Soul21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 210
- 351
Nyerere aliwahi kusema kuwa elimu ya msingi lazima ijikamilishe akimaanisha kuwa mwanafunzi akimaliza pale lazima awe na ujuzi unaotakiwa. Pia alisema elimu ya sekondari isiwe bomba la kupitishia watu kwenda vyuo vikuu bali lazima pia itoe maarifa toshelevu.
Sasa Kauli ya waziri mkuu juu wa wanachuo kijiunga na VETA haina maono mapana juu ya taifa linataka nini kwenye elimu.
Kitendo cha toka awali cha kuharibu mfumo wa Nyerere wa elimu ilifika mahali ikafanya elimu ya VETA ionekane ni ya watu walioshindwa.
Leo hii waziri mkuu anatoa kauli huku wakiendelea kujaza wanafunzi vyuo vya mipango ambapo kozi wanazosoma tayari kwa taifa zina fursa ndogo na wanajua hilo.
Jambo lingine huwezi kuwapuuza wasomi wa degree kwa sababu leo taifa lina watendaji toshelevu au linameshindwa kuajiri kutokana na uhaba wa mapato.
Bado tunahitaji mainjinia wa kutosha, madaktari na wataalamu wengi wenye elimu ya juu hivyo serikali inavyotoa kauli zake lazima ziendane na maono ya elimu ya taifa nasi kuongea hali ambayo inaweza kuchochea vijana kukosa morali ya kusoma na baadae tena upungufu ujitokeze
Mwisho kama wameona wanachina wanastahili miradi yote mikubwa basi wafute koz za degree.