Ni kwanini Akili yangu inazitafsiri hivi Tawala ( Awamu ) zote za Uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Wee ni kilaza huna hoja yoyote ya maana zaidi ya kutaka kumsema jk
 
Asante sana Baba yangu Karibu mno tu.
 
Anayezaliwa Kipindi cha Mkapa anawezaje kuona TV tena Kwao kabisa Mwaka 1983 Nyumba Jirani na Marehemu Former BOT Governor Mtani wangu wa Kihaya Gilman Rutihinda Oysterbay? Huna unachokijua Mkuu na ni bora ukanyamaza tu nisizidi Kukudharau.
Ahaaa miaka hiyo tunaenda kuangalia Tv kwa akina Tony acha uongo
 
Bila kuweka data hili bandiko ni UJINGA mtupu
 
huu ni mtazamo wako kama mwingine tu naye anayeweza kuja na mtazamo wake juu ya kila awamu....

Kila awamu iliongoza nchi kadili ilivyoona nchi ilipofika..japo wote walifail kwa kushindwa kuyajua kiuhalisia matatizo ya Tanzania na solution, wote walishindwa kujenga mifumo imara ikayoishi karne na karne na kuwa muongozo wa Taifa letu milele.. Wote walishindwa kujenga kizazi cha watanzania chenye uelewa na touch itakayokuwa kama alama ya utanzania...

Awamu ya kwanza tunaisamehe maana jukumu lake kubwa ilikuwa kututoa kwenye ukoloni, baada ya kufanikiwa kwenye hili ikashindwa kuweka muendelezo na kujenga misingi na mizizi imara kwa jamii ya kitanzania ambayo ingeishi mpaka leo baadala yake ikaacha issues dhaifu dhaifu ambazo zimekufa au kuuliwa kirahisi, Failure ya Taifa hili ndio ilianza hapa kwa Mzee Nyerere kwa kushindwa kuweka misingi imara itakayoishi na ingekuwa kama muongozo mpaka leo...

Awamu ya pili yenyewe ilikuja na mtazamo tofauti based na maisha iliyowakuta nayo watanzania, umasikini uliotukuka na mkwamo mkubwa wa kila mahala, nchi ikiwa imejifunga na hakuna kinachoendelea, wanannchi wakivaa matambala na kupanga foleni kwenye maduka ya ujamaa, nchi ilikuwa haina mipango yeyote ya kuendeleza Taifa vs population increase na kuendana sawa na kasi ya uchumi wa dunia..
Awamu iliamua kuleta sera au solo huria na kuifungua nchi iliyokwama na hapa watanzania kwa kiasi fulani wakapata mwamko na kuanza kuijua dunia na uelekeao wake japo elimu duni na wasomi wachache + ushamba wa watu kama moja ya athari ya awamu ya kwanza ukasababusha wahindi na waarabu kutuzidi akili kwa kuziwahi fursa na kutengeneza utajiri uliopindukia....Awamu hii ya pili iliamua kuwatoa watanzania tongotongo na kuifungulia milango na dunia kiasi cha maendeleo ya watu kuanza kushika kasi..

itaendelea..
 


✔✔✔💯%, we acha zama zile za giza.

Mzee Ruxa alipendwa mno na watz wote katika zama zile.
 
Wewe jamaa hata hueleweki yani!

Mara leo huku kesho kule yani upoupo tu. Wewe leo ni wa kumsifu Magufuli kiasi hiki bila kutoa dosari!?

Halafu kaneno kadogo tu lakini utakapamba wee mpaka basi mfano ni hiyo Rwanda ulivyoipamba hapo mpaka kukaribia kuleta chuki

Jambo lingine unapenda kujipamba na sifa kemkem za uzuri na uelewa, una katabia ka kujikubali na kujiona (kujichukulia kama) genius kumbe mbumbumbu fulani tu!

Mwisho; "genius create idea, average mind discuss idea, low mind discuss person"

Nimekuchambua wewe, utaangalia pa kuniweka katika makundi hayo!!!
 
Awamu ya tano ilikuwa ya kipumbavu na kijinga kuwahi kutokea.Ujenzi wa miundo mbinu michache siyo kibali cha kutekeleza ukatili,uhuni,wizi na uwongo dhidi ya wenye mtazamo tofauti na watawala waliojivika sifa batili za uzalendo. Mungu alisikia vilio vya waja wake ndiyo maana kamnyofoa Ibilisi na wafuasi wake wanahaha na kutamani dunia ipasuke! oLE KWA WALIOKUWA WANASHABIKIA UBAZAZI HUO. TUBUNI.
 
Uchambuzi uko vizuri mkuu, sema wengi wanaupitia wakiwa na mihemko.

Wanaishia kututajia maharamia waliojivika sura za utakatifu waliotekwa na wale wanaharakati uchwara waliokuwa wanatumiwa waliopata stahiki zao.
 

Awamu ya tano ilikuwa ni ya kiongozi dhalimu na muovu. Ilikuwa ni chini ya kiongozi mwenye mitazamo ya kijima. Kwa ujumla alipaswa kuwa kiongozi wa karne mbili nyuma, zilizokuwa zikitumia mabavu kuliko akili.
 
Ungetaka uchambuzi wako upate likes nyingi ungemchafua JPM! Kuna kakundi humu ndio kazi yake. Ila itafikia sehemu kakundi hako hako katapiga u turn ambayo kuna watu hawatoamini.
 
Yaani ufisadi wote ule wa kipindi cha serikali ya Mkapa ikiwemo EPA, Meremeta, deep green, Rada, Ndege ya Rais Kagoda, Uuzaji wa nyumba za serikali, Kujimiliksha mgodi Kiwira, Mikataba mibovu ya madini, uuzaji wa mashirika ya umma kwa bei sawa na kutupa halafu ufisadi huo uufumbie macho?

Awamu ya JPM ilikuwa awamu ya kuendesha nchi utafikiri familia binafsi, ilikuwa ni awamu isiyoheshimu nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, ilikuwa ni awamu ya kikatil nai uuaji, utekaji, kutoheshimu katiba wala sheria za nchi, Ilikuwa ni awamu inayonuka ukanda na ukabila. Ile Ilikuwa ni awamu mbovu kuliko zote,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…