Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Kalamu,
Ninapopokea barua ya mwaliko kuzungumza chuo fulani nani anampromote nani?

Anaealika au mualikwaji?
Nani amjengae mwenzie?

View attachment 2553028
University of Ibadan International Conference on Terrorism 2006​
EeeenHeeee!

Kama nilivyokuona pale Northwestern na kundi lile la waPakistan si zaidi ya kumi!

Hivi vikundi vya vyuo hivi ukawadanganye wasioelewa kitu.

Hivi ni vikundi tu vyenye 'interest' zao vinajipanga kumwalika mtu yeyote; chuo hakina uhusiano wowote na ualikwaji huo.
 
"Usinipuuze"! Ahaaaaa!

Haya unayoyaeleza hapa kuhusu "kujenga umoja wa kitaifa", ndilo wasilotaka kabisa kulisikia kundi hili la huyo mzee wa kidini.

Kulalamika kote kuhusu kutengwa wazee wao, kamwe hawawezi kukupaq sababu za Mwalimu kufanya hivyo, na kamwe asingefanya hivyo.
Hawawezi kukueleza hao wazee walikuwa na mwelekeo gani kidini na wenzao kutoka Mombasa. Haya kamwe hawawezi kuyaeleza.
Kundi hili ndio hawakubaliani na Bakwata, na hili ndilo chimbuko la kumlalamikia Mwalimu kuhusu dini ya kiislam.
Ingekuwa ni kufuata waliyotaka hao wazee, nchi hii wakati huu ingekuwa ni ya vurugu tupu.
 
 
Kalamu,
Kwa nini unatunga uongo ndugu yangu?

Unaijua Northwestern University?

Northwestern University ndiyo chuo kinachoongoza ulimwenguni katika African History.

Mkuu wa Department of African History Northwestern University ni Jonathon Glassman na tumefahamiana kwa miaka mingi akiniletea wanafunzi wake wa Ph D wakati wa kuandika Thesis zao.

Katika mmoja wa wanafunzi wake waliopita kwangu ni James Brennan kijana bingwa hivi sasa wa historia ya Tanzania na rafiki yangu ndugu kwa zaidi ya miaka 20.

Mimi nilialikwa University of Iowa na aliyenialika ni Prof. James Giblin ambaye nae ni Head of Department of African History chuoni hapo.

Jonathon Glassman yeye alinialika kuzungumza Northwestern University nikiwa University of Iowa.

Sasa haya ya Wapakistani sijui umeyatoa wapi.

Wala hukuwapo ukumbi wa Eduardo Mondlane ambao ndiyo nilipangiwa kuzungumza.

Lakini kwa kuwa umewataja Wapakistani nitakueleza wapi niliwaona Wapakistani na raia wa mataifa mengine ya Asia kama Wabangladesh.

Niliwaona vijana kutoka mataifa haya John Hopkins University Washington katika sala ya Ijumaa.

Vijana hawa ni mabingwa katika fani zao na Wamarekani wamewaleta nchini kwao wanufaike na elimu yao.

Taratibu ndugu yangu tutafahamiana.

Ungeniuliza ningekueleza huna sababu ya kujifedhehesha watu wakakujua kuwa wewe ni mtu muongo unaetaka kuvunja heshima za watu.

Kikundi cha Wapakistani kiniombee mimi visa ya kuingia Marekani?


James Brennan na Mwandishi, Kisutu Dar es Salaam

Prof. James Giblin akinionyesha kitabu cha Abdul Sykes
ofisini kwake University of Iowa
 
Sidhani kama vitabu hivi vitamuonyesha Nyerere hakuwa nationalist, labda tu kama unataka nivisome kujiongezea maarifa. Narudia tena kwa upana, kama kuna kundi lolote linaonekana kuwekwa kando au kutelekezwa na Nyerere sababu zilikuwa ni za maslahi na umoja wa kitaifa na baadaye kidogo ujamaa ukongezeka. Vyama/Makundi ambayo Nyerere aliona ni kitisho kwa hayo mambo mawili hakika alihakikisha vinapotea.

Huenda unaona historia ya wazee wako, baadhi ya vyama vyao na maslahi yao vilikuwa collateral damage kama vile ambavyo mimi naona mfumo wa vyama vingi ulivyofanyika collateral damage katika harakati za kuunda utaifa Imara pamoja na kuchangiwa na fikra za kijamaa, basi msamehe na muachilie tu Julius kutoka kwenye moyo wako kwa sababu hakuna shaka kwamba kama kuna kiongozi mmoja aliyeipenda nchi hii kwa dhati na watu wake wote na akawa mzalendo halisi kwayo bila agenda nyingine zozote binafsi ni Mwl. Nyerere.

Hata leo hii ungepata nafasi ya kuwauliza wazee wako kuhusu jinsi Nyerere alivyowachukulia hakika naamini wengi wao wangekuambia aliwapenda na hakuwa na hiyana au chuki yoyote dhidi yao.
 
Ahaaa, siwezi kukupuza mkuu katika suala la umoja wa kitaifa. Katika watu ambao sina shaka nao walipokuwa wanazungumzia umoja wa kitaifa na maslahi ya taifa hili ni Nyerere. Huyo mwamba aliyaishi maneno yake na hakuna mtu yoyote anaweza kuonyesha au kuthibitisha alitumia mambo hayo kwa maslahi yake binafsi kujinufaisha yeye au kundi fulani la watu wake.
Huyu Mzee Mohamed Said ni kama anajaribu kutuandikia historia mpya( rewrite history), haiwezi kukubalika.
 

Mzee tupe pdf zake.l
Mzabwa,
Sina bahati mbaya.
 
Yoda,
Huwezi kufanya mjadala ikiwa huna taarifa kamili la somo unalojadili.

Sikukuwekea rejea moja ya kitabu cha Prof. Hamza Njozi, ''Mwembechai Killings...'' (2002) kwa makusudi nilitaka uwasome hao kwanza.

Njozi katika kitabu chake ameeleza yale yaliyomo katika vitabu hivyo.

Serikali ikakipiga marufuku kitabu hiki kusomwa.

Ni kosa la jinai kuwa na kitabu hiki hapa nchini.

Ningeweza kukueleza mengi lakini ikiwa hujui vitabu hivyo vina nini ndani ni bora nisubiri kwanza hadi utakapovisoma.
 
Nijuavyo ni kwamba, Marais wengi kabla ya uhuru waliandaliwa na wakoloni kuja kushika dola, so hata nyerere alikuwa ni miongoni mwao ndio maana alikuwa na fame kuwazidi aliowakuta.
 

Yoda,
Nitakujibu moja tu katika hayo yote uliyoandika.

Nitakujibu kuhusu ''kuandika historia mpya.''

Hakika leo tuna historia mpya ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Leo tuna historia mpya ya Julius Nyerere tofauti na ile iliyozoeleka.

Historia iliyokuwapo ya Kimambo (1969) Ulotu (1971), na ya Chuo Cha CCM Kivukoni (1977) hivi sasa hakuna anaeweza kuwa na ujasiri wa kuisomesha tena si shule za msingi, sekondari au Chuo Kikuu.

Hakuna mwalimu wa historia anaeweza akamtanguliza Nyerere katika historia ya TANU akawaacha Hamza Mwapachu na Abdul Sykes.

Hakuna.

Hata baada ya kuandikwa kitabu cha maisha ya Nyerere: ''Nyerere Biography'' (2020) bado kitabu hicho hakijaweza kumweleza Nyerere vizuri katika kuunda TANU.

Nimekataa kukifanyia ''book review'' kitabu hiki ingawa watu wengi wameniomba nifanya hivyo.

Hakika hivi sasa watu wanasoma historia mpya.

Nilifanya mhadhara Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

Baada ya mhadhara nilielezwa kuwa katika wote waliopita hapo na kuzungumza historia yangu ya uhuru wa Tanganyika imewashangaza wengi kwani imepiashana sana na historia zilizozoeleka.

Mada yangu ilikuwa ''Tanzania: A Nation Without Heroes.''

Nilieleza kuwa Tanganyika ina mashujaa wake waliopigania uhuru lakini hawamo katika historia.

Nimehusika katika miradi miwili ya uandishi ya maisha ya Mwalimu Nyerere.

Angalia hapo chini:



 
 
Usiende huko kwa "kujua 'University'"; labda kama unataka kujifunza toka kwangu.
Hizi habari za kujifanya wewe mtaalam wa kuheshimiwa na vyuo mashuhuri duniani kwa kutunga hadithi usidhani kuwa ndio utaalam.

Kama nilivyosema huko nyuma, sifa pekee uliyojaaliwa kama kipaji ni huko kupamba habari ambazo sehemu kubwa ya habari hizo ni uongo.
 
Mwalimu Nyerere angekuwa ni mtu wa hovyohovyo, huyu mzee hapa angekuwa anatamba sana. Lakini kuhangaika kote anakofanya na kupotosha baadhi ya mambo hakuna hata sehemu moja ambayo ameonyesha ni kwa vipi Mwalimu Nyerere alivyowaonea hao wazee wake, au kuwabagua watu kwa sababu tu ya dini yao.
 
Kalamu,
Una joto ndani ya kifua chako.
Joto hili linakufanya ushindwe kufikiri sawasawa.

Mimi sijajifanya kuwa mtaalamu.
Vipi nitajifanya?

Utaalamu unahitaji elimu.
Kama sina elimu nitakuwaje mtaalamu.

Lakini mimi nimezungumza vyuo vikuu vingi: Zanzibar State University, IDM Mzumbe, Kenyatta University, University of Dar es Salaam, University of Johannesburg, University of Ibadan, University of Iowa, Northwestern University na kwengine kwingi.

Nimeandika vitabu kadhaa.

Nimefanya mahojiano mengi na TBC, AZAM, VoA, BBC, Radio Iran, DW, Online TV nyingi, FM Stations nyingi.

Nimefanya kipindi na Al Jazeera cha saa nzima wananihoji kuhusu historia ya Tanzania.

Lakini bahati mbaya sana kwako akili yako inakataa kuamini haya yote na kuona ukweli.

Umeshikilia kuwa mimi muongo.
Onyesha uongo wangu hapa watu wauone na mimi nikujibu.

Wewe ndiyo uliyezua uongo dhidi yangu kwa kusema kuwa nimealikwa Northwestern University na Wapakistani.

Unadhani kama wewe huwezi kualikwa Marekani nami pia sitakuwa na sifa za kualikwa.

Ukazidi kuongopa kwa kutaka kuwaaminisha wasomaji kuwa ulikuwapo Chicago siku mimi nazungumza Northwestern University, Evanston na ukaniona na Wapakistani.

Mimi nimekujibu tena kistaarabu kuwa mimi nilialikwa Marekani na wenyewe Waamerika.

Sikualikwa na Wapakistani.

Angalau kuwa na adabu na ustaarabu wa si kunitaka radhi mimi bali na wasomaji wanaokusoma.

Kujificha nyuma ya pazia isiwe sababu ya wewe kutukana watu.
Mimi niko hapa kwa sura na sauti yangu.

Sijifichi.

Sababu yake sijifichi nataka niaminike na kama yupo anaedhani mimi sisemi kweli anikabili hata uso kwa uso nimpe ushahidi nilionao.

Wengi wamefika nyumbani kwangu watu binafsi na taasisi,


Mahojiano na Al Jazeera

IDM Mzumbe

Mahojiano na TBC​
 
Kalamu,
Sina la kusema kuhusu mimi kutamba.

Lakini ikiwa maana ni kulitawalia jambo nashukuru nimetamba sana.

Wako ''publishers'' wameniomba kukusanya yote niliyondika nimewaruhusu.

Wameniambia kuwa kwa makisio yake nimeandika hapa JF makala 10,000.

Kazi inaendelea.

Kuhusu kuhangaika.
Sihangaiki hata kidogo na kwa hili namshukuru Allah.

Kwanza mimi ni mtu mzima sasa miaka 71.

Siwezi mihangaiko.

Zamani miaka kama 10 iliyopita wanaotaka kunihoji wakinialika studio.

Siku hizi na wao kwa kuniona nilivyochoka huniambia, ''Mzee Mohamed hapana shaka sisi tutakuja nyumbani kufanya kipindi chetu.''

Ikiwa unatafuta ukweli msome Bergen (1991), Sivalon (1992) na Njozi (2002).

Ukiwa huwezi kuvipata vitabu hivi soma kitabu cha Abdul Sykes sehemu ya tatu.

Wasomaji wengi wanasema hii ndiyo sehemu muhimu sana katika kitabu hicho:

Conspiracy Against Islam 1961-1970​

Chapter 10. The Muslim Factor in Post-Independence Tanzania 1961-1970
Islam: The Ideology of Colonial Resistance
The First Muslim Congress, 1962
Resistance to Change
The Second Muslim Congress, 1963
Proposal for an Islamic University, 1964
The Politics of Islam, Church, State and the African Christian
Chapter 11. The East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ‘Crisis’
Fomentation of the BAKWATA ‘Crisis’
Nyerere, Tewa, Bibi Titi Encounter, 1968
The Islamic National Conference, 1968
Omissions Analysed
Betrayal of Ideals
Conspiracy Theory
 
Usidhani ninao muda wa kupoteza kupitia takataka zote hizi unazoweka humu.
 
Unapoteza muda na kujaza tu kurasa humuJF.
 
mudi nyota ya nyerere ni kubwa mpaka kiama haiwezi kuzimwa na vipeperushi vyako vya jf.Uwe unapenda ndo' hivyo,hupendi ndo' hivyo.

Mudi ana chuki binafsi na nyerere,akae akijua wauza kahawa watabaki kuwa wauza kahawa tu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…