Haroub ni gwiji wa tafiti kuliko hivyo vipeperushi vyako.
Prof. Haroub ni mwalimu wangu.

Mimi kuijua historia ya TANU wala si jambo la kukuzwa.

Yeyote yule angezaliwa na watu hawa na katika kipindi kile angeijua historia ya TANU.
 
Ukifuatilia historia na harakati za Uhuru,unaona kuwa huyu kijana wa Kizanaki,mtoto wa Chief na "mvaa kaptula" alikuja baadae sana Dsm wakati wenzake wakiwa mjini kitambo na harakati za kumuondoa Mkoloni.Wakati Julius anakuja DSM tayari harakati za Uhuru zilikuwa zimepamba moto.


Pengine walikuwa waoga wa kutema madini...walikuwa wanaongelea vyumbani...alivyokuja Nyerere akaongea na kueleweka...kwani kule Zanzibar MAKOBAZI SI YALIJIFICHA mapaka JONI akafanya yake!!
 
Make...
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza Government Circular zilizokuwa zinatolewa na serikali kuhusu wafanyakazi wa serikali kujihusisha na siasa.

Inelekea huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mambo makubwa yalifanyika kuanzia mwaka wa 1950 hadi kuundwa kwa TANU mwaka wa 1954.

Yote yalikuwa wazi na wananchi wakishiriki.

Kuhusu Okello soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," utaijua historia ya mapinduzi.

Halikadhalika utamjua John Okello.

Ama hili la "makobazi," hii ni kejeli na kejeli haraka mjadala utaharibika kwani tutawakaribisha watu hodari kutukana kukushinda.
 
Sahihi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…