Kalamu,
Una joto ndani ya kifua chako.
Joto hili linakufanya ushindwe kufikiri sawasawa.
Mimi sijajifanya kuwa mtaalamu.
Vipi nitajifanya?
Utaalamu unahitaji elimu.
Kama sina elimu nitakuwaje mtaalamu.
Lakini mimi nimezungumza vyuo vikuu vingi: Zanzibar State University, IDM Mzumbe, Kenyatta University, University of Dar es Salaam, University of Johannesburg, University of Ibadan, University of Iowa, Northwestern University na kwengine kwingi.
Nimeandika vitabu kadhaa.
Nimefanya mahojiano mengi na TBC, AZAM, VoA, BBC, Radio Iran, DW, Online TV nyingi, FM Stations nyingi.
Nimefanya kipindi na Al Jazeera cha saa nzima wananihoji kuhusu historia ya Tanzania.
Lakini bahati mbaya sana kwako akili yako inakataa kuamini haya yote na kuona ukweli.
Umeshikilia kuwa mimi muongo.
Onyesha uongo wangu hapa watu wauone na mimi nikujibu.
Wewe ndiyo uliyezua uongo dhidi yangu kwa kusema kuwa nimealikwa Northwestern University na Wapakistani.
Unadhani kama wewe huwezi kualikwa Marekani nami pia sitakuwa na sifa za kualikwa.
Ukazidi kuongopa kwa kutaka kuwaaminisha wasomaji kuwa ulikuwapo Chicago siku mimi nazungumza Northwestern University, Evanston na ukaniona na Wapakistani.
Mimi nimekujibu tena kistaarabu kuwa mimi nilialikwa Marekani na wenyewe Waamerika.
Sikualikwa na Wapakistani.
Angalau kuwa na adabu na ustaarabu wa si kunitaka radhi mimi bali na wasomaji wanaokusoma.
Kujificha nyuma ya pazia isiwe sababu ya wewe kutukana watu.
Mimi niko hapa kwa sura na sauti yangu.
Sijifichi.
Sababu yake sijifichi nataka niaminike na kama yupo anaedhani mimi sisemi kweli anikabili hata uso kwa uso nimpe ushahidi nilionao.
Wengi wamefika nyumbani kwangu watu binafsi na taasisi,