Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Kwani katika huo mstari ulio'quote' umeona sehemu yoyote ikikuzuia kuhoji chochote?
 
Sina shida na hiyo milango yako na ni kwa vipi inafunguka.
Kila mtu ana milango yake.
 
Wewe ni mpumbavu na una mitazamo duni sanaaa
 
Na mpaka leo hii asilimia kubwa ya watu wa ukanda huu pwani wengi haiwaijui Tanganyika vilivyo..Dunia yao ni ndogo sanaaa...samba na upeo wao...Sasa hawa wazee wetu akina mohamed said wanapowanywesha habar za chuki chuki na uongo uongo in the name of utafiti huku wakipalilia dini wao huwa wanaziamin kwel yani.
 
mudi nyota ya nyerere ni kubwa mpaka kiama haiwezi kuzimwa na vipeperushi vyako vya jf.Uwe unapenda ndo' hivyo,hupendi ndo' hivyo.
 
Ukweli wazee wengi hao unaowaita ni wamjini, elimu walikuwa hawana. Walikuwa wanaungaunga tu. Ujanja wa mdomoni tu
 
mudi nyota ya nyerere ni kubwa mpaka kiama haiwezi kuzimwa na vipeperushi vyako vya jf.Uwe unapenda ndo' hivyo,hupendi ndo' hivyo.
Luku...
Laiti ningeandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa nia ya kumdogosha Mwalimu Nyerere kitabu changu kingekuwa kimekufa miaka mingi na leo wewe usingeniandikia hapa JF.

Lakini sikunyanyua kalamu yangu kwa nia hiyo.

Niliandika kitabu cha Abdul Sykes (1998) kwa nia ya kusahihisha historia iliyokuwa imekwisha andikwa lakini ina makosa.

Kitabu kilipotoka kiliwavutia wengi kwa jinsi kilivyopishana na historia iliyokuwapo.

Kitabu hiki sasa kinakwenda toleo la tano.
 
Ukweli wazee wengi hao unaowaita ni wamjini, elimu walikuwa hawana. Walikuwa wanaungaunga tu. Ujanja wa mdomoni tu

ABBAS SYKES (1929 - 2021) SEHEMU YA TATU: KING'S COLLEGE BUDO SHULE MOJA NA KABAKA EDWARD MUTESA WA UGANDA 1940s

Siku moja katika mazungumzo na Balozi Sykes akaniambia kuwa yeye baba yake alimtoa Kitchwelle Boys Government School na kumpeleka Kampala Uganda kwa ajili ya kupata elimu.

Balozi anasema yeye hakuwa anajua ni shule gani baba yake alikuwa anataka kumpeleka lakini walipokuwa Nairobi wakiwa pale hotelini wakisubiri safari ya kwenda Kampala baba yake akakutana na jamaa wa Kinubi na katika maongezi baba yake akawaeleza kuwa alikuwa katika safari anaelekea Uganda kumpeleka kijana wake shule.

Basi mmoja wao katika wale jamaa wa Kinubi akamwambia Kleist kuwa shule nzuri sana ni King's College Budo kama ana uwezo na itakuwa vyema kama anatampeleka mtoto wake shule hiyo.

Hapo King's |College Budo ndipo Abbas Sykes ailipokuja kusoma na Freddie Mutesa ambae baadae akajakuwa Kabaka wa Buganda na Rais wa Uganda mwaka 1962 Uganda ilipopata uhuru.

Balozi Sykes anakumbuka kumuona mama yake Freddie Mutesa akiwa kavaa yale magauni ya Kiganda akija shule kumtembelea mwanae na jinsi shule nzima ilivyokuwa ikitetemeka kwa ujio wa bi. mkubwa yule kwani Freddie ndiye aliyekuwa akitegemewa kuwa Kabaka wa Uganda.

Wote Abbas Sykes na Freddie Mutesa katika utawala wa kikoloni wakahusika kikamilifu katika kupigania uhuru wa nchi zao.

Inasikitisha kuwa kutoka miaka ile ya 1940 wazalendo hawa hawakupata tena kuonana wakati nchi zao washazikomboa kutoka kwa Muingereza na labda kwa kuwa Kabaka Mutesa alipunduliwa mwaka wa 1966 na kwenda kuishi uhamishoni Uingereza ambako alifariki mwaka wa 1969.

Miaka hiyo Abbas Sykes tayari alikuwa kwenye ubalozi wa Tanzania Ufaransa na Canada.

Hii shule King's College Budo ina sifa ya pekee katika shule za Afrika ya Mashariki kwani viongozi wengi na watu mashuhuri wamesoma hapo kutoka Uganda kwenyewe, Kenya hadi Nyasaland na wenyewe wanajiita Budoians.

Hii ni ''club,'' pekee ya wasomi kama Yusuf Lule, Godfrey Binaisa na Charles Njonjo kwa kutaja majina maarufu katika siasa za Afrika ya Mashariki.

Balozi Sykes anamkumbuka baba yake kwa mapenzi makubwa sana.

Balozi mara nyingi akinambia kuwa, ''Sisi baba yetu alitujengea msingi mzuri sana wa maisha na alipofariki aliacha jina kubwa la ukoo wetu.

Hakuna mahali ambako baba yetu hakuacha alama yake kuanzia kwenye siasa, biashara na katika dini ya Kiislam hasa katika kuwasomesha watoto wa Kiislam wake kwa waume.

Yeye na wenzake akina Ali Jumbe Kiro walijenga ile shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Mungu akajaalia kuwa Bwana Abdul baada ya kifo cha baba yetu mwaka wa 1949 yeye akavaa viatu vya baba na vikamuenea vizuri sana ndani ya TAA hadi kuasisi TANU mwaka wa 1954.

Hapa ikawa tumekuwapo katika African Association mwaka wa 1929 na tukawepo katika kuunda TANU mwaka wa 1954.

Balozi akipenda sana kunitania kwa kuniita, ''Yaa Mohamed, unaiona Sykes dynasty?''

Nakumbuka siku nilipomtembelea baada ya Kleist Abdul Sykes kuchaguliwa kuwa Mayor wa Dar es Salaam.

''Unajua Mohamed somo yake alikuwa Mwafrika wa pili kuchaguliwa katika board ya Dar es Salaam Municipal Council kwa hiyo Kleist kafuata nyayo za babu yake,'' Balozi aliniambia kwa furaha.

Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa katika board hiyo alikuwa Juma Mwindadi.


Mwandishi na Abbas Sykes katika mahojiano ya kipindi cha televisheni 2012​
 
Kalamu,
Umeghadhibika.

Mimi na wewe tusitishe mjadala huu hadi baadae.
Dah!
Hizi mbinu za mijadala wengine tulishazisoma na kuzielewa siku nyingi sana.
Kiufupi ni kwamba hakuna "mjadala" kati yetu. Huwezi kujadili uongo, jambo ambalo ni batili.
 
Dah!
Hizi mbinu za mijadala wengine tulishazisoma na kuzielewa siku nyingi sana.
Kiufupi ni kwamba hakuna "mjadala" kati yetu. Huwezi kujadili uongo, jambo ambalo ni batili.
Kalamu,
Ingia katika historia ya Mwalimu Nyerere ndani ya kitabu chs Sykes uonyeshe uongo nilioandika.

Jopo la Prof. Shivji lililoandika Nyerere Biography wameisifia Maktaba yangu kuwa ni kati ya maktaba tatu zenye historia kubwa ya Julius Nyerere: Maktaba ya Brg. General Hashim Mbita, Dr. Salim na yangu.

Nina sababu gani ya kusema uongo?

Soma kitabu cha Mwalimu uone mara ngapi wamenifanyia rejea.
Nakuwekea picha nimeshika kitabu cha Mwalimu nilichopewa na Waandishi kwa mchango wangu katika kuwaeleza historia ya Mwalimu toka alkipofika Dsr es Salaam 1952 hadi alipostaafu urais mwaka wa 1985:



 


 
EeeenHeeee!

Unaji'promote' kwelikweli.

Katika kujiuza huna mfano wa kukufikia.

Tatizo ni kuweka chumvi nyingi katika baadhi ya mambo na kupotosha mengine kukidhi ajenda zinazokupa msukumo.

Sifa hii ya ku'exagerate' katika baadhi ya mambo, na kwingine kutunga uongo kabisa inaharibu taswira nzima ya unayoyasimamia.
 
Nyerere alikuwa nationalist na Pan-Africanist, kutakuwa na namna fulani "wazee wa Kariakoo" walikuwa wanataka kutanguliza maslahi mengine mbele juu ya yale ya kitaifa. Kwa Nyerere loyalty ya kwanza ni taifa, ungekuwa tofauti naye katika hilo ungepotea tu katika historia.
Sidhani pia kama wazee wa Kariakoo walikuwa wanaelewa mambo yoyote kuhusu Pan-Africanism, walikuwa kwenye league tofauti sana na Nyerere.
 
Jambo kubwa katika Taifa hili sio kupata uhuru tu. Wakoloni wasingedumu milele, Uhuru tungepata tu katika kipindi fulani kupitia yeyote kama nchi nyingine zote za Africa zilivyopata uhuru. Jambo kubwa zaidi katika historia yetu ni Utaifa imara unaotangulia mambo yote, ni Nyerere kuweza kutengeneza Taifa moja lisilo na migwanyiko ya kikablia, kikanda na kidini kutoka eneo lenye makabila mengi sana, kanda nyingi na dini kubwa mbili.

Hili sio jambo rahisi hasa ukitizama nchi nyingine ambazo zilikuwa na makundi kama haya ya kwetu. Hapo ndipo huwa namsamehe tu Mwl. hata katika blunders zake nyingine kama sera za ujamaa na ufutaji wa demokrasia ya vyama vingi.
 
Kalamu,
Ninapopokea barua ya mwaliko kuzungumza chuo fulani nani anampromote nani?

Anaealika au mualikwaji?
Nani amjengae mwenzie?


University of Ibadan International Conference on Terrorism 2006​
 
Yoda,
Isome historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kabla ya kuandika fikra zako.
Uhuru 1961.

Mwaka wa 1963 ndani ya Halmashauri Kuu ya TANU moto uliwaka:

''Wanakamati wawili wa Halmashauri Kuu ya TANU, Selemani Kitundu na Rajab Diwani, waliiomba Halmashauri Kuu ya TANU imjadili Aga Khan na nafasi yake kama patroni wa EAMWS.

Kitundu na Diwani walidai kuwa wana habari Aga Khan anataka kuitawala Tanganyika kupitia Waislam na EAMWS. Kwa ajili hii basi wakapendekeza EAMWS ifungiwe.

Nyerere aliwaunga mkono Selemani Kitundu na Rajab Diwani. Bibi Titi akasimama kishujaa dhidi ya Diwani, Kitundu na Nyerere, akasema hakuna kati yao aliyekuwa na haki ya kuifungia jumiaya yoyote ya Waislam.

Kama walikuwepo watu ndani ya EAMWS ambao walikuwa wanakwenda kinyume na sheria basi watu hao wapelekwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake.

Bibi Titi akaendelea na kusema kuwa EAMWS imekuwepo kabla ya TANU na siku zote imekuwa ikitoa huduma kwa Uislam.

Inasemekana hasira zilipanda na kukawa na kutoleana maneno kati ya Bibi Titi na Nyerere.

Bibi Titi akamwambia Nyerere yeye hamuogopi yeyote ila Allah.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)


Ofisi za East African Muslim Society (EAMWS) Mtaa wa Indira Gandhi​
 
Yoda,
Narudia kukueleza kuwa unahitaji usome kwanza historia ya uhuru wa Tanganyika kabla hujafanya mjadala.

Nakupa rejea za kusoma zikusaidie:

Jan P van Bergen, ''Development and Religion in Tanzania,'' (1981).

Dr John C. Sivalon, ''Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985,'' (1992).

Yaliyomo ndani ya vitabu hivyo nimeyaeleza katika kitabu cha Sykes kwa urefu na mapana yake.

Soma upate mshangao.

Vitabu hivi vimetolewa katika mzunguko madukani na Cathedral Bookshop kimya kimya.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…